Thursday 16 August 2012

[wanabidii] Balozi Kagasheki akanusha uvumi wa kuwahamisha wamasai

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Khamis Suedi Kagasheki
amekanusha uvumi unaosambazwa na Shirika moja kupitia mtandao wake wa
AVAAZ.org kuwa watanzania wa Jamii ya Kimasai wapatao 48,000
watahamishwa kutoka eneo lao (la Serengeti) kupisha Wafalme kutoka
Mashariki ya Kati ili walitumie eneo hilo kwa uwindaji wa Simba na
Chui.

Taarifa hiyo iliyosambazwa na mtandao huo imewataka watu kutoka
duniani kote kujiorodhesha ili wafikie angalao 150,000 ili
kumshinikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuacha kusaini
mkataba ambao utafanya uhamisho huo utekelezwe.

Waziri Kagasheki amesisitiza kuwa uvumi huo siyo kweli na hauna msingi
wowote kutokana na sababu zifuatazo:

Kwanza, hatua kama hii haiwezi kuchukuliwa na Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika Hifadhi ya Serengeti maana hakuna watu wanoishi ndani
ya hifadhi hiyo. Pia kitendo hicho hakijapangwa kufanyika katika
Wilaya ya Serengeti iliyoko mkoani Mara.

Pili, hata kama taarifa hiyo ilimaanisha Wilaya ya Serengeti mkoani
Mara, bado siyo kweli maana wilaya hiyo haina idadi ya Wamasai
wanaofikia jumla ya 48,000.

Tatu, ndani ya ya Hifadhi ya Serengeti hakuna eneo lolote ambalo
limetengwa kwa ajili ya wafalme wa Mashariki ya Kati ili waweze
kulitumia kwa uwindaji wa Simba na Chui.

Nne, habari hizo siyo kweli maana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania hahusiki kabisa na ugawaji wa vitalu vya uwindaji popote pale
nchini. Hii ni kazi ya Wizara ya Maliasili na Utalii, na Wizara
haijafanya hivyo katika eneo tajwa.

Pamoja na ufafanuzi huo Waziri Kagasheki amewaasa watu
waliojiorodhesha, na wanaotarajia kujiorodhesha, kuwa wamepotoshwa,
hivyo wanatakiwa wasisaini kubariki kitu mbacho hawakijui wala hakipo.

[MWISHO]

George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Tarehe 15 Agosti 2012
Simu: +255 784 468047

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment