Sunday 26 August 2012

[wanabidii] RE: Dr. Amur nasubiri jawabu - SENSA Duuu/Mjadala wa kuhimiliwa!

Ahsante Kaka Mhamed Lodhi,
Kwa kuniletea "vihondo" hivi.
A LUTTA CONTINUA!
Slm Hmd M. B/Tosha



Date: Sat, 25 Aug 2012 11:47:42 +0200
From: lodhimy@gmail.com

---------- Forwarded message ----------
From:
Unique Maher
Date: 2012/8/25


Daktari Amur, ningependa hili neno ulilolitumia la "KWANINI" uligeuze likuelekee na ujiulize nafsi yako "Kwanini" tumeharibu haya unayoomba kwanini yasifanywe wakati yalikuwepo na Wazanzibari wakifaidika nayo na badala yake Mapinduzi yameyapinduwa yakapinduka na leo mtu kama wewe ukawa unajifanya huyafahamu na kupoteza muelekeo wa mjadala wa madai ya Waislamu na kuwageuzia ubao wakati ukweli unaufahamu!
 
Amur, tueleze vile vyoo vya serikali vilivyokuwa mijini, mitaani na majiani ambavyo vilikuwepo na kusafishwa na vyenye maji vyote viko wapi! na nani kaviondosha ukiwacha kilichofanyiwa ukarabati forodhani na Aga Khan pamoja na bustani iliyopo hapo.
 
Amur, hufahamu kuwa mitaro na karo zote Zanzibar zikiangaliwa na kusafishwa na kupeleka pwani mbovu na sehemu nyengine za bahari! na nyakati za mvua maji hayakuwa yakisimama hata siku moja na karo ikiziba haifiki saa watu wenye kazi zao wakija kuzibua na kusafisha!
 
Amur,ikowapi mifereji ya serikali iliyokuwa imejaa vururu mpaka ngambo(u) ambayo ikiwasaidia wananchi kuteka maji bure!
 
Amur, pako wapi pakufulia (Chanoni/vyanoni) kama weles na saateni mulimokuwa sehemu maalum palipotengwa/kuwekwa kwa wananchi bure na maji teleeee!
 
Amur, yakowapi yale magari yakukusanyia taka mijini!
 
Amur, vinu vya taa viko wapi vilivyokuwa vikeneza umeme karibu nchi nzima!
 
Amur, kama Daktari unayefahamu huduma za afya, yale magari ya Ambulance ambayo yakihudumu na kufika mashamba yote kwenda kuchukuwa wagonjwa wakati wote yalipohitajika kwenda, yakowapiiiii?
 
Utapojibu unipe kigezo kutokana na hayo niliokuuliza na ufahamu " Kubomoa rahisi, kujenga kazi"
 

Waislamu tutaendelea kuhamasisha waislamu wenzetu yenye maslaha kwa waislamu na sisi sio kama Bakwata unayoifahamu wewe na kufanya kama walivyomfanyia Professor Kigoma Ali Malima baada ya kutoa taarifa jinsi waislamu wanavyokandamizwa na kubaguliwa katika nyanja zote za maendeleo ya kijamii na kielimu na makatoloki - Tanganyika.
 
 

Date: Thu, 23 Aug 2012 23:15:47 +0100
From: amurpost@yahoo.de



Assalam Aleykum! 

 Jambo linalonishangaza watu kuandaa uhamasishaji dhidi ya SENSA  kwanini tusiandae uhamasishaji ili tujenge Muslim Medical Centre Tanzania ambayo ina Medical School ili tuweze kusomesha  Elimu ya Medicine vijana wetu na tutowe matibabu kwa ajili ya UMMAH. Kwa idadi yetu Zanzibar tunahitaji Hospital za 5 Mkoa na Moja ya Kitaifa .Huko Tanzania tunahitaji Hospital  125 za wilaya , 26 za Mikoa ,  na 5 za Rufaa zaidi.

Vijana wengi safari hii wamefutiwa mitihani na wengine kutofaulu mitihani kwa njia moja au nyengine kwanini tusiuunganishe School zetu zote zifanye mtihani ya Delhi Public Exams,or EDEXCEL GCE,or Sudan Secondary School Certificate?

Maeneo mengi haya maji Salama kwanini tusihamasishe ujenzi  Artisan Wells ili kupata maji salama na pia kujenga vyoo vya kisasa vyenye standard drainage System.

Mazingira yetu ni machafu kwani tusiendeleze uswafi?

Kwanini tusiiimarishe Kilimo na Ajira kwa vijana kwa kuutenengeza Mfuko wa Zakaah?

Tuwache kulalamika na tuungane kuleta Maendeleo ya Jamii.

Tuachane na Taasisi zinazoleta Mivutano na Kasumba tupiganie Truth and Reconciliation kwenye Jamii zetu na Nchi Nzima.


AMUR




Von: Suleiman59 <malkindymalkindys@yahoo.co.uk>

Gesendet: 0:51 Freitag, 24.August 2012


Hapo mwanzo tulikuwa hatuyajui wenzetu wana agenda ya Siri ndio tukataka sass kipengele hicho kipmgezwe kutimiza twende na wakati 

Sent from my iPhone

On 23 Aug 2012, at 08:33 PM, Salma Khamis  wrote:

Bwana Sule karibu Gongo la Mboto, sasa hivi nipo Zanzibar nakula
skukuu for only a week!
 
Kwahio vipindi vya nyuma katika kuhesabu watu (sensa) kipengele
cha dini kilikuwemo?
 

nimekula haya makongoro/falfa nasikia kichefuchefu, aakhh!
 

 
2012/8/23 Suleiman59
Salma inawezekana kwa muono wako wa Gongo la mboto Mina ajili ya dini ina umuhimu ukweli usiokatalika data zilizopita zinaonesha waislam na wakirosto wapo balance ukweli wa mambo wakiristo hawazidi robo moja kwanini wanajiongeza hesabu sifafaham pana agenda ya Siri hapo hapana ubaya tukajijua Japo mataifa ya ulaya sasa dini Haina nafasi sababu makanisa yamehamwa ukweli ushadhihiri

Sent from my iPhone

On 23 Aug 2012, at 07:20 PM, Salma Khamis  wrote:

Sensa ya nchi na dini vina maingiliano gani?
 
Kipengele cha dini kitiwe kwa min-ajil gani?
 
By the way, masheha wawache utumbo wao wa kuwanyima
wananchi vitambulisho.
 
Mi mwenzenu labda mengine yananipita, lakini sioni sababu ya
watu kukataa kuhesabiwa kwa sababu za kidini ambazo wamezikuza!
 
 
 
Salma Khamis/

2012/8/23 Salma Said
Asalamu Alaykum.

Juzi Taasisi za Kiislamu ziliitisha waandishi wa habari zilitoa tamkoa la kuelezea msimamo wao wa kususia sensa kwani haikuwa habari mpya kwa sababu tayari nilishawahi kuripoti msimamo huo wa kususia sensa. Taasisi hizo chini ya Amir Msellem Bin Ally alielezea mambo mawili matatu ya kuonesha kutoshiriki kwako hadi hapo zanzibar itakapokuwa huru, na hatawatkubali kuhesabiwa kama mkoa, wanataka watu wapewe vitambulisho vya mzanzibari mkaazi, wanataka suala la kipengele cha dini kiingizwe katika sensa, wanataka kusitishwa kwa vitambulisho vya Tanzania kupewa wazanzibari kwa kuwa wazanzibari wana vitambulisho vyao.

Kufuatilia taarifa hizo jana televisheni na radio nazo zikasikika ofisi ya Mufti ikitoa taarifa kwamba kuna baadhi ya masheikh wamekwenda ofisi ya mufti na baadhi ya taasisi za kiislamu zikikanusha kuhusika na kutoa tamko la pamoja la taasisi za kidini kuhusu kususia sensa wakisema wanakanusha kwa kuwa taasisi hizo zitashiriki na hazina sababu ya kupingana na serikali.

Na leo masheha na madiwani wote wa zanzibar wameitwa katika hoteli ya bwawani kufahamishwa namna ya kuhamasisha suala la sensa na kufahamishwa utaratibu utakavyotumika baada ya semina fupi ya kufahamishwa utaratibu baadhi ya madiwani wamsimama na kulaumu utaratibu unavyotumika ikiwa pamoja na wao wenyewe kutopewa umuhimu katika masuala mbali mbali hasa hili la sensa lakini zaidi waliongea ni masheha na madiwani wao wamesema hawana umuhimu hivyo wanaawaachia masheha wenyewe.

Lakini masheha kwa upande wao wanaosimama wameongea mengi mbali ya kulaumu lakini wametaka vyombo vya habari vidhibitiwe na vifugiwe kwa sababu vinakwenda kinyume na serikali lakini pia wamenichekesha pale wanaposema kwamba hii ni serikali ya mapinduzi huku mmoja wao akijigamba kwamba yeye mwenyewe amepindua na ninavyomtazama umri wake naona kama tumepishana mimi na yeye basi ni kidogo sana kwa umri lakini amesema hivi viredio vidogo vidogo vifugiwe na vichukuliwe hatua visiachiwe kutuparaganya kwa sababu sisi tunafanya kazi kubwa wao wanawakoroga wananchi?
Duuu yaani uhuru wa maoni usiwepo kitakachoamuliwa na watu fulani ndio hicho hicho tu? tunasonga mbele au tunarudi nyuma?

Na jana nilimsikia mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi yeye amekwenda mbali zaidi akisema watakaokataa kushiriki katika sensa basi watachukuliwa hatua na watafunguliwa kesi lakini sio hivyo tu akasema watakapokaa kuhesabiwa katika sensa basi wafahamu kwamba majimbo ya Pemba tayabaki mawili tu kwa kuwa mengine yote yatafutwa maana yataonekana hayana watu kwa kuwa wamekataa kuhesabiwa. 

Anachokisema Dadi ni upotoshaji mkubwa sana wa kugeuza ukweli na ikiwa viongozi wanaweza kutumia vyeo vyao kuwadanganya watu ni hatari sana.

Nakumbuka muda siku tuliofanyiwa semina na watu wa takwimu ambao ndio waratibu wa sensa nilisimama na kusema kwamba tusijidanganye kwamba tuwapuuze watu ambao wanasema hawatashiriki na wala tusiseme kwamba hao watu ni wachache kwa sababu suala hili limekwenda katika imani za watu na tunapoleta jambo katika imani za dini basi ujue jambo hilo litapata nguvu kwa hivyo tuliishauri serikali kukaa pamoja na watu ambao wanapinga sensa wakishamaliza vikao vyao na kukubaliana au kutokukubaliana basi ndio waite waandishi watoe taarifa kwa umma lakini sasa kinachoendelea ni mikanganyiko ya mawazo na misimamo na katika hili wananchi wengi wapo njia panda. 


Lakini pia kuna suala la makarani wa sensa kwenda kupata vitisho na huenda wakapata madhara kwa sababu tayari vitisho kwa baadhi ya watu vimeshaanza na hili wapo ambao wenye chuki za makusudi wanaweza kutumia fursa hiyo na kuingiza chuki zao   wakati huo. Ni hatari na hakuna usalama wa uhakika na hivyo baadhi ya watu wamekuwa na khofu na kuhesabiwa kwa kuogopa kudhuriwa na wenzao wenye kususia lakini pia wanaosusia pia wamekuwa na khofu na kuogopa kudhuriwa na wenye kutaka kuhesabiwa. Naona kitandawili hiki ni kigumu lakini waswahili wanasema 

Serikali itapoteza fedha nyingi kwa jambo ambalo naona lnaweza kuleta matatizo baadae sensa itafanyika lakini haitafanikiwa kwa 100% kama ambavyo wamekusudia na wale ambao wametaka watu wasusie watasusia lakini hawatafanikiwa 100% kama walivyokusudia.  

Najua vikao kati ya masheikh na serikali vinaendelea lakini mimi jana nilihoji kwa baadhi ya masheikh kwa nini basi masheikh wametoka hadharani kukazia msimamo wao wakati bado wapo katika vikao? nikaambiwa tunasubiri na ikiwa tutakubaliana kwamba tujitokeze basi tutatangaza? nikauliza tena jee mnataka kufanya kama mlivyofanya kwa tume ya maoni mnapanda majukwaani ijumaa kuwaambia watu tume ya warioba mwisho chumbe halafu jumapili mnawaita tena mnawaambia wajitokeze katika tume wakati mnajua tume inakuja jumatatu? nikajibiwa ahhhhhh ndio mambo.

Naomba kuwasilisha 

Salma Said  
 
 
Salma Said,
P. O. Box 1442,
Tel: +255 (024) 223 5219
Mobile: +255 777 477 101
E-mail: muftiiy@yahoo.com
      


_______________________________________________
Zanzinet mailing list
Zanzinet@zanzinet.net
http://zanzinet.net/mailman/listinfo/zanzinet_zanzinet.net




--
Regards/
SALMA KHAMIS.
_______________________________________________
Zanzinet mailing list
Zanzinet@zanzinet.net
http://zanzinet.net/mailman/listinfo/zanzinet_zanzinet.net




--
Regards/
SALMA KHAMIS.

_______________________________________________
Zanzinet mailing list
Zanzinet@zanzinet.net

http://zanzinet.net/mailman/listinfo/zanzinet_zanzinet.net



_______________________________________________ Zanzinet mailing list Zanzinet@zanzinet.net http://zanzinet.net/mailman/listinfo/zanzinet_zanzinet.net

_______________________________________________ Zanzinet mailing list Zanzinet@zanzinet.net http://zanzinet.net/mailman/listinfo/zanzinet_zanzinet.net

_______________________________________________
Zanzinet mailing list
Zanzinet@zanzinet.net

http://zanzinet.net/mailman/listinfo/zanzinet_zanzinet.net



0 comments:

Post a Comment