Monday 27 August 2012

[wanabidii] UBORESHAJI WA DODOSO LA SENSA

Kwanza niseme ya kuwa mie mwenzenu nilihesabiwa jana
majira ya saa sita mchana. na karani ambaye hakuwa na kitambulisho wala t-shirt
ya kumtambulisha kama ilivyokuwa inatangazwa na vyombo mbali mbali vya habari.
Ndg zangu wanabidii ili kuboresha dodoso la sensa kwa miaka ijayo binafsi
nilikuwa napendekeza takwimu zifuatazo ziongezwe
1. umbali kati ya makazi hadi chanzo cha maji
2. umbali kati ya makazi na huduma za afya
3.Wastani wa Kipato cha mkuu wa kaya kwa mwaka
4. Umbali kati ya makazi na shule

kwangu mimi hizi ni baadhi ya nyanja ambazo kama tunaongelea
mipango ya maendeleo ni lazima tuelezee vigezo vinavyohusiana
na maji, afya, kipato na shule tofauti na hivyo lengo la sensa
litakuwa tofauti na takwimu zinazokusanywa

nawasilisha

0 comments:

Post a Comment