Sunday 26 August 2012

[wanabidii] Nyota wa NBA waendesha mafunzo ya kikapu Dar

Nyota wa kikapu Luol Deng wa Chicago Bulls na Hasheem Thabeet wa Oklahoma City Thunder wameendesha mafunzo ya kikapu kwa vijana wadogo chini ys miaka 18.

Mafunzo hayo yalifanyika katika viwanja vya Don Bosco, ijumaa na jumamosi jiji Dar Es Salaam.

Pia mafunzo hayo yalihudhuriwa na Makamu wa Rais wa NBA Afrika ndugu Amadou, Kocha wa NBA na Mkurugenzi wa Ufundi wa NBA Afrika Jobby na Meneja Mkuu na Makamu wa Rais wa timu ya Denver Nuggets ndugu Masai.

Ujio wa nyota hao na vigogo hao NBA ni faraja kubwa kwa kikapu Tanzania na ni matumaini yetu itakuwa ni chachu ya kukuza mchezo huo nchini.

Pia mazungumzo yalifanyika kati ya viongozi wa TBF na NBA kuangalia namna ya NBA kusaidia kuendeleza mchezo wa kikapu nchini na hususani katika maeneo ya miundombinu na kusaidoa kujenga uwezo wa kiufundi kwa makocha wazalendo ili kuwa na maendeleo endelevu katika kikapu.

Kwa niaba ya Shirikisho la mpira wa kikaupu Tanzania tunawashukuru wachezaji hao na viongozi wote wa NBA na tunaishukuru sana kampuni ya CocaCola kupitia kinywaji cha SPRITE kwa kudhamini mafunzo hayo.

Phares Magesa
TBF Vice President

Attached photo from left Chicago Bulls' Star Luol Deng, TBF-VP Magesa, NBA Vice President for Africa Amadou, NBA Africa Technical Director Coach Jobby at the Julias Nyerere International Airport .


Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment