Sunday 12 August 2012

[wanabidii] KWANINI MTOTO ASIZALIWE AKIWA NA MIEZI TISA???

Wadau

Kama nitawaudhi nitaomba radhi.

GHivi kwanini mtoto anapozaliwa tusiseme tayari ana miezi tisa? Kwanini akizaliwa tuseme ndio ana siku moja amezaliwa?

Unajua kwanini nauliza hivo?

Leo nimekwenda church, bahati nzuri akawepo mama anambariki mtoto wake machanga mwenye takribani wiki moja hivi amezaliwa. Kama kawaida yake, Mchungaji akasimama kwa ajili ya kumbariki na kumwombea baraka. Sasa basi, alipotamka maneno haya kuwa "mama huyu anakuja kumshukuru Mungu na kumwombea baraka kwa Mungu mwanae ambaye amembeba tumboni mwake kwa miezi tisa"--Ameen!!

Hapo hapo likazuka swali kichwani mwangu, hivi kwanini tusianze kuhesabu siku ya kwanza mimba inatungwa?? maana ule nao ni uhai!

Kwa mantiki hiyo mtu kama Finnigan wa Simbeye tuseme akiwa na miaka 41 tuongezee na miezi tisa?

Kwani uhai unaanza pale mtu anapokuwa ame-tia timu duniani au pale mimba inapotungwa?

A S Kivamwo


0 comments:

Post a Comment