Wednesday 22 August 2012

RE: [wanabidii]

Egidius Mwabuki

-----Original Message-----
From: wanabidii@googlegroups.com [mailto:wanabidii@googlegroups.com] On
Behalf Of frank John
Sent: Wednesday, August 22, 2012 12:28 PM
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Na mimi niliandika hivi kuhusu bastola ya Rage

Tony quote "nimeongea na mtu aliye na Rage huko Igunga muda mfupi.......
Rage ana pistol lakini haina mkoba na ni ndogo inakaa mfukoni mwa
suruali.....". Tena " hiyo ni simu jamani! ..... Rage awezikuwa mjinga
mnavyomdhania.."
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

-----Original Message-----
From: denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
Date: Wed, 22 Aug 2012 08:27:01
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: Re: [wanabidii] Na mimi niliandika hivi kuhusu bastola ya Rage


Hatukumbuki. Unaonaje tukikumbushana?
On 22 Aug 2012 11:14, "frank John" <msike24@hotmail.com
<mailto:msike24@hotmail.com> > wrote:
Unakumbuka comments za Tony PT? Kuhusu picha ya Rage na mguu wa kuku
kiunoni?
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

-----Original Message-----
From: Mashaka Mgeta <mgeta2000@yahoo.com <mailto:mgeta2000@yahoo.com> >
Date: Wed, 22 Aug 2012 07:51:48
To: <wanabidii@googlegroups.com <mailto:wanabidii@googlegroups.com> >
Subject: [wanabidii] Na mimi niliandika hivi kuhusu bastola ya Rage



Septemba 28, 2011, niliandika makala kwenye NIPASHE kupitia safu yangu ya
MTAZAMO YAKINIFU inayotoka kila Jumatano, nikikemea kitendo cha Rage
kuonekana na bastola kwenye mikutano ya kampeni za Igunga. Wakati nilikuwa
kikazi nchini Kenya. Makala yenyewe ni hii hapa chini:-



Amani, utulivu na bastola ya Rage `nje nje`!
Na Mashaka Mgeta
 
28th September 2011
 
Ni tukio la aibu, linalofedhehesha na kustahili kuwekwa kwenye kumbukumbu
za viashiria vya ulevi wa madaraka, ukosefu wa maadili na uchafuzi wa
kijamii unaofanywa na watawala.
Mbunge wa Tabora Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ismail Aden Rage,
ameonekana katika kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunga mkoani
Tabora, akiwa na bastola.
Hakuna tasfiri rahisi inayoweza kupatikana kutoka katika picha na dhamira
ya Rage kama si ujeuri, vitisho na kuudharau umma.
Ni kitendo kisichostahili kuvumiliwa na mamlaka yoyote ndani ya taifa
linalojali na kutekeleza utawala wa sheria, haki na usawa kwa raia wote.
Katika kusanyiko la raia wasiokuwa na hatia, wenye umri wa kuanzia utoto,
ujana hadi uzee, wakiwa kwa jinsia za kike na kiume, Rage anajitokeza,
anapanda jukwaani huku bastola iliyo maarufu kama 'cha moto' ikionekana
kiunoni!
Sijasikia karipio la aina yoyote kutoka kwa mtawala wa ngazi yoyote, zaidi
ni 'kuipoza jamii', kwamba atahojiwa ili kupata ukweli wa nia hiyo.
Lakini ni tukio linalomgusa Mbunge kupitia chama tawala ambaye alifikia
hatua hiyo mbele ya askari polisi, usalama wa taifa na viongozi kadhaa
katika CCM na serikali.
Sikuwepo katika mkutano huo, lakini historia inayotokana na hulka ya 'ulevi
wa madaraka', inawezekana Rage alishangiliwa.
Inawezekana washangiliaji walianzia jukwaa kuu, wakafuata `wapambe'
waliovalia fulana, kofia ama skafu za njano na kijani, zikiwa na alama ya
jembe na nyundo inayotumiwa na CCM.
Inawezekana ilikuwa hivyo kwa maana mkutano ambao Rage aliamua kuonyesha
bastola hadharani, uliandaliwa na kuhutubiwa na viongozi wa chama hicho.
Je, Rage alitaka kuujulisha umma kwamba iwe iwavyo, silaha kama hiyo ni
sehemu ya nyenzo zinaweza kutumika kufanikisha matokeo ya uchaguzi mdogo wa
Igunga?
Je, Rage alitaka kuwasilisha ujumbe ya kwamba, kama alivyojidhihirisha
machoni mwa waliohudhuria mkutano huo, 'vigogo' wenzake pia walikuwa
wamekamilika hivyo kuwa mfano wa vitisho kwa wapiga kura wa Igunga?
Rage alikusudia nini kuonyesha bastola hadharani! Kwamba angeweza kuifanyia
kazi wakati wowote na kwa yeyote aliyekuwepo na ambaye angeonyesha upinzani
dhidi ya kauli zake jukwaani?
Hayo ni maswali machache miongoni mwa mengi ambayo yakiorodheshwa kwa
ujumla wake, safu hii haitatosha.
Kwa namna iwayo yote, zipo sheria, taratibu na kanuni zinazowaongoza
wamiliki wa silaha kama bastola aliyoinyesha Rage, ambapo ninaamini kwamba
kuionyesha hadharani si sahihi.
Rage akiwa amevaa shati la rangi ya kijani, lisilokuwa na ufito wa njano
(pengine kutokana na uachana wake katika klabu ya mpira wa miguu ya Simba
inayotumia rangi nyekundu, ikiwa ni mpinzani wa Yanga inayotumia rangi ya
njano), ameonyesha `jeuri' ya kumiliki bastola.
Hakuguswa, hakukamatwa, hakuwekwa chini ya ulinzi. Sina hakika ni kwa
sababu gani, lakini yanaweza kuthibitisha kwamba ilikuwa kwa sababu ya kuwa
"mwenzetu'.
Sababu hiyo inatumiwa sana na viongozi wasiokuwa na maono ama wito wa
kuutumikia umma. Viongozi wanaoamini kwamba kwa vile wana dola, majeshi,
silaha zikiwemo bastola, hakuna wa kuwagusa!
Wanafanya wanavyopenda, wanatishia umma pasipo kujali athari zake,
wanajenga 'picha mbaya' kwa kizazi cha sasa na baadaye.hawaguswi!
Itakuwaje akitokea 'mwenzetu' mwingine ambaye kwa asili ni jambazi ama
mhusika wa vitendo viovu, akavaa kwa jinsi ambavyo Rage alivaa kule Igunga,
akiwa na bastola atakayoitumia kukidhi nia ovu dhidi ya raia wasiokuwa na
hatia, itakuwaje?
Kuna msemo unaotumika sana, 'kama baba-kama mwana'. Msemo huo una tafsiri
nyingi ikiwemo ya kuanisha matendo, hulka na tabia zinazofanana, zikiwana
matokeo ya kurithi.
Rage akiwa kiongozi mwenye hadhi ya kidiplomasia inayotokana na ubunge wake
kupitia CCM-chama tawala, aliwasilisha ujumbe gani kwa jumuiya ya wanachama
wenzake wakiwemo majambazi waliojificha humo ili kulinda uovu wao?
Rage anaweza kujitetea kwamba alikuwa analinda! Haiwezekani, haikubaliki
ikawa hivyo. Atakuwa amepotosha kwa maana mkutanoni pale, hapakuwa na ishara
zozote za uvunjivu wa amani ama kitisho kwa mfungwa huyo wa zamani.
Chama, watanzania na jumuiya za kimataifa zinaamini kwamba Tanzania ni
mfano wa kisiwa cha amani na utulivu. Sifa ambazo zimechangia kushamirisha
umoja wa kitaifa na ongezeko la watalii kutoka nje.
Inapofikia Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, tena kupitia chama
tawala anajitokeza hadharani na bastola kiunoni, kuna uhalali wa kuamini
uwepo wa amani na utulivu vingali hai hapa nchini?
Kituko alichokifanya Rage kinastahili kuchukuliwa kwa uzito usiohusisha
misingi ya kulindana, bali kutekeleza kwa kadri ya sheria, kanuni na
taratibu ili umma ubaki kuwa salama na amani.
Rage anaweza kulindwa kwa sababu zozote za kisiasa, lakini kama hali hiyo
itatokea, ni dhahiri kwamba 'walinzi' wake watakuwa wamekubali kuuangamiza
umma, kuliathiri taifa.
Kwa kadri ulivyo msemo wa 'kama baba-kama mwana', wapo watakaofuata nyendo
hizo kwa kuamini kwamba, watalindwa kwa misingi ya 'uenzetu'.
Umma ubasubiri. Usiporidhishwa na hatua zitakazochukuliwa dhidi ya Rage,
umma utachukua hatua dhidi ya waliostahili kuchukua hatua stahiki kwa lengo
la kukomesha vituko vya aina hiyo.
Mashaka Mgeta ni Mwandishi wa Habari za Siasa wa NIPASHE ambaye kwa sasa
yupo nchini Kenya. Anapatikana kwenye simu namba +255 754 691540
<tel:%2B255%20754%20691540> , +254 702 115 303
<tel:%2B254%20702%20115%20303> ama barua pepe: mgeta2000@yahoo.com
<mailto:mgeta2000@yahoo.com> .
 
Source: Nipashe; link (http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=33860)

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com <http://www.mwanabidii.com>
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
<http://www.kazibongo.blogspot.com>
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
<http://www.patahabari.blogspot.com>

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com
<mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com>  Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment