Wednesday 22 August 2012

[wanabidii] Anguko la Kafumu na Mapinduzi ndani ya CCM-UTENZI

Kafumu amevuliwa ubunge,
Makosa Ya 'wahafidhina' wa CCM,
Wale wasioyaona mabadiliko,
Wasiotaka kuyaishi mabadiliko,

Wasioyakubali mabadiliko.
Wamefanya 'uvundo wa kisiasa',
Wameukasirisha umma,
Wameumbuliwa na Mahakama,

Pole sana Kafumu!
Pole sana mwana mawasiliano mwenzatu.
Kwa jeuri na ulevi wa madaraka,
Wasiostahili, wamekusababishia usichostahili.

Hukumu imeshatoka,
Taji la ubunge umevuliwa,
Mjengoni hawatakuona,
Pumzika, anza upya.

Ole wako CCM,
Ole kwa jeuri ya waliomo ndani yako,
Wakitumia rasilimali za umma,
Wanakiuka yaliyo ya umma.

Wanajivisha jeuri ya kutoguswa,
Wafanye wanalolitaka,
Watishie pasipo soni,
Wakiuke kwa matarajio,
Kwamba watadumu siku zote.

Amka enyi mlio wa CCM,
Mapinduzi ya haki myaibue,
Hasira zenu ziwaondoe wasioistahili jamii.
Watoke, watoke kabla hamjatoka.

Msibwete enyi wana wa CCM,
Mkayaona mabaya na kuyaacha,
Kwa vile yanatendwa na wenye majina,
Mkashindwa kuwakemea, kuwatimua.

Mtayaonja mauti ya kisiasa,
Kwa uzembe wa wasio haki,
Wakitisha na kukiuka,
Ubunge wenu mkavuliwa.



....Mwenye beti za tenzi zaidi anaweza kuziongeza. Tuone kama CCM sikivu itatusikiliza.









0 comments:

Post a Comment