Sunday 5 August 2012

[wanabidii] Muungano wa Kikatiba hauhimili mageuzi ya kikanda na ya kimataifa

Na Khalid Gwiji

Muungano wa Katiba uliopo umekuwa ndio chanzo cha migogoro yote ya
muungano huu. Watanzania wote ni mashahidi wa jinsi mfumo wa aina hii
ulivyoshindwa kuweka utulivu na maridhiano katika mahusiano ya nchi
zetu mbili. Zaidi ya yote umeshapitwa na wakati na hauwezi kuhimili
mageuzi ya kikanda na kimataifa yanayotokea.

Mbali na kero zilizoshinda za humu humu ndani, lakini tuchukulie mfano
mdogo wa kuwepo kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na ushiriki wa
Tanzania. Zanzibar haimo kama mwanachama katika Jumuiya hii bali
iliyomo ni Tanzania. Kati ya mambo 18 yanayoshughulikiwa na Jumuiya
hii, ni mambo 4 tu ambayo ni ya muungano na ambayo Tanzania ina
mamlaka ya kisheria kuiwakilisha Zanzibar. Kwa yaliyobakia 14 Tanzania
kuiwakilisha Zanzibar ni kwenda kinyume na Katiba.

Hata suala la Zanzibar kujiunga na OIC lilikwamishwa kutokana na mfumo
wa muundo huu na Tanzania ikadai ingejiunga kwa vile ndio yenye
mamlaka. Takriban inakaribia miaka 20 tokea kutolewa kwa ahadi hio
lakini wananchi hawajaelezwa maombi yalikwama wapi.

Hata hivyo, hili la OIC ni utashi wa kisiasa au kidini tu ndio
uliokwamisha; lakini mfumo huu wa Muungano wa Kikatiba unasutwa hata
na maumbile ya mataifa haya yaliyoungana. Kwa mfano upo umoja wa
visiwa vya Bahari ya Hindi ambao Zanzibar kama kisiwa wanastahiki
kujiunga, lakini Zanzizibar ambayo ni kisiwa inaambiwa haina mamlaka;
na hio Tanzania yenye mamlaka haiwezi kujiunga kwa vile sio kisiwa –
hii imepelekea Zanzibar kukosa haki zake mbali mbali za kimaendeleo.

Njia pekee kwa sasa ambayo itakata mzizi wa fitina ni kuwa na
Mashirikiano ya Mkataba na si ya Kikatiba. Haya ni mashirikiano mema
ambapo kila nchi inajitegemea na inabaki na serikali yake, na
uendeshaji wa mambo yake, utaifa wake n.k, na huingia katika
mashirikiano kwa njia ya Mkataba (Treaty) juu ya mambo maalum yaliyo
wazi na kwa utaratibu wanaokubaliana hizo pande mbili au zaidi
zinazoshirikiana.

Mifano ya aina hii ni kama EAC (Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na
Burundi) na Europena Union ulio na nchi wanachama 27. Uzuri wa muundo
huu ni kuwa unatoa fursa kwa nchi zilizoshirikiana kuweza kuuagalia
kila inapobidi ule mkataba wao bila vikwazo vya Kikatiba na hivyo
kusukuma mbele maslahi yao bila kumezana, kubebana au kuoneana.

Jamhuri ya Watu wa Zanzibar Kwanza – JWZK!

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment