Wednesday 8 August 2012

Re: [wanabidii] Vijana wa umoja wa Kitaifa:Tamko la Indhari

"Anayeitwa baba wa taifa"? Ina maana kuna watu bado wana mashaka na Nyerere kuwa baba wa taifa na bado ni CCM? Anyway, Kama ni mambo ya chama msimhangaishe Shein, Mwenyekiti wa CCM ni Kikwete na Makamu Makamu wake ni Karume kwa upande Zanzanzibar msimhangaishe bure Dk. Shein.
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

-----Original Message-----
From: Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Wed, 8 Aug 2012 06:09:18
To: Wanabidii<wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: [wanabidii] Vijana wa umoja wa Kitaifa:Tamko la Indhari

Tamko la Indhari!

Na, Vijana wa Umoja wa Kitaifa Zanzibar.

Vijana wa Umoja wa Kitaifa Zanzibar tumeshtushwa sana kufuatia
matamshi/kauli na misimamo ya baadhi ya viongozi na wafuasi wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) yenye shabaha ya kutumia vitisho na mabavu katika
kuzizima hoja za baadhi ya viongozi, wanachama na wafuasi wake wenye
mawazo mbadala/tofauti. Hapa tunawakusudia viongozi wa CCM wa Wilaya
ya Mjini na Afisi Kuu, Kisiwandui pamoja na baadhi ya viongozi
wastaafu wa CCM ambao wanawatisha na kuwashinikiza viongozi katika
chama chao hususan Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Wananchi wa
Zanzibar waliochaguliwa na wananchi wa Zanzibar wakiwa na wajibu wa
kuwatetea wananchi wa Zanzibar kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na ile
ya Jamhuri ya Muungano wakilindwa na kinga kwa mujibu na kanuni za
Baraza na Sheria za nchi.

Hao wenye kutoa vitisho na kuweka shinikizo wajue kuwa vitendo vyao
hivyo ni kupora uhuru wa wananchi na kuondosha uhalali wa zoezi zima
la marekebisho ya katiba. Vitendo vyao hivyo ni sawa na kuwapangia
wananchi nini cha kusema na vitendo kama hivyo ni uvunjifu wa katiba
na sharia za nchi na ni uporaji wa haki za msingi kabisa za wananchi
wote na ni fedheha na aibu kubwa kwa CCM. Ifahamike wazi kuwa
kupatikana kwa aina ya mfumo wa muungano tunaoutaka utapatikana pale
tu ambapo wananchi wote bila ya kujali vyama vyao watakuwa na uhuru
usio na masharti ili waweze kutoa maoni yao vinginevyo zoezi hili lote
litapoteza maana na uhalali wake na hivyo kuwa batili.

Katika hali kama hii tunamuomba Mheshimiwa Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein waingilie kati ili kulinda
uhuru wa wanachama na sisi wananchi kwa ujumla wetu. Halikadhalika
tunamuomba Mwenyekiti wa Tume ya Pamoja ya Marekebisho ya Katiba,
Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba pamoja na Mheshimiwa Pandu Ameir
Kificho Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kutoa tamko juu ya
kauli hizi za kushtusha za baadhi ya viongozi hawa wa CCM ili wananchi
turidhike juu ya uhuru wetu na uhalali wetu wa kutoa maoni bila ya
shinikizo la aina yoyote kutoka chama chochote.

Kauli na misimamo hiyo inaonekana sio tu kwenda kinyume na Azimio la
Haki za Binaadamu zinazodhamini uhuru na uwezo wa kila raia kuwa na
mawazo na maamuzi tofauti. Misimamo na matamshi hayo yanapingana hata
na kauli ya Rais Jakaya Kikwete, Rais Ali Mohammed Shein na Jaji
Warioba ambao kwa pamoja walisema wazi kuwa wananchi wako huru kuwa na
maoni tofauti juu ya mchakato wa katiba na wawe huru katika kuyatoa
mawazo yao. Aidha, Rais Kikwete alisema na tunamnukuu: "Kwa upande wa
mchakato wa kupata katiba mpya, nawasihi Watanzania tujiandae kwa
maoni ya kutoa. Tutofautiane bila kupigana". Hata anayeitwa Baba wa
Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kusema katika hotuba
aliyoitoa kwenye mkutano wa Uganda People’s Congress (UPC), tarehe 7
Juni, 1968: "Chama kina uwezo kuiambia Serikali nini matilaba ya watu,
na kwamba ni muhimu kuweko wanachama ndani ya chama wanaoweza
kuhakikisha kwamba Serikali na watu wanashirikiana kutekeleza matilaba
ya watu".

Tunatanabahisha kuwa tutofautiane katika fikra bila ya kubezana,
kutishana wala kupigana. Aidha, tunatanabahisha kuwa kauli kama hizi
zilizoanza kutolewa zinazobeba agenda ya vitisho na kuiviza demokrasia
hazitavumiliwa. Ni busara kusoma alama za nyakati.

Nchi hizi mbili za Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
zimetokana na asili ya utawala wa chama kimoja cha siasa baada ya
mapinduzi ya Zanzibar na uhuru wa Tanganyika, na hatimaye kuwepo kwa
chama kimoja tu kwa nchi zote mbili. Siasa ya vyama vingi imeanza
katika uchaguzi mkuu wa 1995, kiasi cha miaka kumi na saba iliyopita,
tofauti na utawala wa chama kimoja wa miaka zaidi ya thelathini.

Kwa miaka hiyo thelathini na kitu, hakukuwa na tafauti kubwa baina ya
Chama na Serikali. Kwa mfano, Mkuu wa Mkoa alikuwa Katibu wa Mkoa wa
Chama, viongozi wa Chama walikuwa na hadhi ya viongozi wa Serikali
kama vile kusafiria pasi za kibalozi. Katika kila Wizara, Idara na
Mashirika, kulikuwa na ofisi za Chama cha Mapinduzi, na Mwenyekiti
wake, na bendera ya chama ndio ilokuwa ikipepea. Hii inaonesha wazi
tutokapo na jinsi mfumo wa fikra za watu (mindsets) ulivyojengeka.

Kutokana na hali hii sera za Chama na Serikali hazikuweza kuwa na
tafauti yoyote. Sera zote za chama ndio zilikuwa sera za serikali. Kwa
maana hiyo sera ya kuwa na Muungano wa Serikali mbili iliyopo ndani ya
Katiba ya Muungano ndiyo ya Chama tawala cha wakati huo na ndio maana
bado kuna baadhi ya viongozi (wahafidhina) wanaolalamika leo juu ya
haya mabadiliko tunayoyatarajia, na ndio maana vilevile tunashuhudia
wakikaripia na hata kupinga juu ya mabadiliko ya sera hizo.

Wakati umebadilika na nchi zetu zina vyama vingi vya siasa, vyenye
sera zao na wanachama wao ambao wote ni wananchi wenye haki sawa juu
ya maamuzi mazito ya nchi kama katiba zinavyoeleza. Zaidi ya Chama
tawala, hakuna hata chama kimoja chenye sera yake ya muundo wa nchi,
kwa sababu vinafahamu kwamba sera hii haiwezi kuwa ukiritimba wa chama
kimoja, bali ni ridhaa ya wananchi wote, hata wale ambao siyo
wanachama au wafuasi wa chama chochote cha siasa.

Kwa hivyo huu utaratibu wa kukusanya na kuratibu maoni ya wananchi ni
wa kupongezwa. Hata hivyo, indhari ichukuliwe ya kuhakikisha kwamba
ukweli na uadilifu unatawala katika zoezi hili, na kwamba kila
mwananchi apewe fursa ya kutoa maoni huru bila ya shinikizo la kuimba
nyimbo ya sera za Chama chake. Hii itakuwa kinyume kabisa na
wanavyofanya baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) kutaka kuwatisha na kuwanyanyapaa baadhi ya wanachama wake wenye
fikra tofauti zinazokwenda kwa mujibu wa hali ya siasa zilivyo hivi
leo. Huu ni wakati wa wananchi kupingana bila ya kupigana na hii ndio
demokrasia itakayotuletea amani na usalama. Hapa elimu ya uraia ndipo
inapohitajika.

Tunasisitiza kuwa matokeo ya zoezi hili yaheshimiwe na wote. Tunajua
kwamba Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni kiongozi
mwandamizi wa Chama chake. Tunamuomba kwamba asiyumbishwe na sera za
Chama chake katika zoezi hili. Tume ni suala linalojitegemea na
maslahi ya nchi na watu wake ni makubwa kuliko sera za vyama. Huu ni
wakati wa kusonga mbele si wakati tena wa kutazama nyuma. Wakati na
mawimbi hayamsubiri mtu.

Tufanye kazi katika maadili ya shabaha yanayoheshimu mawazo, maoni na
maamuzi ya wananchi. Tuna wajibu wa kusimama juu ya ukweli kama
tunavyouona bila ya kujali misingi na mirengo ya vyama. Sote kwa
ujumla wetu kuanzia vyama, Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Serikali
zote mbili ni watumishi wa watu. Na watumishi hawana haki wala mamlaka
wala nguvu zinazowazidi mabwana zao ambao ni wananchi kama Katiba zote
mbili zinavyolidhamini hilo. Tunawajibika katika hili kutoa huduma ya
kizalendo na kwa sababu hiyo itakuwa huduma ya kweli na isiyosimamia
misingi ya vyama.

Sisi Vijana wa Umoja wa Kitaifa ni waumini wenye kuheshimu uhuru wa
mawazo ya kila mwananchi; lakini pia tunabeba kauli mbiu (motto)
isemayo: "Maslahi ya wananchi ni makubwa zaidi kuliko yale ya vyama
vya siasa." Historia itakuja kutuhukumu.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment