Tuesday 14 August 2012

RE: [wanabidii] WATANZANIA WASUSIA MKUTANO WA CHADEMA LONDON

Loh! Dada Rehema na dada Rukia Kilemile, nadhani Watanzania wenzetu hao wa London walikuwa wamechapa maji haswa. Mpaka wanafikiri eti kuwa London maana yake wana uwezo wa kuchambua hoja kuliko watu walioko Bongo? Eti "jamaa wanabwabwaja tu hawawezi hata kujenga hoja. Wanafikiri hapa ni walipotoka. Ovyo!". Yaani hawajui kwamba uwezo wa kuelewa na kuchambua hoja hautegemei mtu yuko wapi. Hao kweli ni watu wa baa na siyo kwamba walipuuza mkutano (kama kweli uilkuwapo) bali wao ndo wanapaswa kupuuzwa. Halafu sentensi ya ambayo ni judgment kwa CHADEMA na sifa kwa CCM mwisho eti "ikitarajia kufuata nyayo za CCM UK itabidi CHADEMA waombe miujiza ya aina yake kupata wanachama na si washabiki tu... CCM ilifanikiwa kufungua mashina katika miji/majiji 10 hapa UK" ni ya kwako (Rehema), ni mwandishi (Rukia) ama ni ya wale jamaa wa baa? Ona ilivyokaa kishabiki: CHADEMA waombe miujiza ya aina yake; CCM walifanikiwa kufungua matawi katika majiji 10! Tunashukuru kutujuza kwamba uko UK. Tupe nyingine za huko!
 

Date: Tue, 14 Aug 2012 13:19:26 +0100
Subject: Re: [wanabidii] WATANZANIA WASUSIA MKUTANO WA CHADEMA LONDON
From: kiganyi@gmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com

Hii dhadti ya " mchambuzi" wa masuala ya jinsia niliiona mara ya kwanza kwa dada SubiNukta kule wavuti, na kwa kweli ni mtu wa kupuuzwa kabisa! Kwanza imeandikwa kishabiki sana! CCM mwaka huu watachanganyikiwa!

Nadhani tunakoelekea ndiko wengi tunapenda tuwe na vyama vyenye nguvu ana si hili "Dudu" CCM liendelea kudhani lina hati miliki ya kuongoza watanzania!

Magiri.
www.wotepamoja.com

Tarehe 14 Agosti 2012 12:31 alasiri, Azaveli Lwaitama <kerezesia_mukalugaisa@hotmail.com> aliandika:
Rehema Kikwete
Asante kwa kutupa nafasi ya kufanya uchambuzi wa lugaha zilizosheheni propaganda za CCM- Mamboleo. Mchambuzi wa lugha kwa kigezo cha utamaduni wa kiuwanazuoni( scholarly traditions) unaojulikana kama " crtical discourse analysis"  ataanzia kwenye kudadisi kwa nini unahitimisha taarifa yako kwa kusema "Habari hii imeandikwa na Rukia Kilemile. Mwandishi huyu ni  mchambuzi wa sera za jinsia na uchumi hapa United  Kingdom. Mwandishi si mwana chama wa chama chochote cha siasa." ? Kwa nini mwandishi unaye mnukuu unatanguliza  kusema eti "si mwana chama wa chama chochote cha siasa."? Je alikutuma useme hivyo au wewe tu ulijituma? Pili, taarifa ya hiyo ya mwandishi wako inabainisha kweupe kuwa "Katika mahudhurio hayo machache,idadi kubwa walikua ni wanaCCM  waliohudhuria kwa makusudi na wengine kuchangia kwenye mkutano huo. Baada ya mkutano vicheko vya kebehi vilisikika na kuambatana na kauli kama ".jamaa wanabwabwaja tu hawawezi hata kujenga hoja.wanafikiri hapa ni walipotoka..ovyoo."
 
Sasa  huyo mwandishi wako anatujulisha lipi tusilotarajia kutoka kwa watu wa aina hiyo?  Hivi mwandishi wako hajui kuwa Watanzania  wa kawaida  walio wengi ambao wanaweza wakawa  hapo London  watakuwa ni  wanafunzi walio masomoni na si wengi wangekuwa na uwezo wakuja kwenye huo mkutano kwenye Bar hiyo moja London . Tena wanafunzi  wenyewe waje kwenye mkutano  huo huku wakijua kuwa waandaaji wengi wao ni wana CCM wenye lengo la kukiumbua chama cha Chadema? Come on give us a break hatupo wote mbumbumbu kiasi hicho kuhusu mji wa London jamani!!!  Hata huyo huyo mwandishi  anakiri kuwa  mahudhurio ya mkutano huo yalikuwa  "   machache,idadi kubwa walikua ni wanaCCM  waliohudhuria kwa makusudi na wengine kuchangia kwenye mkutano huo"? Aaha!!!
 
Sasa habari ya eti  "Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimepata aibu ya mwaka hapa jijini London baada ya Watanzania kususa kuhudhuria mkutano wao waliofanya katika Bar imiliikiwayo na Wakenya ya The Thatched House" ina mashiko gani  kimantika ?  Ni mtu gani atapoteza muda mwingi kuipa umuhimu habari kama hiyo ya yenye harufu ya propaganda  za CCM tulizozizoea Bungeni Dodoma za watu wenye kupenda kutamka mananeo  ".jamaa wanabwabwaja tu hawawezi hata kujenga hoja.wanafikiri hapa ni walipotoka..ovyoo." ?
 
Nani hasiye jua kuwa  bila shaka  jiji la London litakuwa nao Watanzania kiasi chake ambao kuwepo kwao London kunatokana na  ufadhili wa serikali iliyo madarakani  ya CCM kama vile kuwa watumishi wa serikali ya Tanzania  kwenye ubalozi  au  wawakilishi wa makampuni ya Uingereza au ya Tanzania  yenye ushirika wa karibu na serikali ya chama tawala cha CCM au matajiri Wakitanzania ambao wengi wao wako karibu na chama tawala cha CCM?...Ndugu yangu Rehema Kikwete, Watanzania wa kileo si wa zamani wa enzi za Zi dumu Fikra za Mwenyekiti wa CCM!!! Wamebadirika na wanabadirika kwa kasi, ari  na nguvu zaidi kila kukicha!!!
 
 Hayo ya eti Chadema ni washirika wa chama cha Conservative cha Uingereza eti chenye kukumbatia uteteza wa haki za kibinadamu za mashoga, ilo nalo ni kichekesho maana serikali ya CCM ya enzi hizi pia  hiko karibu kweli kweli na serikali ya Uingereza ya chama cha  mseto cha Conservative na Lib-Lab . Pia  serikali ya CCM ipo karibu  kweli kweli na serikali ya Rais Obama wa Marekani ambayo nayo inakumbatia utetezi wa haki za binadamu za mashoga. Zaidi ya yote   serikali ya CCM ya kileo  ilikuwa na ipo bado pamoj karibu na Rais mtaafu wa Marekani  George Bush ambaye ni wa chama cha Republican cha Marekani ambacho ni chama  rafiki wa  karibu sana  wa chama cha Conservative cha Uingereza.
 
Hizi propaganda za kutuambia eti Chadema kiko karibu na chama  hiki au kile Uingereza au Marekani hazina mashiko kiitikadi kwa kungalia itikadi za vyama vyetu vya siasa nchini Tanzania. Vyama vyote vya kisiasa  vilivyo na madaraka au vinavyotarajiwa kuwa na madaraka Tanzania au Uingereza au Marekani ni vyama venye kufuata itikadi ileile ya ubepari wa uliberali mamboleo. Watanzania wanachotaka nikuondoa CCM madarakani ili tuwe kama Uingereza na Marekani mahali ambapo vyama hivi vinatawala kwa kupokezana vijiti kila baada ya mika michache ili visije kujiamini mno na kufanya wananchi watumwa wa vyama hivi kama iliyo Tanzania iliyokidhiri kwa  ukiritimba wa chama kimoja cha  cCCM ambacho nacho  ni mtetezi wa ubepari wa uliberali mambo leo kama kilivyo Chadema. Kutarajia kuwazuzua na kuwazuga Watanzania kwa kuwafanya wadhani  kuwa CCM ni chama cha kimapinduzi na kizalendo  zaidi kuliko Chadema ni kucheza karata ambayo itafanikiwa kwa muda kiasi lakini si  kwa wakati wote na kwa watu wote.    Asante hata hivyo kwa kutupa data za kufanyia majaribio ya uchambuzi wa propaganda hizi za CCM.
Mwl. Lwaitama- CCM-Mfu


Date: Tue, 14 Aug 2012 02:48:17 -0700
From: fredrick197958@yahoo.com

Subject: Re: [wanabidii] WATANZANIA WASUSIA MKUTANO WA CHADEMA LONDON
To: wanabidii@googlegroups.com



Hao wanaoenda nje ya nchi (CHADEMA&CCM)
wanatafuta shekels kufanikisha agenda ya kuwafikia wananchi. Kwa hiyo tusishangae pale tunapoyaona haya.

Kimsingi hawa jamaa wana haki ya kuchangia maadamu wanajua kuwa chama kinachochangiwa kinaenda vijijini 
kupeleka itikadi zao kwa wanachi


From: Gwa Ntegeye <gwantegeye@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, August 14, 2012 12:02 PM
Subject: Re: [wanabidii] WATANZANIA WASUSIA MKUTANO WA CHADEMA LONDON

Ila hata mimi sielewi umuhimu wa matawi nchi za nje maana hata ikiwa
nchi nzima  ya nje inaunga mkono lakini sioni kama hawana mchango
katika upigaji kura haina maana yoyote.

anyway kama kuna mtu ana muono mzuri kuhusu huo uhusiano wa jamii za
nje atuambie.

On 8/14/12, Laurean Rugambwa B. <rugambwa@hotmail.com> wrote:
> Rehema,
> Asante kwa hii taarifa ulotuwekea hapa.
>
> Mimi sijawahi kuelewa kwanini watu wahangaishwe na watu wasio piga kura.
> Hayo matawi wanayofungua Chadema au CCM London, Washington ni public
> relations tu, haiongezi kura.
>
> Wapiga kura wako Kishapu, Meatu, Karagwe, Bahi nk. Hao ndo wakikuzomea
> unapata taabu kidogo.
>
> Kazi njema,
> LR
> Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
>
> -----Original Message-----
> From: Rehema Kikwete <rehemaki@gmail.com>
> Date: Tue, 14 Aug 2012 08:40:59
> To: <wanabidii@googlegroups.com>
> Subject: [wanabidii] WATANZANIA WASUSIA MKUTANO WA CHADEMA LONDON
>
>
> Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimepata aibu ya mwaka hapa
>  jijini London baada ya Watanzania kususa kuhudhuria mkutano wao
>  waliofanya katika Bar imilikiwayo na Wakenya ya The Thatched House.
>
>  Sababu nyingi zilizotajwa ni pamoja na urafiki mkubwa na kukubali kila
>  sera ya Chama Tawala cha Uingereza cha Conservative ambacho
>  kinachukiwa na Waingereza wenyewe kwa sera za kulazimisha zilizoleta
>  hali mbaya ya maisha na umaskini nchini hapa.
>
>  Aidha ni Chama kilichoilazimisha serikali kuwabagua na kuwafukuza
>  Watanzania wengi waliokuwa wakiishi Uingereza na kuwarudisha Tanzania
>  kwa Aibu kubwa huku wakiacha mali zao nyuma.
>
>  Maandalizi ya mkutano wa Chadema pia yaliwachefua Watanzania wengi na
>  kukataa kushiriki kwa kuwa yalichangiwa na kufanywa na baadhi ya watu
>  wenye kudhaniwa kwa muda mrefu kuhusudu tabia za USHOGA na USAGAJI
>  wakati ambapo Watanzania wengi hawajapona kidonda kilichotibiwa kwa
>  mabavu na serikali ya CCM wakati iliposhinikizwa kukumbatia utamaduni
>  wa USHOGA na serikali ya Conservative au isahau misaada ya maendeleo
>  ya kitaifa. Chadema katu haikupinga shinikizo hili la rafiki zao
>  Conservative.
>
>  Aidha waandaaji wakuu wa mkutano huo iliwajumuisha wakurugenzi wakuu
>  wa SERENGETI FREIGHT, kampuni inayojishughulisha na usafirishaji wa
>  mizigo kwenda Tanzania na kwingineko. Kampuni ya Serengeti imekuwa
>  ikilaumiwa na kushutumiwa sana siku hizi kwa kutokusema ukweli kwa
>  Watanzania kuhusu muda, gharama za ghafla na uhakika wa usafirishaji
>  wa mizigo ya Watanzania ambao wengi wameishia kulipa gharama kubwa za
>  ziada, ucheleweshwaji au kuamua kuacha mizigo dhidi ya muda
>  uliokubalika. Kuhusika kwa Wakurugenzi hawa kuliongeza uchungu kwenye
>  kidonda kibichi.
>
>  Baadhi ya Watanzania waliokuwa wakijiburudisha ndani ya Bar hiyo na
>  kuangalia mashindano ya Olyimpic walimrushia Bw. Lema maswali ya
>  kebehi na kumzomea pia na kusema.. "Gwanda linanuka RUSHWA meku"..huku
>  wengine wakitoa kadi zao za CCM na kunyanyua juu.
>
>  Katika mahudhurio hayo machache,idadi kubwa walikua ni wanaCCM
>  waliohudhuria kwa makusudi na wengine kuchangia kwenye mkutano huo.
>  Baada ya mkutano vicheko vya kebehi vilisikika na kuambatana na kauli
>  kama ".jamaa wanabwabwaja tu hawawezi hata kujenga hoja.wanafikiri
>  hapa ni walipotoka..ovyoo."
>
>  Ikitarajia kufuata nyayo za CCM UK itabidi Chadema waombe miujiza ya
>  aina yake kupata wachama na si washabiki tu katika maeneo tofauti ya
>  UK ili itoke kwenye sura ya Kijikundi. CCM UK ilifanikiwa kufungua
>  mashina katika miji/majiji kumi hapa UK.
>
>  Habari hii imeandikwa na Rukia Kilemile
>   Mwandishi huyu ni  mchambuzi wa sera za jinsia na uchumi hapa United
>  Kingdom.
>
>  Mwandishi si mwana chama wa chama chochote cha siasa.
>
>  --
>  Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com <http://www.mwanabidii.com>
>  Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> <http://www.kazibongo.blogspot.com>
>  Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
> <http://www.patahabari.blogspot.com>
>
>  Kujiondoa Tuma Email kwenda
>  wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
>  Disclaimer:
>  Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.





--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment