Tuesday 21 August 2012

[wanabidii] KIKWETE AMKATA MAINI MOBHARE MATINYI PIA

KIKWETE AMKATA MAINI 
MOBHARE MATINYI PIA!

Bw. Matinyi kazizowea siasa za kikoloni
Hata Unguja atataka ivamiwe ikitaka kuacha Muungano


Zanzibar, Tanzania
Kwa RAIS Jakaya Kikwete kusema kuwa hajaliagiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupigana vita na Malawi kwa sababu za mpaka wa Ziwa Nyasa 
kati ya nchi hizo mbili aliwakata maini sio Membe na Lowassa tu, bali mpaka yule muandishi mkorofi wa gazeti la The Citizen anaejulikana kwa jina la 
mapambano (nom de guerre) kama Mr Eagle, wakati jina lake hasa ni Mobhare Matinyi.
Katika ukumbi wa Wanabidii Bw. Matinyi bila ya haya na bila ya kuwa amelewa gongo alinukuliwa akiandika…" …invade Malawi (because Lilongwe won't listen), 
kick out every stupid guy and restore a new sensible government. We did it in Uganda, why not in Malawi? After all Joyce Banda has already said that she 
is ready to die for her country - so let us help her."



0 comments:

Post a Comment