Tatizo ni je, utasaidia au utakuwa mwanzo wa kufumuka kwa utawala wenye kuleta haki na kuendeleza amani. Utaratibu wa uanaharakati bungeni ni nadharia potofu tu ya akina Rosa na Lennin lakini haitumiki kivitendo na wala haijatumika popote pale; ni hypothetical zaidi na hivyo sisi tunataka kuijaribu! Lakini kujaribia kitu kama hiki kwenye taifa ni hatari sana maana madhara ya failure yake hatuifahamu!
Mafundisho ya falsafa ya dola (Statehood), yanatukumbusha kuwa katika taifa lolote vyombo vikuu vya dola ni:
Jeshi, Polisi, Mahakama, Magereza, na Kodi (bunge na serikali ni walezi wa kulinda dola). Vyombo nilivyotaja awali ni msingi ya dola lolote na hufanya kazi kwa kuogopana na kuheshimiana (sio kulindana). Polisi wanaogopa na kuheshimu Jeshi, vile vile mahakama na magereza wanaheshimiana na kuogopana. Utekelevu wa nguvu zao wote unalindwa na chombo kingine. Kama hawaheshimiani na kuogopana leo itaona polisi hawatakuheshimu jeshi na Magereza hawataheshimu amri ya mahakama na pia polisi hawatajali mahakama na kadhalika!
Bunge na serikali navyo vinaheshimiana na kuogopana na katika kuwa hivyo ndipo utekelezaji ya matakwa ya mmoja yanaheshimiwa na mwingine! Huwezi kusema bunge halitegemei serikali na serikali nayo hailitegemei bunge. Lazima waheshimiane na kuogopana ndipo tunapata utawala wa sheria na utaratibu. Kuumbuana na kudharauliana kati yao kutaondosha kutegemeana na hivyo kukosa nguvu za kuwa Dola.
Hilo ndio tatizo ninalojaribu kulieleza hapa ingawa kuna ushabiki unatawala mawazo au fikra za baadhi yetu! Wanashabikia lolote linallosemwa na "X" na wanabeza na kupinga lolote la "Y". Kwa msingi huu uwezo wa kuchambua mambo unaghubikwa na ushabiki wa "Y" au "X". Hili nalo tatizo hapa!
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.
From: Lutgard Kagaruki <lutgardk@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Mon, 20 Aug 2012 02:59:35 -0700 (PDT)
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
Tony, kama unaharakati wa kisiasa utatusaidia kurekebisha mambo yanayoiyumbisha Tanzania kama ilivyo sasa, basi huo uanaharakati unafaa sana. LKK
From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, August 20, 2012 11:19 AM
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
TL,
Sijui uelewa wangu na wako kwenye hili kama wazidiana kiasi gani, wewe mwanasheria inawezekana unao utaalamu huu (!) wa kuweza kubashiri uelewa jadidi wa binadamu mwenzio katika kipindi kifupi!
Kwanza maandiko ya Rosa na Lennin nimeyasoma na yamepata critique za kila aina na wanataaluma wengi na mahiri hapa duniani. Na they're no longer upheld na kubeba umahiri (authority) wa siasa za kimamboleo!
Lakini itikadi yako ambayo naiona toka matendo na hotuba zako, imelalia kuhusudu ujamaa wa akina Marx na waliofuata itikadi hiyo (Wachina na Wakyuba), sioni ajabu unapokumbatia maandiko hayo kwenye karne ya leo. Ukumbuke theory zao zilidumu miaka 70 tu na zimebadilishwa sana hata waliozishikilia hadi leo.
Activism haitumiki ndani ya mabunge bali inatumika kwenye "deliberative democracies practices" mara nyingi activism, social justice movements, structural inequalities na deliberative democracy hutumiwa vizuri na institutions za kisiasa nje ya Bunge. Bunge ni structured state organ na ni taasisi inayofuata prescribed procedures, rules na kuongozwa na katiba. Tofauti na activism ya jambo lolote huwa haielekei hata siku moja kufuata utaratibu ingawa kinadharia, wanashikilia kufanya kuwa na taratibu katika kudai wanachokitaka!
Katika karne hii baada ya liberal democracies kuingia kwa kasi tumeshuhudia uanaharakati kuingia kwenye bunge; mfano vyama vya kijani (green parties), ambao ni wanaharakati wa mazingira. Hata hao waliingia bungeni na hawajafaulu sana na walikuwa na lengo maalum.
Staili ya activism hii kwenye democracy mara nyingi tangu mwanzo wa karne hii tunaishuhudia kwenye vyombo vya habari (democratic media activism), ambayo inakubalika na jamii kwavile ni kati ya "social movement theories" za akina Melucci, Cohen+Arato, Habermas, na Fraser.
Uanaharakati kama tunaouona hapa Tz na ambao umekuwepo nchi nyingine (na sio kwenye mabunge), ambao wewe unatuaminisha ni sawa na wakudai haki na utawala bora, mara nyingi hufadhiliwa na vikundi kutoka nje ya nchi husika na huwa si endelevu kwavile baada ya kubadilisha utawala uliopo kwenye nchi husika, huishia hapo na makundi mengine ya kianaharakati huibuka kupinga status-quo! Ufadhili huo hufanywa na vikundi vyenye maslahi ya kiuchumi au with strategic interest kwa taifa husika!
Kulingana na historia, uanaharakati wa aina hii unatumika nje ya taasisi za kidola kama pressure groups ukisaidiwa sana na tasnia za habari.
Unaweza kusoma tofauti hizi kwenye kitabu cha Fishkin & Laslett cha 2008.
Swali dogo la kujiuliza ni kwanini theories za akina Lennin leo hazitawali tena dunia na zimebaki rejea za wanafunzi wa political history na uchumi wa kijamii? Hazina mshiko ena kwenye neo-political philosophy na hata uchumi jamii mamboleo.
Tunachangia hapa kupanuana uelewa tu na sio kudhalilishana au kubezana kama mwelekeo ninaouona kushamiri kwako. Utusamehe bure kama tunakuudhi Mheshimiwa.
Jambo ambalo nalishangaa kidogo kwenye hoja yako hapa ni uwezo gani ulio nao wa kudhani mtu anayekupinga kuwa na uelewa mdogo kuhusu jambo unaloelezea? Unajuaje uelewa wako ni wa juu kuliko wengine (authoritative)? Hiyo nayo ni dosari, kama mwanasiasa inabidi uibadilishe, ni sawa kama ungekuwa upo mahakamani ili kushinda kesi.
Ni tafakuri yangu tu!
From: deogratius temba <deojkt@yahoo.com>;
To: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
Sent: Fri, Aug 17, 2012 6:35:45 AM
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
-- Sijui uelewa wangu na wako kwenye hili kama wazidiana kiasi gani, wewe mwanasheria inawezekana unao utaalamu huu (!) wa kuweza kubashiri uelewa jadidi wa binadamu mwenzio katika kipindi kifupi!

From: Tundu Lissu <lissubulali@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 19 Aug 2012 23:57:49 -0700 (PDT)
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
Tony, Nilichokisema bungeni kinaitwa na Kanuni za Kudumu za Bunge 'Maoni ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.' Kwa sababu hiyo, hayo ni maoni yangu. Lakini kwa kuwa yametolewa in my official capacity kama Msemaji wa Kambi, ni maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Tumejenga utamaduni mzuri katika Kambi yetu ambapo Maoni ya Msemaji wa Kambi hujadiliwa kwanza kabla ya kuwasilishwa Bungeni. Of course, kama Msemaji wa Kambi amefanya kazi yake sawa sawa, what's eventually presented in Parliament will bear a very strong imprint, if not style, of the author. Mimi huandika hotuba zangu mwenyewe, nafanya research mwenyewe na kwa hiyo whatever you see presented in the House bears my unmistakeable style and ideological bent hata kama kimejadiliwa na kupitishwa kwenye Kambi. Kuhusu kuchanganya uanaharakati na siasa, n.k., nadhani uelewa wako wa historia ya Western democracies ni too limited kuweza kutusaidia kwenye mjadala huu. Kwa vile unaelekea kutokujua nitakuelekeza kwa wanaharakati wakubwa wa siasa za kimapinduzi wa karne iliyopita, Vladimir Lenin na Rosa Luxemburg ambao, licha ya ku-dedicate maisha yao yote kwenye harakati za kuupindua mfumo wa demokrasia ya kiliberali, waliandika sana juu ya haja, na namna, ya kutumia uwanja wa siasa za kibunge kwa malengo ya kimapinduzi. Rosa Luxemburg wrote a beautiful pamphlet titled 'Reform or Revolution'. Nakushauri ukitafute ukisome. Lenin, perhaps the greatest revolutionary mind since Marx, aliandika kijitabu kiitwacho 'Left Wing Communism or an Infantile Disorder?' ambapo alizungumzia sana umuhimu wa parliamentary politics. Kwa hiyo kaka, unachokisema kuhusu kutokupeleka uanaharakati Bungeni kinatoka zaidi kwenye kichwa chako na sio historia halisi ya demokrasia za Magharibi. Tundu |
From: deogratius temba <deojkt@yahoo.com>;
To: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
Sent: Fri, Aug 17, 2012 6:35:45 AM
Utamaduni wa kuendelea kulindana na kupena anafasi za kazi kwa wanaojulikana au waliotufanyia mambo fulani kama sehemu ya kulipana fadhila unaendelea. Taifa hili halitakaa libadilike kwa kuendelea kuwaajiri watu vihiyo, wasio na uwezo huku wenye uwezo wakikimbilia nchi za nje na wengine kujifanyia shughuli zao binafsi. kuna kundi la watanzania weledi, waadilifu na wenye uwezo mkubwa wa kubadilisha taifa hili lakini hawapewi nafasi kwasbabu tunataka watakaotulinda. Suala la majaji ni la kusitikisha, Rais anapoingia madarakani anataka kudfanya kazi na safu ya watu atakao watumikisha bila kuhojiwa, wasaidizi wa 'ndiyo mzee' ambao watafanya wanachoamabiwa bila kuhoji au kukataa, ambao wataamriwa kuvunja sheria, katiba au haki za binadamu na kukubali. hili linahitaji mabadiliko makubwa na ni Kuwa na katiba mpya nzuri itakayompokonya Rais wa Tanzania madaraka ya kuteua kila mtendaji wa serikali. Vinajana wanaohitimu vyuo vikuu sasa wataenda wapi? kama wazee wanateuliwa hata baada ya kupoteza uwezo wa kuona? Hivi tujiulize Tume ya utumishi wa mhakama inafanya nini? kazi yke ni nini? macommisner wa Tume nao wanakula mishara na posho bila kufanya kazi kumbe rais anateua majaji na watendaji wakuu wa mhakama peke take. Tubadilike, na tujitokeze kutoa maoni kwenye mchakato wa katiba mpya kama haturidhiki na hili. -------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------- "By faithfulness we are collected and wound up into unity within ourselves, whereas we had been scattered abroad in multiplicity" Saint Augustine (354-430) Theologian
|
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
0 comments:
Post a Comment