Wednesday 8 August 2012

[wanabidii] Re: MAFANIKIO KUELEKEA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE

HUU NDIO UJUMBE ULIOTUMWA DECEMBER 2010

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Dr. Donath R.Olomi" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>
Date: Thu, December 16, 2010 9:37 pm
To: many groups/individuals by email
--------------------------------------------------------------------------

Salaam

Nimekuwa nafuatilia jinsi desturi ya kuchangia na kufanya sherehe
kubwa
inavyozidi kushika kasi, ikipelekea ule wigo wa kuomba michango
kupanuka
kiasi kwamba sasa hata mtu ambaye jina lako halijui vizuri anaweza
kukuomba mchango.

Aidha michango na sherehe hizi zimekuwa mzigo mkubwa sana kwa baadhi
ya
watu, ikiwa ni pamoja na wale wenye kipato kidogo wanaochangiwa na
kulazimika kulipa michango hiyo kwa miaka mingi. Je, wajua kuwa kuna
familia ambazo zimefikia kulazimisha ndugu wauze mashamba au mifugo
mtaji
ili kupata fedha za kuchangia sherehe?. Je, wajua kuwa kuna watu ambao
zaidi ya nusu ya kipato chao wanatumia kuchangia sherehe na huku
wakishindwa kulipia huduma muhimu kama shule, matibabu, lishe, nk. Na
kuwa
wakati mwingine wewe au mimi (au wengine kama mimi na wewe) ndio
wenyeviti
na makatibu wa sherehe hiyo?. Na ni sisi tunaoona fahari ya kutumia
milioni 30 au zaidi kwenye sherehe usiku mmoja?

Kuna kijana mmoja jamaa yetu juzi juzi alipata shule Australia akawa
anatafuta mchango wa dola 5,000 aende. Alipata 2,000 na amwekwama
kwenda.
Mwaka kesho akisema anaoa tutamchangia milioni 15-20!!!. Hii si
hadithi,
ni ukweli, na ni kielelezo cha ulimbukeni tuliofikia.

Siku za karibuni nimetambua kuwa kuna kundi kubwa tu linasikitishwa na
huu
mwenendo, na hata kutambua kuwa tunaweza kuwa tunaandikiwa dhambi
kubwa
(na hukumu yatusubiri) kwa jinsi wengi wetu tunashindwa kusaidia mambo
ya
msingi lakini tunakuwa wepesi kutoa kwenye sherehe. Wengi wanaamini
kuwa
tumeshatumbukia kwenye lindi la mazoea ambapo hatuwezi kujitoa mpaka
upepo
uje ubadilike wenyewe!.

Mimi nafikiri wasomi tuna jukumu muhimu la kuwa chachu ya mabadiliko
pale
ambapo mazoea yenye madhara yanavuka mipaka na kuweza hata kuwa chanzo
cha
ufukara na kuviza maendeleo.

Ili kubadilisha hili jambo, lazima tuanzie mahali. Mimi napendeleza na
kuanza kutekeleza. Kuanzia Januari 2011, nitapunguza michango
ninayotoa.
Nitatoa tu kwa mtu wa karibu sana, na nitachanga kidogo. Usishangae
nikakuchangia 20,000/= kama ulitegemea 50,000/= kwa mfano. Kuanzia
July
2011, nitaacha kabisa kuchangia sherehe. Badala yake nitakuwa
nachangia
elimu pale ambapo mzazi hayupo au mhusika kweli hana uwezo na pia
nitachangia miradi mingine ya jamii na maendeleo.
Je waniunga mkono? Kama ndiyo sambaza huu ujumbe kwa mtandao wako.


Dr. D.R.Olomi
Box 35036 Dar es Salaam, Tanzania

HAYA NDIYO MAJIBU NA MAONI YA WASOMAJI WALIOCHANGIA HUU MJADALA.
SIJABADILI KITU ILA KUPUNGUZA IDADI YA WALIOPELEKEWA KUPUNGUZA UREFU
WA HAYA MAKALA

ONA MWENYEWE WENGI WANAVYOSEMA ILI UNAPOGAWA KADI ZA MICHANGO UJUE
KUNA WENGI ROHONI WANAUMIA SANA



-----Original Message-----
From: Suleiman Stima
Sent: 17 December 2010 20:23
To: Lilian Mahimbo; Ladislaus Mrope; Mwangalimi Kiwonde; Ibrahim
Chuma; Mwanakombo
Joshua; Bakiri Thabit; Ramadhan Lesso; Aziz Chakoma; Albert Lecuu;
Emmanuel.Hamaro@nbctz.com; Fardus Mohamed; George Njunde; Godfrey
Mabonye; Hellen
Mushi; John Nyaindi; Adam Mihayo; Mussa Mbassa; Omari Basheikh
Subject: FW: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE

Dr. Olomi,
You are more than 100% right!! I will circulate this message to as
many people as possible and I have also determined to follow your
footsteps on this as from January 2011!

STIMA, S. H.
BRANCH MANAGER,
NBC LTD, P. O. BOX 40, NJOMBE.
Subject: RE: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Stanley Ndanshau" <Stanley.Ndanshau@nbctz.com>
Date: Mon, December 20, 2010 5:48 am
To: "'olomi@imedtz.org'" <olomi@imedtz.org>
--------------------------------------------------------------------------



---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: ceo@eastc.ac.tz
Date: Mon, December 20, 2010 12:04 am
To: olomi@imedtz.org
Cc:
--------------------------------------------------------------------------

Dear Olomi and all,

Kwanza nishukuru kwa nyaraka zako mbili ambazo nitasoma punde tu.
Swala la sherehe za harusi lina nafasi tatu moja ni send off, pili ni
kitchen party na tatu ni harusi yenyewe. Biashara hii inalete tena
kitchen
party ya wanaume na hii itakuwa ya nne.

nakubaliana na wewe kwamba tupunguze halafu tuache kabisa na kwamba
tujali
elimu, elimu na misiba.

Inashangaza tu kwamba tuna nymba zetu tunaziacha tunaenda kukodisha
nyumba
za watu na tunazipamba kwa gharama kubwa tu. Mbona wakati wa misiba
tunaenda kwa mfiwa na kukaa pale hata kama pakoje? Tunaweka maturubai
kwa
nini tusiyachukue wakati wa harusi tukaweka kwa mwenye harusi na ile
hele
ya mapambo tukarekebisha nyumbani pa mwenye shughuli? Mimi naona
tunaenda
bila kufikiri. Mapesa mengi yanatumika kulipia na kupamba majengo ya
watu
kwa saa tatu tu.

Mimi naanza kubadilika na kuwaeleza watu waziwazi.

Michael P. Sindato

-------------------- Original Message ----------------------------
Subject: FW: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Masumbuko Myaga" <Masumbuko.Myaga@nbctz.com>
Date: Sat, December 18, 2010 3:50 am
To: "olomi@imedtz.org" <olomi@imedtz.org>
--------------------------------------------------------------------------
From: Masumbuko Myaga
Sent: 18 December 2010 10:47
To: olomi@imedtz.org
Subject: RE: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE

Inabidi waTanzania sasa tufunguke akili maana hapa tulipofikia
sasa panatisha mimi binafsi niko sambamba kabisa pamoja na wewe.Watu
wanaingia tamaa ya kufanya masherehe makubwa yenye kushindana kwa
kutegemea viwango vikubwa vya michango toka mifukoni mwa watu wengine
hata kwa kulazimishana,
sasa hivi shida ni nyingi,kuna watu wanaoguza,matatizo ya ada ya
shule,magumu ya maisha nk. ila wao wanachoangalia ni starehe ya siku
moja tu.

nbc ltd,morogoro
another e-mail address: justmyaga2007@yahoo.co.uk
asante Dr.olomi

________________________________________
From: Mathias Mhangilwa

Ndugu zangu,
Nadhani tulichelewa kuanza.Sasa tuanze kukataa michango hiyo.Na
inapobidi mtu afanye
sherehe husika kwa kadri ya uwezo wake.

Jamani tupo hapo.

Job Nshatsi
Branch Manager|Kibaha Branch|NBC Ltd|P.O Box 30200
Kibaha|Office:+255232402217|Fax:+255232402253|Cell:+255767434304|Email
Job.Nshatsi@nbctz.com|Website:www.nbctz.com
________________________________________
From: Geoffrey Ndossa
Sent: 17 December 2010 17:36
To: Job Nshatsi; Jasson Shumbusho; Ashura Waziri; Abdallah Chimgege;
Salema;
Alphonce Musiba; Loiruck Mollel; Godhard Hunja; Consolata Henjewele;
Salma Yatera;
Salim Rupia; Said Kilala; Jane Dogan
Cc: olomi@imedtz.org; olomi@imedtz.org
Subject: RE: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE

Ndugu zangu,
Naunga mkono msimamo huu, kwani hata mahala pengine ndugu au rafiki
anaugua
anatafuta tu hela kidogo kama laki kadhaa au milioni moja za matibabu
lakini hapati na hakuna ushirikiano wala mkakati wa dhati kuona
tunamsaidia. Tena mbaya zaidi anaonekana kama ombaomba tofauti na pale
aombapo mchango wa arusi au sherehe ya ubatizo/kipaimara ya mwanae.
Zaidi sana hata huyu mgonjwa hatuko tayari kumsaidia katika matibabu
lakini akishafariki kwa sababu ya kukosa matibabu ya hela ndogo tu
basi tuko tayari na kwa haraka haraka kuchangia mazishi. Jamani ndugu
zangu tubadilike na tuielimishe jamii yetu kuona mambo muhimu na ya
msingi yapasayo kusaidiana kama jirani zetu wa hapa Kenya wafanyavyo.

W i t h r e g a r ds ,
Geoffrey W. Ndossa
Branch Manager; NBC LTD Kichwele Branch
Mob +255 767 210325, l direct 022 2116948 l fax 022 213 8571
e-mail: Geoffrey.Ndossa@nbctz.com === Website:www.nbctz.com
'The essence of quality time is how much VALUE you get out of it
rather than how
much chronological you put in it'

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: RE: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Abdallah Chimgege" <Abdallah.Chimgege@nbctz.com>
Date: Fri, December 17, 2010 11:32 am
To: "Geoffrey Ndossa" <Geoffrey.Ndossa@nbctz.com>
Cc: "olomi@imedtz.org" <olomi@imedtz.org>
--------------------------------------------------------------------------

Hi all.

Nimeguswa sana. Hili ni jambo la kiroho. Tukiacha au kupunguza
michango mikubwa ya sherehe tutakuwa tumepunguza pia uharifu na
matatizo mengine egemezi kama uenezwaji wa magonjwa n.k

Kumbe basi kutoa michango mikubwa ya sherehe ni kuharibu rasilimali na
kwa hiyo kumchukiza mungu.

Hatujachelewa, let us start a new ending

Allah bless u all

Abdallah
NBC Limited|Masasi Branch|Phone:+255232510771|Fax+255232510773|cell:
+255767210649
Think before you print this e-mail. Save costs. Every little helps

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: MICHANGO YA HARUSI
From: "Ezekia Mwambwanje" <Ezekia.Mwambwanje@nbctz.com>
Date: Tue, December 21, 2010 2:52 am
To: "olomi@imedtz.org" <olomi@imedtz.org>
--------------------------------------------------------------------------

NASHUKURU KWA MAWAZO YAKO
KWANI WATU TUMECHANGANYIKIWA NA MAMBO YA KUIGA BILA KUJALI KIPATO
CHAKO

UMENILENGA NA UMENIBADILISHA ASANTE


Important Notice:

The National Bank of Commerce Limited is a registered Commercial Bank
in the United Republic of Tanzania.

This e-mail and any files transmitted with it are confidential and
intended for the use of the individual or entity to whom they are
addressed.
---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: RE: Fw: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "AUDAX TIBUHINDA" <tibuhinda@yahoo.com>
Date: Mon, January 10, 2011 7:45 am
To: krchurch@googlegroups.com
Cc: "nsafari@hotmail.com" <nsafari@hotmail.com>
"olomi@udbs.udsm.ac.tz" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>
"imuro@eandco.net" <imuro@eandco.net>
--------------------------------------------------------------------------


Huu ni mjadala wazi Ndg Msangi hivyo kila mmoja aweza kutoa mawazo
yake kwa mtazamo wake ili mradi maadili ya mawasiliano yamezingatiwa.

Kimsingi hili ni suala la kimfumo kutokana na kuota mizizi ndani ya
jamii hata "mind-set" iko hivyo. Kwa upande wangu dhana nzima ya
kupunguza michango ya arusi (sebure party, kitchen party, send off,
arusi yenyewe) naiunga mkono kwa asilimia kubwa. Wenzetu Kenya kama
ilivyoelezwa dhana ya uwekezaji na marejesho yake (rate of return)
imewakaa vizuri pia suala la kuokoa maisha ya watu. Nafikiri neno
watanzania ni wakarimu na wanaushirikiano linaweza lisiwe na usahihi
wakati mwingine, wakarimu kwa kutatua tatizo gani? Wakati umewadia
tuanze kushughulikia huu mfumo ambao unatumia pesa nyingi sana na
kulazimisha wachangiaji kushindwa kutimiza malengo ya kimaendeleo na
hata kuchangia huduma na maendeleo ya kikanisa kwa mfano.

Hili ni suala la mabadiriko ambapo kwa kawaida mabadiriko yanakumbana
na vikwazo (resistance). Hata kama kihistoria waliotutangulia
walichangiwa lakini tunaweza kujenga hoja na haja ya kubadirika kwa
wakati huu. Tuchukue hatua.

Tibu

--- On Sun, 1/9/11, Mathias Godfrey <Mathias.Godfrey@tigo.co.tz>
wrote:


From: Mathias Godfrey <Mathias.Godfrey@tigo.co.tz>
Subject: RE: Fw: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
To: "krchurch@googlegroups.com" <krchurch@googlegroups.com>
Cc: "nsafari@hotmail.com" <nsafari@hotmail.com>,
"olomi@udbs.udsm.ac.tz" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>, "imuro@eandco.net"
<imuro@eandco.net>
Date: Sunday, January 9, 2011, 4:01 AM

Wapendwa Bwana Yesu asifiwe;nakubaliana na hoja ya msingi iliyopo
mbele yetu lakini ninachokiona ni kile kipaumbele na muitikio katika
mambo yote.Binafsi kwa mtazamo wangu naona yote yana umuhimu kwamba
yanahusisha jamii kwa ujumla ikiwa ni pamoja na familia,ndugu jamaa na
marafiki.Kwa hiyo sioni kama inawezekana kuacha kabisa isipokuwa
tunapofanya jambo lolote tufanye kwa moyo na kwa nafasi iliyopo lakini
la msingi zaidi kuangalia kipaumbele kwa wakati ulionao.Mimi binafsi
wasi wasi wangu ni kwamba kama nitaitisha ndugu wa kuzaliwa kwenye
familia peke yao na kuishia hapo nitakuwa na watu wengi walio karibu
nikiwaacha au vinginevyo mnamaanisha niwajibike kugharamia na
kuwakaribisha,waswahili wanasema sherehe ni watu na watu wenyewe ndio
ikina nyie.Halafu pia naomba tusiwe wasahaulifu wengi wetu
tumeshapitia hatua hiyo na ninyi ni mashahidi wa mlichokifanya na watu
wengine walihusika kikamilifu.Najaribu kuweka angalizo tusije tuka
kata tamaa na kuacha
kabisa pasipo kuwatia moyo vijana ambao wana maono na maono yao
yakapotea kwa sababu ya hofu.Kipaumbele katika mabo yote ni jambo la
msingi pamoja na kuwa na kuwa na kiasi tunaweza kuyatimiza mambo yote
kwa ukamilifu.Swala la kuchangia elimu ni mfumo ambao unamtazamo hasi
kwa jamii ni wajibu wetu kuielimisha jamii faida na matokeo ya
uwezweshaji kielimu kwenye jamii.

Samahani kama nitakuwa kinyume lakini huo ndio mtazamo wangu.

Bwana awabariki

Mathias G. Msangi


From: krchurch@googlegroups.com [mailto:krchurch@googlegroups.com] On
Behalf Of George Wandwalo
Sent: Saturday, January 08, 2011 11:28 AM
To: krchurch@googlegroups.com
Subject: Re: Fw: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE


Nina waslimu nyote kwa jina la yesu na Heri ya mwaka mpya 2011 wenye
strategies kibao kimaisha na kiroho.


Ningependa zaid kumunga mkono Dr Olomi kwa hili swala la Michango ni
kweli ina bidi liwe na mwisho maana tuna utofauti mkubwa na jamaa zetu
wa kenya, na ndo maana wako mbele kitaluma maana wao hakuna mtu
atakuchangia mchongo wa harusi ama sherehe labda close relatives na
lazima wewe uwe na mtaji kwanza inakuwa kituko ukisema unaitaji
mchango wa arusi maana hii nia yako binafsi ila ukisema mtoto amekosa
school fees kila mtu atatoa hata kuku ama umelazwa umekosa pesa
hospitalini watachangia hata "chief" atahusikia kuitisha harambee ili
mtoto aende shule ama kuokoa maisha ya mlipa kodi! maana wansema
ukisomesha atakuja kuisadia nchi yake ama siku mmoja ata saidia
mwanainchi mwenzake je Harusi ama sherehe ni ya mtu binafsi! nadhani
swala hili linabidi litafutiwe mbinu mbadala

na mbinu hiyo ni kuanza kupunguza kiwango cha michango ama kutoa pale
pana po gusa na hatimaye dhana itafutika vizazi vijavyo kwa kweli
ukijumlisha overhead expenditure ( Cost unit ya sherehe na arusi)
inachukua percentage kubwa na wakati mwingine una shangaa labda hata
kibanda fulani ungekuwa umemaliza, tufungue macho, michango hii
tukaelekeza kijamii kama kanisani nadhani itafanya kazi kubwa zaidi.

2011/1/5 apasaa nuru <apasaa3@yahoo.co.uk>






--- On Mon, 3/1/11, Benson Mahenya <bmahenya@yahoo.com> wrote:

From: Benson Mahenya <bmahenya@yahoo.com>
Subject: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
To: "'Elizabeth Ngoye'" <elizabeth.ngoye@eandco.net>, ETC
Date: Monday, 3 January, 2011, 8:40


I support!
In the next 2 weeks you will read/hear from me on this topic.
Happy New Year.

Kind regards,
Benson Mwasaga Mahenya
Director - ACG/Tanscott CPA

UMATI Building, 3rd Floor
Samora/Zanaki Street
P. O. Box 63214
bmahenya@acgtz.com

www.acgtz.com
Think this is the best resolution, at least watu watafanya sherehe
ambazo
zipo ndani ya uwezo wao tu au harusi itaanza kuwa ni kwa ajili ya
ndugu wa
karibu tu....

---------- Forwarded message ----------
From: neema mogha <moghang@yahoo.com>
Date: 2011/1/7
Subject: Fw: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
To: David Kacholi <kacholi78@yahoo.com>, David Kacholi
<dkacholi@duce.ac.tz>,
Luba Pascoe <lubapascoe@yahoo.com>, clotide mathew
<clotidemathew@yahoo.com>,


Mimi nimevutwa sana na huu ujumbe kwani ndio kitu ambacho kila
siku
kinaniumiza. Sasa na wewe soma halafu fanya maamuzi ya kuchangua
upande
unaopendelea. kila laheri na siku njema
Neema


---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Anthony Kaijage" <akaijage2003@yahoo.com>
Date:
--------------------------------------------------------------------
Bwana Sambua na Olomi.
Kwanza Heri ya Mwaka mpya?
Ujumbe wenu bahati mbaya nilichelewa kuupata kutokana na sababu zilizo
nje ya uwezo wangu. Ninakushukuru Bw. Sambua kwa 'mail' yako,
umeniunganisha tena na rafiki yangu Bw.Ntengua Mndoe, tuliyekutana
mara ya mwisho miaka ya tisini tukiwa Wakurugenzi  Waanzilishi wa
CRDB Bank( a very big surprise to him also I presume?) Kwa mail hii
ninamwomba tuanze tena mawasiliano. Kuhusu ujumbe wenu, ninauona si tu
ni ushauri wa kawaida tu bali ni muendelezo wa elimu ya Ujasiriamali,
nyanja ambayo Bw. Olomi na mwenzangu Bw. Sambua (sijui wengine
samahani?) na mimi pia, tumebobea? Ninaliunga mkono asilimia mia moja!
Mnajua ndugu zangu, baada ya miaka hamsini ya Uhuru, Wasomi tuache
kuendeleza tabia ya 'lip service' bila matendo! Taifa limetusomesha(au
hata kama tumesomeshwa na wazazi)
tuanze kuchanganua vyanzo vya Mtanzania kuendelea kuzama katika dimbwi
la umaskini wa kujitakia, kama michango ya sherehe?
Mimi pamoja na kuwa tayari kusambaza ujumbe huu nina pendekezo:
TUAZNZISHE MTANDAO RASMI AU CHAMA CHA HIARI CHA KUPIGA VITA TABIA HII
YA MICHANGO.
Naona tayari idadi inatosha, na Mwenyekiti wake wa kwanza awe Dr.
Olomi nk..Baada ya hapo tuandae Workshops za kuandaa 'Facilitators' na
ndipo kazi rasmi ya kuhamasisha jamii ianze?
 Nadhani kitu hiki kinaweza kupata 'support' ya Serikali na pia
'Non- State Actors', mnaonaje jamani? Liwezekanalo leo kwa nini
lingoje kesho?
Anthony Kaijage,
Mhadhiri, St.Augustine University of Tanzania-Mwanza.

--- On Fri, 12/31/10, Sosthenes Sambua <ssambua@tpsftz.org> wrote:


From: Sosthenes Sambua <ssambua@tpsftz.org>
Subject: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
To: "'Dr. Donath R.Olomi'" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>, "'Ntengua Mdoe'"
<nmdoe@yahoo.co.uk>


Dr Olomi,

Nimepata ujumbe wako kwanza kwa sms na pia kwa email baadae. Binafsi
Nimejaribu kufanyia kazi jambo hili miaka matatu iliyopita. Katika
familia yetu binti yetu alikuwa anaolewa na na mchumba wake hakuwa na
uwezo wa kuchangisha fedha nyingi. Sisi tukatafakari na kukubaliana
kwamba kati ya send off na harusi ni harusi ambayo ni muhimu sana.
Haya mawili ni matukio ya mpito (passage rites) za tangu enzi na enzi.
Tukaamua tutamtoa binti yetu kama zamani yaani mshenga na wazazi wa
kijana wakaja nyumbani kwetu hapa Dar tukakaanga nyama kilo 10 na bia
kreti 5 na soda kreti 4. Tukacheza mduara na ndombolo na tukapiga
mndoro na kadhalika. Pia majirani walioshiriki na wazee wa mtaani
kwetu.

Michango tuliyoipata tukafanya sherehe moja ya harusi iliyosimamiwa na
familia zote mbili. Hapakuwa na mashindano ya ni familia ipi imekuwa
na sherehe kubwa kuliko nyingine. Hizi familia mbili zimeungana kwa
hali na mali. Full stop.

Katika hili ulilopendekeza Nakubaliana kwamba tupeleke nguvu nyingi
kwenye maendeleo zaidi ya sherehe ambazo mchango wake kwa maendeleo
yetu ni kidogo tu. Tunawanufaisha wenye ukumbi, ambao sasa wamehodhi
kila kitu, kinywaji, chakula, mapambo yote kwa mtu mmoja. Huu si
ujasiriamali hata kidogo.

Elimu yangu ya chuo nimesoma Kenya kwa miaka takribani 7 hivi. Kule
watu hufanya harusi na pia hupeleka watoto shule. Baada ya ndoa
kufungwa watu hukaa kwenye ukumbi na kula ugali na wali na soda.
Wakacheza ngoma zao na kutoa zawadi. Baada ya hapo kuna inner party
(kwa wale wenye umri kidogo mtakumbuka inner party) ambapo wachache wa
karibu huwasindikiza maharusi nyumbani na kusheherekea tukio la
kuoana. Hawa huendelea kusheherekea hadi maharusi wanapoingia
kupumzika na kukamilisha ndoa.

Huko Kenya kuna harambee nyingi sana zinafanywa ili kuchangia watoto
waende kusoma shule za upili (sekondari) na vyuo vikuu hasa Uingereza
na Australia. Harambee hizi hutangazwa kwenye redio, magazeti na
runinga. Jirani zetu wanasomesha watoto wao kwa wingi kwa mtindo huu
tangu miaka ya 90. Sisi tumelala. Jirani yetu Kagame anampango kabambe
wa kusomesha watoto wa Rwanda ili waje kutawala soko la ajira Afrika
Mashariki. Sisi tutalala mpaka lini? Tutawanchagia wenye ukumbi mpaka
lini?

Mimi Naungana nawe kusambaza ujumbe huu na pia kupunguza Kiwango cha
michango kwa miezi 6 ijayo. Hii itakuwa kama notisi kwa ndugu, jamaa
na marafiki. Tufanye harusi pasipo kumkufuru Mungu. Wenye harusi yao
wakiambua kufanya sherehe kubwa wana hiyari kwa uwezo wao lakini
tusikope kuwachangia. Tukope kusomesha watoto au kujenga shule au
kujenga daraja.

Sambua

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: Fw: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "nixon matowo" <mlungwe@yahoo.com>
Date: Thu, January 6, 2011 1:44 am
To: "Benjamin Swai" <bmswai@yahoo.com>
nsafari@hotmail.com
Cc: olomi@udbs.udsm.ac.tz
--------------------------------------------------------------------------
Ndugu ulomi nakuunga mkono asilimia 105.wajua ilibidi Yesu aje ili
watu waokolewe na dhambi zao.naamini mawazo yako sio ya mwilini ni ya
rohoni kabisa.na hii tabia sio ulimbukeni ni ujinga na ukosefu wa
maarifa.watu wanachangia kitu wanachoona kina returns up front.kama ni
harusi watakula na kulewa.lakini sio kwa vitu ambavyo faida yake ni ya
muda mrefu na ina affect jamii za sasa na zijazo.pse songa
mbele .ujumbe na mie nasambaza.kitu cha ajabu huku kwa wenzetu
waliotuzidi kimaendeleo kwa maswala ya kijamii hawachangishi hela kwa
ajili ya sherehe.never.kama ni harusi ni busines yako mwenyewe.wata
support vitu vya kimaendeleo vinavyogusa jamii kwa ujumla sio ulaji na
unywaji.Pia ubinafsi nao unachangia sana.watu tunapenda maendeleo yetu
sisi wenyewe tu bila kujali watu wengine.sijawahi kusikia mtu amekuwa
maskini au wattoto wake wakakosa chakula kwa sababu alisaidia
mhitaji.kuna watu watainuka na kuwa watu wa maana sana hapa duniani
lakini ili wafikie
lengo hilo ni lazima kuwe na watu wa kuwasaidia.mimi na wewe ni
mmojawapo wa hao watu wa kuwasaidia watu wahitaji ambao hawana
uwezo.ukiweka hela bank riba yake unapata kidogo sana.lakini amsaidiae
maskini amemkopesha Mungu.Fikiri kwa kiwango cha kimungu kama Mungu
akirudishia atakurudishia kiasi gani.Maana ni Mungu lazima arudishe na
atarudisha kwa ukubwa.

Nixon
Washington DC

--- On Mon, 1/3/11, Benjamin Swai <bmswai@yahoo.com> wrote:

From: Ali Selemani [mailto:ASelemani@deloitte.co.tz]
Sent: 30 December 2010 20:29
To: Ntengua Mdoe; Dr. Donath R.Olomi
Cc: 'Ntengua Mdoe'; atemu@dcl-tz.com; 'Anna Temu'; 'Anna Temu';
tiisekwa@suanet.ac.tz; Abel Lyimo; director.general@coffeeboardtz.org;
Altemius Altemius Millinga; AMOS WANYIRI; 'Atiba Amalile';
btiisekwa@yahoo.co.uk; bzebedayo@yahoo.com; bazelux@yahoo.com;
ibdiagency@gmail.com; bndabikunze@yahoo.co.uk; bndabi@suanet.ac.tz;
karambi@yahoo.com; Iddy Lujina -private; ilujina@pass.ac.tz; 'JACOB
CHUWA'; joempagalile@suanet.ac.tz; jjmpagalile@yahoo.com; 'Peter
Kikoka'; linus gedi;
Subject: RE: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE

Dr. Olomi,

Huu ni ujumbe muhimu sana kwa watanzania wote hasa wakazi wa mijini.
Desturi hii ilianza taratibu kwa harusi za milion 5 mpaka 8, mara
ikatokea inflation ya michango na kufikia harusi za milioni 20, 30 na
kuendelea. Ni ugonjwa ambao mara zote nimekuwa nawaza. Kwa sasa
ugonjwa huu unaenda kuwa sugu. Naungana na wewe kwa asili 100. Siku
hizi unakuta watu wanabariki ndoa kwa 10 milioni na wanaona sawa.
Ukiambiwa kuna mtoto kafaulu anahitaji laki 5 watu wataanza kuuliza
kwani akisoma mie nitafaidi nini, je ukitoa laki 1 kwa ajili ya harusi
unafaidika na chochote zaidi ya kunywa na kula ndani ya masaa 3 tu.
Mie nadhani tunatakiwa tubadilike tena haraka. Mie naanza January 2011
kutokuchanga kama sio mtu wa karibu.

Asante kwa kuanzisha topic hii

Sent from my mobile device



Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Rafiy Saleh" <rsaleh@rana.co.tz>
Date: Thu, December 30, 2010 6:34 pm
To: "Dr. Donath R.Olomi" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>
--------------------------------------------------------------------------

Thanks Dr. Olomi

Rafiy Saleh (+255 767 888 566). Sent from my BlackBerry® smartphone
from Vodacom
---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: FW: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "mary lubuva" <marylubuva@yahoo.co.uk>
Date: Tue, December 28, 2010 3:28 pm
To: "vincent assey" <vincentassey@yahoo.co.uk>
Cc: olomi@udbs.udsm.ac.tz
deomalamsha@nbs.go.tz
--------------------------------------------------------------------------

THANKS FOR UJUMBE, INFACT MIMI NILIANZA HILO ZOEZI LA KUTOKUTOA SINCE
JULAI 2010 MICHANGO YA HARUSI, K/PARTY, UBATIZO SEND OFF NK ISIPOKUWA
YA MISIBA NA NINATOA PALE AMBAPO KWELI KUNAHITAJIKA MSAADA WA PESA KWA
SABABU SIYO KILA MTU ANAHITAJI MSAADA WA PESA NDIO MAANA KADI
ZINAANDIKWA " MCHANGO WA HALI NA MALI" KWINGINE NATOA 100% MCHANGO WA
HALI.......... NAENDELEA NA OBSERVATIONS, WHAT HAPPENED, WALE WOTE
AMBAO SIJAWACHANGIA REGADLESS YA SABABU NILIZOTOA WAME-CUT -OFF
COMMUNICATION LAKINI KWANGU MIMI NI POSITIVE RESULTS KWANI
NIMESHAPUNGUZA MLOLONGO WA KULETEWA KADI.
TUJIFUNZE KUTAYARISHA SHUGHULI/SHEREHE ZETU KWA KADIRI YA UWEZO
TULIONAO NA IDADI YA WATU/NDUGU NA MARAFIKI WAALIKWE KWA KILE KIDOGO
AU KADRI MTU ALIVYOJAALIWA NA SIYO KUJALI WATU WENGINE WATAKUONAJE.

M. LUBUVA.

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: [Fwd: Fw: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA
SHEREHE]
From: kideghesho@suanet.ac.tz
Date: Sat, December 25, 2010 4:11 pm
To: dvc@suanet.ac.tz
Cc: allsua@suanet.ac.tz
allsuasa@suanet.ac.tz
--------------------------------------------------------------------------

Awali ya yote namshukuru sana huyu aliyeleta huu ujumbe hapa.

Kwa kweli michango inaumiza sio mchezo!!! Michango imekuwa ndio
kipaumbele
chetu. Hapa SUA kinachofanyika ni mtu kubeba prospectus na kuanza
kuorodhesha majina ya wqachangiaji. Juzi bwana mmoja kanionyesha idadi
ya
kadi za michango alizopata mwaka huu. Bahati nzuri yeye huwa ana faili
la
kadi za michango kabisa. Kimahesabu tu kama angesema achangie 20,000
kwa
kila mmoja ilikuwa inafikia laki nane (ukiachilia mbali zile
alizoombwa
kuwa mwanakamati).


Kama kawaida maneno mazuri - UKIWA KAMA NDUGU WA KARIBU ndiyo
kibwagizo!
Jamani huu undugu wa karibu unakuja wakati wa michango ya harusi tu?
Mbona
nilipolazwa Mazimbu hukuja kuniona? Kasheshe zaidi ni pale unapokuta
mtu
kaishi na mke miaka 20 anakuja na hoja ya kubariki ndoa - na yeye
anataka
achangiwe kwa sababu hakuwa amefunga ndoa!! Kama huu si usanii wa aina
yake unatuambia kuwa miaka yote hiyo alikuwa sio mke!!! Ingawa pengine
hii
inafanyika makusudically baada ya mtu kuona kuwa amekuwa anachangia tu
na
hamna dalili kuwa kesho ataozesha ili naye achangiwe!

Ningeelewa sana kama 50% ya michango wangekuwa wanapewa maharusi
wakaanzie
maisha! lakini milioni 15-20 tumboni tu!!! Hapa sielewi na sitaelewa
kitu!! Hii ni israfu (kufuru!!). Majuzi Kuna mtani wangu mmoja
alifanya la
maana sana hapa Moro- Michango yote kwa ajili ya send-off ya binti
yake
ambayo ilipita kwake badala ya kwenye kamati aliipeleka CRDB!!!
kifuatacho
ITV baada ya harusi ni biashara!!! Wanakamati walikuja juu lakini
haikusaidia kitu - send-off ilifanyika kwa mafanikio makubwa,
waliosusa
walisusa na baadhi (nikiwemo mimi) nilisema BRAVO Mathaawe!! Keep it
up!!!

Halafu sasa harusi nyingi zinafanyika November-January. Kama una
watoto 6
wa kupeleka shule shauri lako - lakini michango ya watu utoe!! Wewe
mwambie mtu kuwa una mgonjwa anatakiwa shs milioni 2 za matibabu -
bado
atasisitiza - kuwa deadline ya michango ya harusi ni kesho. Mgonjwa
wako
afe tu lakini mchango wa watu ni lazima.Kimsingi ni kwamba binadamu
hatuna
huruma. Hiyo ndiyo ghrama ya kutafuta social capital!!! Lakini hivi
social
capital lazima itafutwe kupitia michango ya harusi?

Jamani naomba msinipige mawe lakini haya ni mawazo yangu katika kuweka
mkazo wa hayo yaliyowasilishwa hapa!! Jamani tutafakari na tuchukue
hatua!! Naomba kutoa hoja!!

Kind rgds,
Kideghesho



---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: eric@udbs.udsm.ac.tz
Date: Mon, December 20, 2010 8:31 pm
To: "Elly" <elly@udbs.udsm.ac.tz>
Cc:
--------------------------------------------------------------------------

Naomba kuchangia hoja kama ifuatavyo
Kuma mambo ya kimsingi ambayo yanatupasa kufanya kama wanajamii
wawajibikaji. Mambo kama kusaidia wenye shida kwa chakula,mavazi elimu
n.k,kuwafariji wafiwa na kusalimia wagonjwa ni wajibu wetu. Wajibu huu
umesisitizwa na mafundisho ya dini zote, kuyafanya ni kutimiza ibada
na malipo yake ni kupata thawabu kwa Mola.Utoaji wa mtu katika mambo
haya ni hiari kwa jinsi mtu alivyoguswa na alivyobarikiwa na Mwenyezi
Mungu.

Kuna mambo mengine yasiyo ya kimsingi lakini tunayafanya kutokana na
mazingira tuliyopo na jamii inayotuzunguka.Mambo haya ni kama
kushiriki kwa hali na mali katika sherehe,misiba n.k, huu ni utaratibu
wa kijamii ambao umejengeka kwa miaka mingi.Ushiriki wa mtu katika
mambo hayo bado ni
hiari kwa jinsi mtu anavyojisikia. Kutokushiriki kunamfanya mtu awe
amejiweka mbali na jamii inayomzunguka. Kushiriki kunajenga mahusiano
mema, kunadumisha upendo na mshikamano kwa jamii. Haya yote ni mambo
mema.

Jambo lingine la kizingatia katika hoja zilizotolewa na baadhi ya
wachangiaji ni kuwa si kila matumizi lazima yawe in the typical
economic sense. Mfano it does not make any economic sense to spend
millions to transport a deceased person toka sehemu aliyokua akiishi
miaka yake yote kwenda kumzika kijijini alikozaliwa ambapo hajaishi
kwa miaka nenda rudi.Lakini watu wanafanya hivyo kwa sababu zao
wanazozielewa. Lingine ni utaratibu wa watu kujenga nyumba huko
mashambani zinazokaliwa kwa majuma mawili kwa mwaka( Krismas na mwaka
mpya), na hakuna mtu wa kupanga hizo nyumba hivyo kuwalazimu wamiliki
kuingia gharama za walinzi na watunzaji wa nyumba hizo.Matumizi ya
aina hii hayana mantiki kiuchumi lakini yanakidhi mahitaji ya
kisaikolojia kwa watimiaji. Viashiria vya matumizi
binafsi vina mkanganyiko ambao ni mgumu kidogo kuutathmini.In many
cases personal spending behavior is diffucult to capture in any
economic model because of its complexities.

To sum up,is it bad to indulge ourselves in eating, drinking and be
merry for a one day occassion called a wedding? probably not

Should we expect others to finance our extravagances? definately no,
it depends on how we relate to those we ask to contribute

Should we stop to contribute to weddings? probably no,again the
decision of weather to contribute or not is a matter of personal
choices and preferences and it is entirelty voluntary!!!!
To all!
> Greetings----- as a contribution
> I think this is a very important discussion. Let me take an extra step, by calling people interested in doing some more scholastic investigation on this matter and come up with one or several articles. The issue is multifaceted including social, economic, prioritization etc.
>
> Elly,Tumsifu
>
>
>
>>
>
>
>> Hello!
>>
>> This is certainly an interesting issue and there are bound to be divergent views. I however, do not think a communal position can be reached. It will have to be an individual position. And if a critical mass of individuals take, for example, the position that Dr. Olomi suggests for himself then >> this matter of wedding contributions will move a certain direction.
>>
>> I guess this is how it started in the first place - a few people went for these big, superficial, show weddings and it caught up and we are all in the bandwagon.
>>
>> I took a position a long time ago. I think it was at the Audio Visual Institute as it used to be known [currently where TBC offices and studios are]. I went to a wedding reception that I was somehow involved in its preparation. Substantial sums of money were involved and in the end every joker wanted to make a bit of money for themselves. But that was not the principal issue for me - it was the whole atmosphere and the service quality. I had to endure nearly 3 hours of high decibel noise [music and a very self important MC] at the end of which I was given a fried potatoe and a large bone [think it was part of a knee cap] wrapped in a foil. I was indeed hungry and felt doubly dissapointed - that I had allowed myself to be worked up by something that was just a bad show.
>>
>> So since then I made my decision. I would contribute and be involved in the old traditional way - to a close relative, or a personal/family friend. But they must also need the contribution! If one sat at home and came up with a TAS. 100 million budget for their daughter's wedding it would be a signal to me that they actually did not need my contribution and would give none, even if they were my brother. I would attend too on the same basis, regardeless of whether I contributed or not. Just the same old way.
>>
>> Sorry if my views hurt anyone's feelings. Vote with your wallet!
>>
>> Cheers.

>>> Winnie,
>>> Hili nalo neno

Mbura, UDBS

>>>> Dr. Olomi et al:
>>>>
>>>> Kimsingi nimejiuliza maswali mengi sana kabla sijaunga au kukata mkono
>>>> hoja.
>>>>
>>>> Tunafahamu kuwa hela hailiwi, kinacholiwa ni chakula, vinywaji, muziki
>>>> kidogo, relaxation na quality place. Hela huwa inapewa aliyetoa hizo
>>>> huduma (caterers, DJ, MC, Umeme, tarumbeta, n.k). Na aliyetoa huduma
>>>> anakwenda kuwasomesha watoto wake. Huenda nyingine anakuja kutumia
>>>> kwenye biashara zetu (wengine shule, wengine hotel, wengine banks, nk.).
>>>>
>>>> Je, ni rahisi zaidi kukutana na mtoto wa mtoa huduma tukamgawia dola
>>>> 5000 ili akwende shule, au kumpa mzazi wake aliyetoa huduma na wewe ukala
>>>> hapo kidogo na nyingine akampea mwanawe kwenda shule?
>>>>
>>>> Kwa kifupi, naomba yeyote anayeweza kufanya study ya
>>>> ku-estimate/measure economic impact ya weddings, send-offs, etc ili tujue the end-user wa
>>>> ile laki moja au elfu hamsini tunayotoa inashia wapi. Genuine, economist,
>>>> econometric kidogo hapa, kazi kwako.Naomba data ili tu-make decisions:
>>>>
>>>>
>>>> Winnie
>>>>
>>>>

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Genuine Paul Martin" <genuine@udbs.udsm.ac.tz>
Date: Fri, December 17, 2010 10:50 pm
To: wineaster@udbs.udsm.ac.tz
Cc: "Genuine Paul Martin" <genuine@udbs.udsm.ac.tz>
academicstaff@udbs.udsm.ac.tz
--------------------------------------------------------------------------

Dr. Winnie, hujakosea kwa sababu kiuchumi tunasema consumption
inastimulate demand, inakuza biashara, vipato, ajira na hatimaye pato
la
taifa katika ujumla wake. Ikizidi sana pia, inapunguza capital stock
na
ukosefu wa mitaji unafanya mikopo kuwa ghali (pushing up interest
rates)
hii ikichangiwa pia na risks zilizopo katika mazingira. Changamoto ni
kuweza kujua which is the optimal level of consumption and savings
ambazo
itaoptimize economic growth.

Dr. Aikaeli ameandika paper ya 'Determinants of excess liquidity in
tanzanian commercial banks' ipo kwa internet, moja ya sababu alizoona
ni
credit risk, costs of illiquidity among others. Kwa mfano wa harusi,
fedha
zinatoka kwenye michango ya watu, na zinalipwa in cash kwa hiyo bank
intervention is not an issue here. Vitu vitatu ambavyo ni ununuzi wa
magari ya kifahari, kuwepo na sherehe kama hizi na utumiaji wa fedha
nyingi kwa mawasiliano ya simu yasiyo na msingi (asilimia kubwa).
Inaonesha tuna fedha lakini hatuelewi au hatuna mwamko wa kuziingiza
katika shughuli za maendeleo.

Nafikiri Dr. Olomi na wenzake wa Enterpreneurship watatusaidia kuelewa
tufanye nini ili fedha hizi ziingie kwenye shughuli za maendeleo,
nakumbuka Dr. Alan alinifundisha concept ya 'pro-consumption' type of
spending is damaging for the development of our economy. Kuna vitu vya
kuconsume, chakula bora, huduma za afya, mavazi, malazi, elimu, maji,
umeme, na vingine, vyote ni consumption lakini kwa harusi na sherehe,
its
extremely superfluous.

> Genuine:
>
> Hapa nimevutika. Kuna baadhi ya vitu tumesahau though.
>
> Nchi zilizoendelea, consumption is highly encourage ili kukuza
> investments. Mikopo mingi hupewa watu wao ili waweze kununua vitu (mara
> nyingi mogeji inatumika), ili viwanda viendelee kuzalisha na watu waweze
> kuajiriwa. Investments zikikuwa sasa, unaona wanakuja huku kwnye nchi zetu
> kwa ajili ya madini na kupata cheap labor. Akina Resolute Ltd; Ashanti
> Goldfields AngloGold; Barrick Gold Corp; Placer Dome Inc; Meremeta Ltd;
> and Pangea Goldfields Inc na Miniere du Nord hawakuamka wakiwa matajiri wa
> kuchimba dhahabu. Walianzia somewhere. That is business growth through
> some variables-consumptions included.
>
> Kwa bahati mbaya sana, nchi zetu huwa zinachukulia consumption kama
> dhambi. Hela zinaozea banks. Kumbe tungezitoa kwenye systems kwa njia
> mbalimbali kama maharusi yetu na vitu vingine uchumi wa biashara mojamoja
> ungekua, na vibes zingeendelea kwa nchi nzima kukua kiuchumi.
>
> Winnie
>
>
> Vitu vingi
>> @Ambege... naona suala hapa si kiasi gani bali ni kwa ajili ya nini
>> ambacho kitakuwa na manufaa ya muda mrefu, yaani elimu au sherehe.
>> Nakubaliana na ukweli kuwa mawazo ya KIJAMAA tuliyorithi kwa mababu zetu
>> yameathiri sana mitizamo na fikra zetu, yaani undugu, mshikamano na
>> umoja,
>> bila kuzingatia matokeo ya kiuchumi.
>>
>> Nafurahi kwamba, hoja za manufaa ya sherehe hizi zimetajwa na zina
>> ukweli;
>> yaani kuimarisha social capital, umoja na undugu katika moyo wa
>> kusaidiana; pia kutengeneza ajira na kipato kwa biashara hizi, MC, DJ,
>> mapambo, caterers, kumbi na kadhalika. Katika exchange yoyote kuna
>> watakaogain na watakaolose, kwa wafanyabishara na kwa pato la taifa
>> litokanalo na huduma hii, ni neema. Lakini kwa burden ya wanaochangia
>> its
>> hectic. Katika uchumi kwenye consumption function, kama proportion kubwa
>> inakuwa consumed, savings zinadecline, investments flow inasinyaa na
>> hatimaye capital stock inapungua, capital stock ni factor kubwa sana
>> katika ukuaji wa uchumi wa muda mrefu yaani longrun economic growth
>> (Y=f(A, K, L)).
>>
>> Hoja nyingine ya kiuchumi ni necessity ya bidhaa yenyewe inayozalishwa,
>> ambapo hapa ni sherehe, watu wanakunywa, wanakula, waenjoy muziki,
>> wanashereheshwa, wanashangilia, nderemo na vifijo, ndo final product
>> hapa.
>> Swali ni je, bidhaa hii ni muhimu kwa maendeleo ya muda mrefu? Je, kwa
>> Tanzania hatuna changamoto za kumudu vitu vya msingi kama huduma ya
>> elimu
>> na afya, tukawa na program za bima ya afya kwa mfano? Vipi kuhusu umeme,
>> maji, miundombinu, n.k. Vipi kuhusu uwekezaji katika rasilimali zetu za
>> msingi, sisi twawekeza kwenye sherehe, wenzetu wanakuja kuvuna madini
>> yetu, ardhi yenye rutuba, n.k. Vingine vingi kama misitu, uvuvi, n.k.
>>
>> Naomba nipewe mfano wa taifa liliondelea duniani kwa staili hii. Wenzetu
>> kama Korea wameinvest heavily in education, wengine kwenye export
>> sector,
>> ss tunashabikia sherehe, na hali tuliyo nayo.
>>
>> Just mtizamo wangu, si lazima uwe sahihi.
>>
>> Genuine.---------------------------- Original Message ----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: kananrenger@udbs.udsm.ac.tz
Date: Mon, December 20, 2010 11:09 am
To: "Elly" <elly@udbs.udsm.ac.tz>

--------------------------------------------------------------------------

Hi to all udasans

It is such an amazing discussion,i couldnt imagine if the issue of
marriage contribution hurt so much to so may individuals,"VERY
SORY".Personally am not the fond of Extravagant spending,but again can
not
deny the trickle down effect of the marriage indutry in the economy of
our
country and education sector at large.I do believe there is time for
everything and every activity in the world

- a time to contribute to social events and time to contrinute to
marriage
- a time to mourn and a time to dance
- a time to weep and a time to laugh,
- a time to tear down and a time to build
- a time to plant and a time to uproot,
- a time to embrace and a time to refrain,
- a time to search and a time to give up,
- a time to keep and a time to throw away,
- a time to tear and a time to mend,
- a time to be silent and a time to speak,

I am not telling anyone to take position on whether to keep on or to
refrain from contributing to weeding ceremony as it is personal
decision,
but the fact is the supply chain of wedding industry is so big and
employing a lot of people in such a way that we can not dare to kill
it,
if at all our aims is to contribute to our education system and the
economy as a whole
---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: hodihenga@yahoo.com
Date: Mon, December 20, 2010 7:38 am
To: "Dr. Donath R.Olomi" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>

--------------------------------------------------------------------------

Dk, nakubaliana na wewe kwa asilimia mia moja! Mimi binafsi nilikwisha
litolea uamuzi hilo tangu mwaka jana! Jamani tuzitendee haki nafsi
zetu! Too much for nothing much!Dihenga.
Prof Hamisi Omar Dihenga, PhD; Permanent Secretary and Professor of
Agric Engineering, Sokoine University of Agriculture
---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "dominick haule" <dominickhaule@yahoo.co.uk>
Date: Sun, December 19, 2010 10:16 am
To: "Donath Olomi" <olomi@yahoo.com>


"--------------------------------------------------------------------------

Waungwana, tatizo aliloliainisha Dr. Donath Olomi, ni tatizo la
kisaikologia. Huo ni ugonjwa ambao unatibika kwa mtu kujitambua na
kuelewa kimsingi mambo muhimu kwa binaadamu. Kuna wengi ambao hawajui
kwa mfano wamekuja duniani kufanya nini.


Ugonjwa huo ni mkubwa zaidi kwa ndugu zangu watanzania na tatizo kubwa
ni la kifikra. Kuna tabia mbaya sana ya kufanya mambo ili kuridhisha
na kufurahisha watu bila kujali madhara au matokeo ya mambo hayo.

Ukiitafakari kwa kina hoja ya Dr. Olomi haiishii katika michango ya
harusi na, vipaimara, komonio, sherehe za kuzaliwa, pamoja na shughuli
za kuwatowa watoto wetu waliovunja ungo, bila kujali wengine wanakuwa
wameanza mapenzi kabla ya kuvunja ungo.

La msingi hapa, tubadilike kwa ujumla na tufanye mambo ya maana na ya
maendeleo bila kujali kama yatawafurahisha watu au yatawaudhi na
kuwabugudhi.

Tufanye mambo ya msingi, kwa mfano, mtu ambaye hajaweka mlango wa
choo,
asichangie harusi, na siyo harusi tu, asitoe hata offer za vinywaji
kwa
kuzungusha "round", hadi hapo atakapomaliza kuweka vizuri choo chake
na
kutengeneza nyavu za mbu za nyumbani kwake kwanza. Wengi
hawatamfurahia lakini atakuwa amesonga mbele kimaisha.

Kwa kifupi, wengi wetu tunapenda sifa, watu watuone na tuwaoneshe kuwa
sisi tupo katika hali gani. Kuna jamaa nchi hii wananunua vitu vha
gharama sana na wanateseka navyo bila sababu ya msingi, Kwa nini kwa
mfano mtu anajenga nyumba ya shilingi milioni 700 wakati hana mradi
hata mmoja? Kwa nini kwa mfano tununue suti za dola 1000, za ulaya
wakati tuna nguo zinazotengenezwa na dada zetu wa hapa nchini na
wanaziuza kwa chini ya shilingi laki moja.

Azimio la kuacha kuchangia harusi mimi nimeanza kulitekeleza mwaka
jana,
nachangia harusi za familia tu tena kwa kiasi kisichazidi shilingi
laki moja. Hilo mwisho ni mwaka huu baada ya hapo, kila atakayefanya
harusi atawajibika kutualika kama anataka kufanya hivyo na kama ana
uwezo.

Katika shughuli za harusi, la maana na kitu cha msingi ni ibada ya
ndoa. Ibada hizo huwa zina gharama ndogo ambazo mwenye shughuli
atazimudu. Hivyo uganjwa huo wa kisaikolojia utakwisha kwa kuelewa tu
kwamba katika vitu kama vile harusi, vipaimara, maulid, ubatizo,
komunio, LA MSINGI NI USHIRIKIANO KATI YA MHUSIKA NA MUNGU WAKE.
SHUGHULI YA MAANA IPO KANISANI BAADA YA HAPO YOTE NI UBATILI MTUPU.

Ninaunga mkono huja hiyo, hata hivyo, nakaribisha maombi ya kuchangia
elimu kwa wale wenye mahitaji na hawana uwezo kabisa.

Huu ni wakati sasa wa kuanza kufanya harambee za kusaidia elimu kwa
wale wasio na uwezo. Tuanzie mahali fulani, nashari, yeyote ajitolee
na aanzishe utaratibu wa harambee za kuchangia elimu. Linaonekana kama
vile ni jambo la mzaha lakini tutaleta mabadiliko makubwa na mazuri
kwa maendeleo ya familia zetu na taifa kwa ujumla.

Naomba kuwasilisha.

Dominick Haule


---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Simon Edward Mangesho" <mangesho@udbs.udsm.ac.tz>
Date: Fri, December 17, 2010 10:06 pm
To: mbelwa@udbs.udsm.ac.tz
Cc: academicstaff@udbs.udsm.ac.tz
--------------------------------------------------------------------------

Latifa umeleta changamoto ngumu kutekelezeka, wachangiaji wanatumiaje
nguvu zao kusaidia ndoa ya wahusika idumu?
>
>> Salaam,
> Nakubalina na Dr, Olomi. Mimi nashauri badala yakufanya harusi za gharama
> na anasa kubwa, tujitahidi ziwe simple lakini kama mdau mkuu anataka ya
> gharama kubwa basi ajitahidi mwenyewe kujichangia kwa kiasi kikubwa kama
> vile mtu ajengapo nyumba yake sidhania kama atakaribisha watu wachangie
> kwa ajili yakulinda ownership. Na pia tujitahidi kutumia nguvu zetu
> kuzifanya ndoa hizi zikawa zakudumu badala ya temporal business like joint
> venture, Going concern haipo kabisa. Ndoa ya inagharimu mil 30 inadumu kwa
> miaka 2, yaani depreciate kwa mil 15 kwa mwaka! halafu ikawa na zero
> value. Nyingine zinaendelea with operation lakini with a very big repair
> and replacement cost(small house). Lakini pia hii isiwafanya wala ambao
> hawajao/kuolewa kusita kuingia kwenye mchakato, Kwa ufupi ndoa ni kitu
> kizuri kimebalikiwa na Mungu, kinajenga heshima, kinakuza uwezo wakufikili
> na kutenda hakihitaji initial cost(Quantitative) kubwa ila kinahitaji
> qualitative things such as upendo wenye kuendelea, uvumilivu, hekima na
> busara, usamehevu, utiifu n.k..
>
>
> Best regards,
> Latifa

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Maua Daftari" <daftaridr@yahoo.com>
Date: Fri, December 17, 2010 4:04 pm
To: "Dr. Donath R.Olomi" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>
--------------------------------------------------------------------------

Dear dr olomi,nakubaliana kabisa na wazo lako,huko tunakotoka haya
kuchangia
harusi,na hadi hii leo wako wanaojitahidi kukata pua na kuunga wajihi-
hawawapi mzigo wengine ktk kutimiza wajibu wao.hebu siku moja tpn
katika vikao vyake vya kuelimishana agenda hii iwekwe mwisho as
aob.daftari.
_________________________

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "HRT Muzale" <hmuzale@udsm.ac.tz>
Date: Fri, December 17, 2010 12:47 pm
To: olomi@udbs.udsm.ac.tz
Cc: udasa@udsm.ac.tz
--------------------------------------------------------------------------

Dr Olomi, et al.

Kwa kawaida, na/au kwa walio wengi, hawakuchangii ili ufaidike, bali
wanachanga ili waje kula pesa zao kwenye sherehe yako, na wewe
uburudike
nao.

Ndiyo maana, kwa baadhi ya watu, wakikuchangia unaoa, hawataki utumie
pesa
hizo kununua suti au nguo za bibi harusi.

Mtu atakwambia: Nimchangie mtoto wako apate elimu, kisha mimi
nifaidikeje?
Yaani unataka tukusomeshee watoto wako!?! Hili ni tatizo lako...!!!

Ni sawa na mtu kukualika kwenda baa, ukasema "leo sinywi"; hawezi
kusema
basi chukua hizi 10,000 ambazo ningekununulia pombe..!! Kama hunyi,
basi
yameisha; nenda zako!

Ukiwa na bahati kama mimi, watakuchangia kwa dhati. Mimi wakati naoa,
marafiki zangu waliujua udhaifu wa kipato changu, na wakaniambia
nisiichangie harusi hiyo, bali nitumie pesa zangu kukamilisha mengine.
Sikuamini masikio/macho yangu. Nilipojaribu kufanya hivyo kwa marafiki
zangu wengine, wajumbe wa vikao walitaka kunitoa macho, wakisema:
"Kama
hawezi kuchangia kwa nini ametuita!"

Wengine pesa wanazo, tena za bure zinazoingia kila siku; wengine
wanaokoteza na kuchangiana kwa moyo na upendo. Walio nazo waache
wazimwage, maana zipo. Ambao hawana wanapima hali halisi na kuamua.
Wengine wanazo, lakini zina matumizi mengine ambayo kwao ni muhimu
zaidi.

Lakini na wasanii pia wapo! Na matapeli wapo pia. Na wengine
wanatumia
nafasi hiyo kutengeneza mtaji. Akili ku kichwa, kila mtu ana zake...!!

Hayo ndiyo maisha
Huyo ndiye binadamu;
Kiumbe mwenye akili
Lakini anayefanya viroja
Kuliko wanyama wote!
Kiumbe asiyetabirika
Kiumbe anayebadilika
Anayependa anayoyachukia
Na kuyachukia anayoyapenda;
Huyo ndiye Bin Adam!

Pole sana Kiumbe we...!


HRTM

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Genuine Paul Martin" <genuine@udbs.udsm.ac.tz>
Date: Fri, December 17, 2010 1:05 pm
To: ambege@udbs.udsm.ac.tz
Cc: wineaster@udbs.udsm.ac.tz
"Dr. Donath R.Olomi" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>
academicstaff@udbs.udsm.ac.tz
--------------------------------------------------------------------------

@Ambege... naona suala hapa si kiasi gani bali ni kwa ajili ya nini
ambacho kitakuwa na manufaa ya muda mrefu, yaani elimu au sherehe.
Nakubaliana na ukweli kuwa mawazo ya KIJAMAA tuliyorithi kwa mababu
zetu
yameathiri sana mitizamo na fikra zetu, yaani undugu, mshikamano na
umoja,
bila kuzingatia matokeo ya kiuchumi.

Nafurahi kwamba, hoja za manufaa ya sherehe hizi zimetajwa na zina
ukweli;
yaani kuimarisha social capital, umoja na undugu katika moyo wa
kusaidiana; pia kutengeneza ajira na kipato kwa biashara hizi, MC, DJ,
mapambo, caterers, kumbi na kadhalika. Katika exchange yoyote kuna
watakaogain na watakaolose, kwa wafanyabishara na kwa pato la taifa
litokanalo na huduma hii, ni neema. Lakini kwa burden ya wanaochangia
its
hectic. Katika uchumi kwenye consumption function, kama proportion
kubwa
inakuwa consumed, savings zinadecline, investments flow inasinyaa na
hatimaye capital stock inapungua, capital stock ni factor kubwa sana
katika ukuaji wa uchumi wa muda mrefu yaani longrun economic growth
(Y=f(A, K, L)).

Hoja nyingine ya kiuchumi ni necessity ya bidhaa yenyewe
inayozalishwa,
ambapo hapa ni sherehe, watu wanakunywa, wanakula, waenjoy muziki,
wanashereheshwa, wanashangilia, nderemo na vifijo, ndo final product
hapa.
Swali ni je, bidhaa hii ni muhimu kwa maendeleo ya muda mrefu? Je, kwa
Tanzania hatuna changamoto za kumudu vitu vya msingi kama huduma ya
elimu
na afya, tukawa na program za bima ya afya kwa mfano? Vipi kuhusu
umeme,
maji, miundombinu, n.k. Vipi kuhusu uwekezaji katika rasilimali zetu
za
msingi, sisi twawekeza kwenye sherehe, wenzetu wanakuja kuvuna madini
yetu, ardhi yenye rutuba, n.k. Vingine vingi kama misitu, uvuvi, n.k.

Naomba nipewe mfano wa taifa liliondelea duniani kwa staili hii.
Wenzetu
kama Korea wameinvest heavily in education, wengine kwenye export
sector,
ss tunashabikia sherehe, na hali tuliyo nayo.

Just mtizamo wangu, si lazima uwe sahihi.

Genuine.
>> Ni mjadala mzuri kwa kweli na ninaamini tutajifunza vitu hapa.
>
> Ingawa sitetei matumizi ya kiwango kikubwa cha pesa kwa ajili ya sherehe.
> Lakini najiuliza kama mtu hautakuwa tayari kumuunga mkono ndugu wa karibu
> au rafiki/jirani kwa sh elf 50,000 or so kufanikisha sherehe yake utaweza
> kuchangia Dola 3,000 kumpeleka shule mtoto wake? ni wazo langu.
>
> Ambege

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: ambege@udbs.udsm.ac.tz
Date: Fri, December 17, 2010 12:20 pm
To: wineaster@udbs.udsm.ac.tz
Cc: "Dr. Donath R.Olomi" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>
academicstaff@udbs.udsm.ac.tz
--------------------------------------------------------------------------

> Ni mjadala mzuri kwa kweli na ninaamini tutajifunza vitu hapa.

Ingawa sitetei matumizi ya kiwango kikubwa cha pesa kwa ajili ya
sherehe.
Lakini najiuliza kama mtu hautakuwa tayari kumuunga mkono ndugu wa
karibu
au rafiki/jirani kwa sh elf 50,000 or so kufanikisha sherehe yake
utaweza
kuchangia Dola 3,000 kumpeleka shule mtoto wake? ni wazo langu.

Ambege

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: ekitindi@udbs.udsm.ac.tz
Date: Fri, December 17, 2010 11:46 am
To: "Dr. Donath R.Olomi" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>
--------------------------------------------------------------------------

Dr. Olomi,

Hii nimeipenda sana. My thoughts exactly!

Kitindi


---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Gabriel Landa" <landag99@yahoo.com>
Date: Fri, December 17, 2010 8:44 am
To: "fcm staff" <academicstaff@fcm.udsm.ac.tz>
udasa@udsm.ac.tz


--------------------------------------------------------------------------

Ni jambo la kushukuru kwa kuanzisha mjadala huu.Kwa mawazo yangu,
sherehe zifanyike bali isiwe kama ni lazima. Jambo hili limepelekea
kusababisha migogoro baina ya ndugu, jamaa na marafiki ambao
hawakuchangia si kwamba hawakunuia, bali ni kutokana na vipato vyao
kuwa duni au kuwa na mambo mengine ambayo ni muhimu kwa wakati huo. Si
kwamba sherehe si muhimu ila tunahitaji kubadilika na kuelekeza
michango katika mambo ya maendeleo kama elimu, kuanzisha na kuendeleza
biashara n.k. Tujaribu kujifunza kutoka kwa baadhi ya jamii (waasia-
wahindi) ambao wanasaidiana kuchangiana mitaji ya biashara n.k.


---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Ellinami J Minja" <minja@fcm.udsm.ac.tz>
Date: Fri, December 17, 2010 11:24 am
To: "Dr. Donath R.Olomi" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>
Cc: academicstaff@udbs.udsm.ac.tz
--------------------------------------------------------------------------

Salaam,
Uelewa wangu kwa ujumbe wa Dr. Olomi ni kuwa "WE ARE EXTREMELY
EXTRAVAGANT" na tunajaribu kwalazimisha wengine nao wawe hivyo. Na
mwisho
ametoa msimamo wake. Kama utatumia econometrics au mbinu nyingine
kufikia
uamuzi ni juu yako.(Jitahidi kwenye model yako uweke kila kitu - kama
wewe ni MC au una biashara ya mapambo, your expectations, your EGO,
aspired social status etc. Hapa naweza kutoa msaada - for a small
fee).

Kwangu mimi nimeacha kwa muda mrefu sasa kuhudhuria haya masherehe
makubwa
ya usiku ambayo nimechangia. Mchango ni kama "SUNK COST" na model
yangu
niliyotumia imenipa jibu kwamba it is not worth it. They are held very
far
and sometimes in risky enviroments, you eat very late, you expose
yourself
to high decibels and possibly drunkards, you drive late - probably
while
intoxicated, you are seen by your kids as a FISADI because you
subscribe
to the idea that watoto ni marufuku in such events etc. What I do is
just
to take my family out for a treat

Ellinami

PS: Do not take this debate seriously. Just enjoy your friday and the
weekend ahead.

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Tobias Swai" <tobias@udsm.ac.tz>
Date: Thu, December 16, 2010 10:02 pm
To: wineaster@udbs.udsm.ac.tz
"Dr. Donath R.Olomi" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>
Cc: academicstaff@udbs.udsm.ac.tz
--------------------------------------------------------------------------

Wineaster
Mimi pia napata kigugumizi.
Unajua watu wengi wamekuwa wajasiriamali kwa ajili ya hizi shughuli
za
sherehe kitu ambacho hakuna anayepinga. Kama zinafaidisha taifa ni
kitu cha
kuangalia wahusika wanao kusanya kodi. Nakumbuka pia kwenye sherehe
hizi
baadhi wanatenga 10% kwa ajili ya watoto yatima at least kwenye kikao
cha
rafiki yangu nilichosimamia hapa karibuni. Zamani kulikuwa hakuna
biashara
hizi za ma MC, mapambo, chakula kizuri, kumbi, nk. Sasa kama watu
hawatachangia nafikiri vibaka watashika hatamu, ajira hamna, maua
yanayolimwa kule Moshi na ndizi sijui vipi. Pia ile kampuni ya hapo
Ilala na
Temeke pale karibu na Uwanja wa taifa wanaongoza kulipa kodi kwa
bidhaa
zinazotumiwa. Si hivyo tu hata kampuni nyingine kaza za wine, nk.

Na nafikiri pia kuwa fedha ni mzunguko na kuna namna ya kupata fedha
kwa
ajili ya vitu vingine kama kusomesha watoto, kwenda nje kusoma, nk.
Nafikiri
pia kumsaidia mtu mmoja mmoja haitakuwa inasaidia sana kujenga nchi
kwa
sababu kwa mfano uliotoa wa mtu anaenda AUS ni kufanya capital
flight..
kuchangia hapa kwenye harusi fedha inabaki ndani 100% kuna kigugumizi
hapa.
Nafikiri hili la kuchangia elimu lifanyike kama scholarship funds. Pia
hili
la harusi ni jukumu la Bwana na Bi harusi na wazazi pia.

@Genuine... maisha ni zaidi ya kutokuchangia harusi. Watu wanachangia
watu
si kwa sababu watakuchangia ama uliwachangia. Life is to be lived, how
you
define is up to you, do not perceive how people will judge you rather,
you
really do not know when you will be judged. Mimi siwezi kukuchukia
kama
hukuja kwenye mnuso wangu na wala siwezi kukupenda kama utanialika
kwenye
mnuso wako ama kukuchukia eti hukunikaribisha kwenye mnuso!!
Naomba niseme pia kuwa mimi nachangia mtu kwa binafsi yangu na
nafikiri
natoa michango mingi sana ya shule na shughuli za kijamii na kiroho
kuliko
harusi na kipaimara.
Tobias

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Janet Mbene" <maorchid@gmail.com>
Date: Thu, December 16, 2010 9:51 pm
To: "Dr. Donath R.Olomi" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>
--------------------------------------------------------------------------

Asante kwa kwa mchango wako wa wa mawazo.

Janet


---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: glad@udbs.udsm.ac.tz
Date: Fri, December 17, 2010 2:52 pm
To: academicstaff@udbs.udsm.ac.tz
Cc: administrativestaff@udbs.udsm.ac.tz
--------------------------------------------------------------------------

yaani tukiacha kuchangia harusi, mbona kama vile effect hiyo itarudi
pale
pale kwa mfano, wale wote wenye maduka pale namanga ya maua, wenye
catering services etc itabidi zife halafu sie tulio ajiriwa ndio
tutabeba
mzigo zaidi maana badala ya kusomesha wawili basi watakuwa kumi. sasa
tuna
intervene kwa strategy ipiiiiiiiiii!!!!!!!!!!


jamani mama yangu tena mnataka akose ajiraaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!! ha
haaaaaa
tena naye anasomesha kwa michango yenu ya harusi kazi ipooooooooooo

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "inter business" <ibdiagency@gmail.com>
Date: Thu, January 20, 2011 6:35 pm
To: "DJALOU FRANCO" <djalou_f@yahoo.com>
Cc:
"--------------------------------------------------------------------------

Guyus
jamani mimi nadhani wakati nisahihi kabisa wa kuanza kuchukua hatua,
hebu
tutafute njia na mahala pa kuanzia sasa

2011/1/20 DJALOU FRANCO <djalou_f@yahoo.com>

> mimi nakubaliana na nyinyi kabisa , na tuanze sasa, kwa kweli mimi
> binafsi nimekuwa msali wambele hata kuwachangia wamama wajane na
> waliotelekezwa vimitaji vidogo vidogo visivyo na riba ili waweze
> kujitegemea. na jamii imekuwa ikinishangaa kwanini sihudhurii harusi sana .
> yaani hiyo biashara ya harusi ilikwisha nichosha.
>
> nilipokuwa naolewa nilikataa sharehe wazazi wangu hawakunielewa. wakatsema
> si wanakuchangia watu wengine. lakini ukweli sikuona sababu yakuchangisha
> watu
>
> anyway all in all DR. Olomi hili ni wazo bora sana. kuna watoto wengi tu
> wamitaani, wajane ambao wanatunza familia zao. yatima ambao hawawezi kwenda
> shule hata kama kafaulu
>
> jamani kama tukiwasaidia hawa badal ya sifa yakuwanunulia watu magari kama
> zawadi za harusi na kufanya mashindano. JAMII YETU YAKESHO ITABADILIKA
>
> --- On *Sat, 1/8/11, Anthony Kaijage <akaijage2003@yahoo.com>* wrote:
>

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "gosbert katunzi" <gosbert2002@yahoo.com>
Date: Thu, January 20, 2011 10:24 pm
To: "inter business" <ibdiagency@gmail.com>
"Amos Wanyiri" <awanyiri@gmail.com>
Cc: "DJALOU FRANCO" <djalou_f@yahoo.com>

--------------------------------------------------------------------------

Ndugu wote,
Â
Heri ya mwaka mpya .
Â
Inasikitisha eti watu wanakusanyika kula na kulewa kisa eti Â
wanavunja kamati ya sherehe fulani !  Haohao au miongoni mwao
wanalalamika eti maisha magumu au fulani au chombo fulani hakileti
maendeleo !
Â
Wazo la kuanzisha Asasi au jukwaa kuhusu swala hili ni muhimu na la
kufanyiwa kazi haraka.
Â
"TUKOMESHE MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE NA KUELEKEZA NGUVU ZETU KATIKA
MICHANGO YA MAENDELEO"
Â
Gosbert Stanslaus

Subject: Fwd: Fw: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "SUBIRA MUNISHI" <evasubira@gmail.com>
Date: Mon, January 10, 2011 8:07 pm
To: fabyera@yahoo.com

--------------------------------------------------------------------------

Think this is the best resolution, at least watu watafanya sherehe
ambazo
zipo ndani ya uwezo wao tu au harusi itaanza kuwa ni kwa ajili ya
ndugu wa
karibu tu....


---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: RE: Fw: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Mathias Godfrey" <Mathias.Godfrey@tigo.co.tz>
Date: Sun, January 9, 2011 1:01 pm
To: "krchurch@googlegroups.com" <krchurch@googlegroups.com>

--------------------------------------------------------------------------

Wapendwa Bwana Yesu asifiwe;nakubaliana na hoja ya msingi iliyopo
mbele yetu lakini ninachokiona ni kile kipaumbele na muitikio katika
mambo yote.Binafsi kwa mtazamo wangu naona yote yana umuhimu kwamba
yanahusisha jamii kwa ujumla ikiwa ni pamoja na familia,ndugu jamaa na
marafiki.Kwa hiyo sioni kama inawezekana kuacha kabisa isipokuwa
tunapofanya jambo lolote tufanye kwa moyo na kwa nafasi iliyopo lakini
la msingi zaidi kuangalia kipaumbele kwa wakati ulionao.Mimi binafsi
wasi wasi wangu ni kwamba kama nitaitisha ndugu wa kuzaliwa kwenye
familia peke yao na kuishia hapo nitakuwa na watu wengi walio karibu
nikiwaacha au vinginevyo mnamaanisha niwajibike kugharamia na
kuwakaribisha,waswahili wanasema sherehe ni watu na watu wenyewe ndio
ikina nyie.Halafu pia naomba tusiwe wasahaulifu wengi wetu
tumeshapitia hatua hiyo na ninyi ni mashahidi wa mlichokifanya na watu
wengine walihusika kikamilifu.Najaribu kuweka angalizo tusije tuka
kata tamaa na kuacha kabisa pasipo kuwatia moyo vijana ambao wana
maono na maono yao yakapotea kwa sababu ya hofu.Kipaumbele katika mabo
yote ni jambo la msingi pamoja na kuwa na kuwa na kiasi tunaweza
kuyatimiza mambo yote kwa ukamilifu.Swala la kuchangia elimu ni mfumo
ambao unamtazamo hasi kwa jamii ni wajibu wetu kuielimisha jamii faida
na matokeo ya uwezweshaji kielimu kwenye jamii.

Samahani kama nitakuwa kinyume lakini huo ndio mtazamo wangu.

Bwana awabariki

Mathias G. Msangi

From: krchurch@googlegroups.com [mailto:krchurch@googlegroups.com] On
Behalf Of George Wandwalo
Sent: Saturday, January 08, 2011 11:28 AM
To: krchurch@googlegroups.com
Subject: Re: Fw: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE

Nina waslimu nyote kwa jina la yesu na Heri ya mwaka mpya 2011 wenye
strategies kibao kimaisha na kiroho.

Ningependa zaid kumunga mkono Dr Olomi kwa hili swala la Michango ni
kweli ina bidi liwe na mwisho maana tuna utofauti mkubwa na jamaa zetu
wa kenya, na ndo maana wako mbele kitaluma maana wao hakuna mtu
atakuchangia mchongo wa harusi ama sherehe labda close relatives na
lazima wewe uwe na mtaji kwanza inakuwa kituko ukisema unaitaji
mchango wa arusi maana hii nia yako binafsi ila ukisema mtoto amekosa
school fees kila mtu atatoa hata kuku ama umelazwa umekosa pesa
hospitalini watachangia hata "chief" atahusikia kuitisha harambee ili
mtoto aende shule ama kuokoa maisha ya mlipa kodi! maana wansema
ukisomesha atakuja kuisadia nchi yake ama siku mmoja ata saidia
mwanainchi mwenzake je Harusi ama sherehe ni ya mtu binafsi! nadhani
swala hili linabidi litafutiwe mbinu mbadala
na mbinu hiyo ni kuanza kupunguza kiwango cha michango ama kutoa pale
pana po gusa na hatimaye dhana itafutika vizazi vijavyo kwa kweli
ukijumlisha overhead expenditure ( Cost unit ya sherehe na arusi)
inachukua percentage kubwa na wakati mwingine una shangaa labda hata
kibanda fulani ungekuwa umemaliza, tufungue macho, michango hii
tukaelekeza kijamii kama kanisani nadhani itafanya kazi kubwa zaidi.
2011/1/5 apasaa nuru <apasaa3@yahoo.co.uk<mailto:apasaa3@yahoo.co.uk>>

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Anthony Kaijage" <akaijage2003@yahoo.com>
Date: Sat, January 8, 2011 11:05 am
To: "'Dr. Donath R.Olomi'" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>

--------------------------------------------------------------------------

Bwana Sambua na Olomi.
Kwanza Heri ya Mwaka mpya?
Ujumbe wenu bahati mbaya nilichelewa kuupata kutokana na sababu zilizo
nje ya uwezo wangu. Ninakushukuru Bw. Sambua kwa 'mail' yako,
umeniunganisha tena na rafiki yangu Bw.Ntengua Mndoe, tuliyekutana
mara ya mwisho miaka ya tisini tukiwa Wakurugenzi  Waanzilishi wa
CRDB Bank( a very big surprise to him also I presume?) Kwa mail hii
ninamwomba tuanze tena mawasiliano.
Kuhusu ujumbe wenu, ninauona si tu ni ushauri wa kawaida tu bali ni
muendelezo wa elimu ya Ujasiriamali, nyanja ambayo Bw. Olomi na
mwenzangu Bw. Sambua (sijui wengine samahani?) na mimi pia, tumebobea?
Ninaliunga mkono asilimia mia moja!
Mnajua ndugu zangu, baada ya miaka hamsini ya Uhuru, Wasomi tuache
kuendeleza tabia ya 'lip service' bila matendo! Taifa limetusomesha(au
hata kama tumesomeshwa na wazazi)
tuanze kuchanganua vyanzo vya Mtanzania kuendelea kuzama katika dimbwi
la umaskini wa kujitakia, kama michango ya sherehe?
Mimi pamoja na kuwa tayari kusambaza ujumbe huu nina pendekezo:
TUAZNZISHE MTANDAO RASMI AU CHAMA CHA HIARI CHA KUPIGA VITA TABIA HII
YA MICHANGO.
Naona tayari idadi inatosha, na Mwenyekiti wake wa kwanza awe Dr.
Olomi nk..Baada ya hapo tuandae Workshops za kuandaa 'Facilitators' na
ndipo kazi rasmi ya kuhamasisha jamii ianze?
 Nadhani kitu hiki kinaweza kupata 'support' ya Serikali na pia
'Non- State Actors', mnaonaje jamani? Liwezekanalo leo kwa nini
lingoje kesho?
Anthony Kaijage,
Mhadhiri, St.Augustine University of Tanzania-Mwanza.


---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: RE: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Ali Selemani" <ASelemani@deloitte.co.tz>
Date: Fri, December 31, 2010 5:58 am
To: "mboka mwanitu" <memwanitu@yahoo.com>
Cc: "nmdoe@yahoo.co.uk" <nmdoe@yahoo.co.uk>

--------------------------------------------------------------------------

Mboka,

Mawazo yako ni mazuri, issue ni kuwa miji yetu ishaparanganyika, open
spaces washachukua wakubwa community halls zitajengwa wepi. Mipango
mengine kama community kugharamia kila kitu ndo itakayosaidia
kureverse situation.

Heri ya mwaka mupya 2011

Sent from my mobile device
-----Original Message-----
From: mboka mwanitu
Sent: 30/12/2010, 22:05
To: Ali Selemani
Cc: nmdoe@yahoo.co.uk; "<olomi@udbs.udsm.ac.tz>" <nmdoe@suanet.ac.tz>;
<ngingite@yahoo.com>
Subject: Fw: RE: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE



My views:
1. Kuna haja ya kuwa na 'community halls'? watu wachangie kuziendesha
na kila mwana-jamii apate free access ya kufanya sherehe badala ya
kuzikodi kwa one day occassion kwa pesa toka kwa
enzie!.....inawezekana
2.Vyakula vya sherehe- tulink wakulima basi na hawa makatara?
au....model inaweza kuwekwa kwa tunataka kuleta maendeleo kwa kila mtu
3.Sherehe nzima kama ni(harusi,kipaimara,anniversaries) wenye sherehe
wajiandae kugharamia all basic things siyo wasubiri hela kutoka mifuko
ya watu!...nialike nije na zwadi yangu nikiweza
4. Tuanzishe fund raising basi ktk community zetu-sherehe hatuwezi
kuziepuka ni part ya life ila tuwena mipango/plans ukitaka
'extraordinary thing' ufanye mwenyewe hii ni free country kila mtu
anahaki ya kufany anachotaka, Dr ukianza kutochangia ni mwanzo mzuri
na ni mipango yako ya 2011
5. Tanzania hatutaweza kufanikiwa kama hatufanyi hivi vitu
practically,what i know wengi tunapenda kuongea tu......but its has to
begin with u......at ur own community with ur own circle of friends
and family!

Heri ya Mwaka Mpya 2011!



,Ahsante,Thanks,
With kind Regards,
Mboka Mwanitu- Massawe


---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Amos Wanyiri" <awanyiri@gmail.com>
Date: Thu, January 20, 2011 7:03 pm
To: "inter business" <ibdiagency@gmail.com>
Cc: "DJALOU FRANCO" <djalou_f@yahoo.com>

--------------------------------------------------------------------------

I fully agree with Dr. Olomi's proposal.

We can influence things from 'design' or planning stage and by
enlightening people to own the idea as well as using influencing
skills where we are invited to support.

It may take time to change the norms but eventualy and with good
success cases we shall achieve.

Amos wanyiri
IPhone

---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Omari Mbura" <Mbura@udbs.udsm.ac.tz>
Date: Sat, December 18, 2010 3:27 pm
To: "Dr. Donath R.Olomi" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>
Cc: academicstaff@udbs.udsm.ac.tz
--------------------------------------------------------------------------

Dr Olomi,
Pole sana kwa namna ambavyo unaonekana umeumizwa na hili la michango.
Nikisoma maelezo yako naona amabvyo unaumia. Sina la kusema ila kukupa
pole. Mfumo wetu wa jamii umetufikisha hapa.


---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Omari Mbura" <Mbura@udbs.udsm.ac.tz>
Date: Sat, December 18, 2010 3:32 pm
To:
--------------------------------------------------------------------------

Mkuu genuine,
ni kweli msimamo wako baadhi ytu tunautambua. Lakini nadhnai suala la
michango laweza kubaki kuwa matakwa ya mtu na ndio maana ulipoweka
msimamo
wako hakuna aliyezidi kukubana
> Wanataaluma na wote wenye mapenzi na taifa letu, Dr. Olomi ameelezea
> kitaalamu na kwa ufasaha mkubwa sana, siongezi neno bali kumwambia Dr.
> Olomi na wengine kuwa nimefurahishwa sana na maelezo yake.
>
> Mimi binafsi ingawa sikusema kwa umma, lakini nadhani kila anayenijua
> vizuri anafahamu msimamo wangu, idadi ya michango niliyowahi kutoa katika
> maisha yangu haifiki mitatu na sijawahi kuhudhuria sherehe hizi zaidi ya
> mbili hapa Dar es Salaam. Whether tutakuwa labeled kuwa antisocial au
> tumeignore social capital na kwamba hatutachangiwa; natarajia ndoa yangu
> kuwa tafrija ndogo ya familia na watu wa karibu na haihitaji kuchangiwa na
> yeyote.
>
> Watanzania tuamke, tunachoma mabilioni ya fedha kwa sherehe zisizo na
> msingi ukizingatia nchi yetu ni masikini pamoja na rasilimali zetu zote,
> ni kutokana na mambo kama haya yanayogharimu future ya taifa letu.
_________________
---------------------------- Original Message
----------------------------
Subject: RE: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "Sanctus Mtsimbe" <mtsimbe@simbanet.co.tz>
Date: Thu, December 16, 2010 9:43 pm
To: "'Dr. Donath R.Olomi'" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>

--------------------------------------------------------------------------

Dr. Olomi;

I support you 100%.

Let TPN take it in a way as one of our advocacy agenda.

Wishing all of you happy seasons.

Regards

SM
------------------------ Original Message ----------------------------
Subject: Re: MWANZO WA MWISHO WA MICHANGO MIKUBWA YA SHEREHE
From: "John J. Sanga" <jsanga@udbs.udsm.ac.tz>
Date: Thu, December 16, 2010 9:56 pm
To: "Dr. Donath R.Olomi" <olomi@udbs.udsm.ac.tz>
Cc: academicstaff@udbs.udsm.ac.tz
--------------------------------------------------------------------------

Dr. Olomi, naunga mkono hoja kwa vitendo kama unavyoona
nimekwishasambaza
ujumbe huu kwa zaidi ya watu 10 wasiofikiwa na mtandao ulioutumia.

Dr.Donath R. Olomi, P.O.Box 35036 Dar es Salaam, Mobile :
255-754/715-296660


--- On Thu, 11/17/11, Geoffrey mwa Ngulumbi <ngulumbig@yahoo.de>
wrote:

From: Geoffrey mwa Ngulumbi <ngulumbig@yahoo.de>
Subject: Re: MWISHO WA MICHANGO YA SHEREHE - REMINDER
To: "Donath Olomi" <olomi@yahoo.com>, "Nelson Kiwia"
Ndugu zangu,
Hongera. Ni maamuzi magumu haya lakini yanawezekana. Kimsingi
nilishaacha kuchangia baada ya kuacha kuchangisha. Harusi yangu
sikuchangisha, nilijiandaa mapema kwa sababu matukiyo yote hayo siyo
dharura, ni mbwembwe, na mbwembwe ni fedha. Ujumbe uendelee kusambaa.
Geoffrey mwa Ngulumbi
Mobile 0767 449 364/0783 449364

Von: Donath Olomi <olomi@yahoo.com>
An: Nelson Kiwia <nelkiwia@yahoo.com>; Chriss Shoo
<kncutsm@kilinet.co.tz>; "kncu@kilinet.co.tz" <kncu@kilinet.co.tz>;
Gesendet: 15:52 Donnerstag, 17.November 2011
Betreff: Re: MWISHO WA MICHANGO YA SHEREHE - REMINDER
Ezekiel
Nashukuru kwa reminder hii.
Mimi nateleleza tangu January, kama nilivyoahidi, na najua watu
wengine kadhaa ambao walikwishaacha kabla yangu na wengine wameacha
baada ya hii kampeni. Ukweli ni kuwa asilimia kubwa sana ya watu
wanakereka na tabia hii, ila wanashindwa kufanya uamuzi mgumu wa
kuacha. Kuna profesa mmoja ameniambia mkewe kamshauri wahame Dar maana
hii michango inawamaliza, wahamie mji ambao hawajulikani sana. Mimi
nimemshauri hawana haja ya kuhama Dar, ila waihame michango. Hebu
fikiria unapopeleka kadi ya mchango inavyowakera baadhi ya unaowapa
(ingawa watajifanya wanapenda kukuchangia) mpaka wanatamani kuhama
mji, halafu bado unapeleka tu??? Dr.Donath R. Olomi, P.O.Box 35036 Dar
es Salaam, Mobile : 255-754/715-296660 --- On Wed, 11/16/11, Ezekiel
Joachim <ezecjo@yahoo.com> wrote:

From: Ezekiel Joachim <ezecjo@yahoo.com>
Subject: MWISHO WA MICHANGO YA SHEREHE - REMINDER
To: "Nelson Kiwia" <nelkiwia@yahoo.com>, "Chriss Shoo"
<kncutsm@kilinet.co.tz>, "kncu@kilinet.co.tz" <kncu@kilinet.co.tz>,
maruojoseph@gmail.com, "rasonel2000@gmail.com"
<rasonel2000@gmail.com>, "christian.shoo@gmail.com"
<christian.shoo@gmail.com>, "Athanasio Masenha"
<athanasiom@yahoo.com>, "Jaq George" <jaqgeorge@yahoo.com>,
specioza2003@yahoo.com, "Donath Olomi" <olomi@yahoo.com>, "gideon
gabriel" <ggabriel@crdbbank.com>
Cc: matthias_07@yahoo.com, "PAULO MHACHE" <paulomhache@yahoo.co.uk>,
melyoki@udbs.udsm.ac.tz, nixonb52@yahoo.com, "restituta"
<repao2002@yahoo.com>, "jeff fungo" <jfungodz@yahoo.com>, "max
novatus" <maxnovatus82@yahoo.com>, "Nico Mwakilema"
<nickmwakilema@yahoo.co.uk>, "Mwkisole" <mwaki1982@yahoo.com>,
mwakip76@yahoo.co.uk, "geoffrey mwangulumbi" <ngulumbig@yahoo.de>,
"silvest felix" <slyfelix2003@yahoo.co.uk>, jntesha@yahoo.com
Date: Wednesday, November 16, 2011, 9:39 PM
(ujumbe huu niliusambaza January 2011 ila bado watu wananisumbua na
michango)
Ni hivi,
Nimekuwa nafuatilia jinsi desturi ya kuchangia na kufanya sherehe
kubwa inavyozidi kushika kasi, ikipelekea tabia isiyokuwa ana mshipa
wa aibu kuomba michango kiasi kwamba sasa hata mtu ambaye jina lako
halijui vizuri anataka kukuomba mchango wa sherehe au ya
kumunyo,ubarikio,ubatizo wa mtoto,birthday,graduation,kitchen
party,send off,harusi na nyingine kibao.
Aidha michango na sherehe hizi zimekuwa mzigo mkubwa sana kwa baadhi
ya watu,ikiwa ni pamoja na wale wenye kipato kidogo na kulazimika
kulipa michango hiyo kwa ulazima mkubwa kuliko hata bili za matibabu
za ndugu zetu wa katibu.
Je, wajua kuwa kuna familia ambazo zimefikia kulazimisha ndugu wauze
mashamba au mifugo mtaji ili kupata fedha za kufanya sherehe?. Je,
wajua kuwa kuna watu ambao zaidi ya nusu ya kipato chao wanatumia
kuchangia sherehe na huku wakishindwa kulipia huduma muhimu kama
shule, matibabu, lishe, nk. Na kuwa wakati mwingine wewe au mimi (au
wengine kama mimi na wewe) ndio wenyeviti na makatibu wa sherehe
hiyo?. Na ni sisi tunaoona fahari ya kutumia milioni 30 au zaidi
kwenye sherehe usiku mmoja?
Kuna kijana mmoja jamaa yetu juzi juzi alipata shule Australia akawa
anatafuta mchango wa dola 5,000 aende. Alipata 2,000 na amekwama
kwenda. Mwaka kesho akisema anaoa tutamchangia milioni 15-20!!!. Hii
si hadithi, ni ukweli, na ni kielelezo cha ulimbukeni tuliofikia.
Siku za karibuni nimetambua kuwa kuna kundi kubwa tu linasikitishwa na
huu mwenendo, na hata kutambua kuwa tunaweza kuwa tunaandikiwa dhambi
kubwa (na hukumu yatusubiri) kwa jinsi wengi wetu tunashindwa kusaidia
mambo ya msingi lakini tunakuwa wepesi kutoa kwenye sherehe. Wengi
wanaamini kuwa tumeshatumbukia kwenye lindi la mazoea ambapo hatuwezi
kujitoa mpaka upepo uje ubadilike wenyewe!. Mimi nafikiri wasomi tuna
jukumu muhimu la kuwa chachu ya mabadiliko pale ambapo mazoea yenye
madhara yanavuka mipaka na kuweza hata kuwa chanzo cha ufukara na
kuviza maendeleo.(be a change agent)
Ili kubadilisha hili jambo, lazima tuanzie mahali. Mimi nimeamua na
kuanza kutekeleza.
Kuanzia Januari 2011, niliamua kupunguza michango ninayotoa. Natoa tu
kwa mtu wa karibu sana, na ni kiasi kidogo. Usishangae nikakuchangia
20,000/= kama ulitegemea 50,000/= kwa mfano. Kuanzia July 2011,
nilipanga kuacha kabisa kuchangia sherehe. Badala yake nitakuwa
nachangia elimu pale ambapo mzazi hayupo au mhusika kweli hana uwezo
na pia nitachangia miradi mingine ya jamii na maendeleo.
Je waniunga mkono? Kama ndiyo acha sasa na sambaza huu ujumbe kwa
mtandao wako.
Ezekiel Joachim
+255 784 371338, +255 713 371339, +255 767 371338





On Aug 8, 1:45 pm, "Donath R.Olomi" <ol...@imedtz.org> wrote:
> Ndugu zangu,
>
> Disemba 2010, niliandika waraka wa kuhimiza kubadili desturi ya
> kuchangisha mamilioni ya fedha kwa ajili ya kufanya sherehe kubwa, nikitoa
> mifano hai jinsi michango hii inavyowaumiza baadhi ya wachangaji, na
> kuathiri maisha yao. Vile vile nilielezea umuhimu wa wasomi kuwa chachu na
> viongozi wa kubadili desturi ambazo zinaleta madhara, ikiwemo ya kuchangia
> sherehe kubwa. Ikumbukwe kuwa desturi ikishajengeka, inajijengea uhalali
> wake na kuibadili kunahitaji msukumo.
>
> Nafurahi kuwa karibu kila aliyechangia mjadala ule aliuunga mkono, na pia
> kwamba kuna ambao walishaanza siku nyingi kuacha kuchanga na kufanya
> kampeni hii hata kabla ya waraka wangu (ona kiambatanisho).
>
> Napenda pia kuwafahamisha kuwa, nimefanikiwa kutimiza ahadi yangu, na sasa
> nashiriki kuchangia tu sherehe ndani ya familia.  Taratibu idadi ya kadi
> za michango ninazopata imeshuka na sasa imekaribia 0. Pia kuna watu wengi
> wanaonizunguka ambao wameniambia kuwa kadi za michango wanazopata
> zimepungua. Kuna watu nafahamu walikuwa wakigawa kadi kwa kila wamjuaye
> miaka ya nyuma, lakini sasa wanapooza au kuozesha wanachagua nani wampe
> kadi.  Pia watu ninaowafahamu wanaopata kadi na kuacha kuzichangia bila
> kuona aibu wameongezeka. Kwa hiyo tumepiga hatua. Natamani tungekuwa na
> utafiti wa kisayansi kuona hii desturi inavyobadilika.
>
> Nashukuru sana kwamba kuacha kuchangia harusi hakujaniletea matatizo
> yeyote ya kuharibu mahusiano na watu wengine. Kuna watu sikuchangia harusi
> zao na za wanao na uhusiano wetu umezidi kuimarika. Kwani kutoa kwa ajili
> ya kujenga mahusiano lazima iwe kwa kuchangia sherehe tu? La hasha. Kuna
> wachache wamekuwa wakinialika kwenye sherehe zao ingawa sijachanga � kwa
> sababu ya ukaribu wetu � nami nakwenda kwa sababu ya ukaribu. Na mimi
> nikiwa na sherehe nitakualika si kwa sababu umenichangia, ila kwa kuwa
> ningependa uwepo kama mtu wa karibu.
>
> Leo napenda kuwashirikisha mawazo yaliyotolewa katika huu mjadala.
> Unaposoma na hata unapoongea na watu mtaani, unaona kuwa jamii imelichoka
> hili jambo, na ingependa libadilike, ila tu baadhi wanaogopa. Wako
> wachache wanapenda liendelee, ama kwa sababu kweli wanaamini ni jambo
> zuri, ama kwa sababu linawasaidia wao moja kwa moja. Hawa hatuna la
> kufanya mbali na kuwanyima michango wabadilike kidogokidogo.
>
> Kuna ambao wanasema sherehe zinasaidia uchumi. Kwani fedha isipotumika kwa
> sherehe si itatumika kufanya kazi nyingine ambazo zitajenga uchumi ambazo
> hazifanyiki kwa kuwa fedha zinakwenda kwenye sherehe kubwa? Kiuchumi
> tunasema kila kitu kina �opportunity cost�. Unachokitumia huku unashidwa
> kukitumia kule�  Wanaochanga wangetumia fedha hizo kwenye ada, kujenga
> nyumba, kukarabati choo kilichoharibika, kuboresha lishe nyumbani, nk.
> Hivi navyo vinajenga uchumi.
>
> Naomba kuwasilisha
>
> Na tafadhali sambaza, na tushirikishe uzoefu wako
>
> --
> �Give your energy to things that give you energy.�,
>
> �Learn enough to begin and then learn as you go.�
>
> Dr. Donath R.Olomi
> Chief Executive Officer
> Institute of Management and Entrepreneurship Development (IMED)
> Mwalimu  House 7th Floor, Ilala
> P.O. Box 35036 Dar es Salaam, Tanzania E-mail: i...@imedtz.org, website:www.imedtz.org
> Mobile +255-754-296660
>
>  MAFANIKIO KUELEKEA MWISHO WA MICHANGO YA KUFANYA SHEREHE KUBWA.docx
> 111KViewDownload

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment