Thursday 23 August 2012

[wanabidii] UJUMBE WA BODI ZA UTALII KUSHINDANIWA

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Sued Kagasheki amebadili taratibu za kuwapata wajumbe wa Bodi mbali mbali zilozoko chini ya Wizara. Kuanzia sasa Wajumbe wa Bodi hizo watapatikana kwa njia ya ushindani badala ya kuteuliwa moja kwa moja na Waziri.
Kwa sasa kuna Bodi nane (8) ambazo muda wake umeisha au unakaribia kuisha.Bodi hizo ni za za Taasisis/Mashirika yafuatayo;-
I. Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
II. Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI)
III. Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI)
IV. Makumbusho ya Taifa
V. Chuo cha Mafunzo na Usimamizi wa Wanyamapori (MWEKA)
VI. Chuo cha Mafunzo ya Wanyamapori Pasiansi
VII. Wakala wa Mbegu za Miti (TTSA)
VIII. Bodi ya Leseni za Utalii (TTLB)
Watanzania wenye sifa za kuwa Wajumbe wa Bodi hizo wanatakiwa kupeleka maombi kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii.Maelezo zaidi ya namna ya kupeka maombi yataweka kwenye magazeti na tovuti ya Wizara  www.mnrt.go.tz 

NB: BOFYA HAPA KAMA UNAHITAJI KUOMBA NAFAZI ZA UJUMBE WA BODIwww.mnrt.go.tz

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment