Thursday 23 August 2012

[wanabidii] Luol Deng na Hasheem Thabeet kuendesha mafunzo ya kikapu

Wachezaji nyota wa NBA Luol Deng wa Chicago Bulls na Hasheem Thabeet wa Oklahoma City Thunder wako jijini Dar Es Salaam.

Wachezaji hao wataendesha mafunzo ya kikapu kwa vijana wadogo walio na umri chini ya miaka 18.

Mafunzo hayo yatafanyika viwanja vya Don Bosco, Upanga ijumaa 24/08 na jumamosi 25/08 kuanzia saa 4 asubuhi.

Pia Makamu wa Rais wa NBA anaeshugulikia Afrika Ahmadou na maofisa wengine wa NBA wako jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo na TBF kuhusu maendeleo ya mchezo huo nchini.

Mafunzo haya yamewezeshwa na Kampuni ya Cocacola kupitia kinywaji cha SPRITE, tunawashukuru sana.

Wote mnakaribishwa katika viwanja vya Don Bosco.

Phares Magesa
Makamu wa Rais
Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF)

Pichani ni Luol Deng na Phares Magesa wakiwa katika mazungumzo katika katika chumaba cha wageni Mashuri uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment