Monday 20 August 2012

Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

TL,

Sijui uelewa wangu na wako kwenye hili kama wazidiana kiasi gani, wewe mwanasheria inawezekana unao utaalamu huu (!) wa kuweza kubashiri uelewa jadidi wa binadamu mwenzio katika kipindi kifupi!

Kwanza maandiko ya Rosa na Lennin nimeyasoma na yamepata critique za kila aina na wanataaluma wengi na mahiri hapa duniani. Na they're no longer upheld na kubeba umahiri (authority) wa siasa za kimamboleo!

Lakini itikadi yako ambayo naiona toka matendo na hotuba zako, imelalia kuhusudu ujamaa wa akina Marx na waliofuata itikadi hiyo (Wachina na Wakyuba), sioni ajabu unapokumbatia maandiko hayo kwenye karne ya leo. Ukumbuke theory zao zilidumu miaka 70 tu na zimebadilishwa sana hata waliozishikilia hadi leo.

Activism haitumiki ndani ya mabunge bali inatumika kwenye "deliberative democracies practices" mara nyingi activism, social justice movements, structural inequalities na deliberative democracy hutumiwa vizuri na institutions za kisiasa nje ya Bunge. Bunge ni structured state organ na ni taasisi inayofuata prescribed procedures, rules na kuongozwa na katiba. Tofauti na activism ya jambo lolote huwa haielekei hata siku moja kufuata utaratibu ingawa kinadharia, wanashikilia kufanya kuwa na taratibu katika kudai wanachokitaka!

Katika karne hii baada ya liberal democracies kuingia kwa kasi tumeshuhudia uanaharakati kuingia kwenye bunge; mfano vyama vya kijani (green parties), ambao ni wanaharakati wa mazingira. Hata hao waliingia bungeni na hawajafaulu sana na walikuwa na lengo maalum.

Staili ya activism hii kwenye democracy mara nyingi tangu mwanzo wa karne hii tunaishuhudia kwenye vyombo vya habari (democratic media activism), ambayo inakubalika na jamii kwavile ni kati ya "social movement theories" za akina Melucci, Cohen+Arato, Habermas, na Fraser.

Uanaharakati kama tunaouona hapa Tz na ambao umekuwepo nchi nyingine (na sio kwenye mabunge), ambao wewe unatuaminisha ni sawa na wakudai haki na utawala bora, mara nyingi hufadhiliwa na vikundi kutoka nje ya nchi husika na huwa si endelevu kwavile baada ya kubadilisha utawala uliopo kwenye nchi husika, huishia hapo na makundi mengine ya kianaharakati huibuka kupinga status-quo! Ufadhili huo hufanywa na vikundi vyenye maslahi ya kiuchumi au with strategic interest kwa taifa husika!

Kulingana na historia, uanaharakati wa aina hii unatumika nje ya taasisi za kidola kama pressure groups ukisaidiwa sana na tasnia za habari.

Unaweza kusoma tofauti hizi kwenye kitabu cha Fishkin & Laslett cha 2008.

Swali dogo la kujiuliza ni kwanini theories za akina Lennin leo hazitawali tena dunia na zimebaki rejea za wanafunzi wa political history na uchumi wa kijamii? Hazina mshiko ena kwenye neo-political philosophy na hata uchumi jamii mamboleo.

Tunachangia hapa kupanuana uelewa tu na sio kudhalilishana au kubezana kama mwelekeo ninaouona kushamiri kwako. Utusamehe bure kama tunakuudhi Mheshimiwa.

Jambo ambalo nalishangaa kidogo kwenye hoja yako hapa ni uwezo gani ulio nao wa kudhani mtu anayekupinga kuwa na uelewa mdogo kuhusu jambo unaloelezea? Unajuaje uelewa wako ni wa juu kuliko wengine (authoritative)? Hiyo nayo ni dosari, kama mwanasiasa inabidi uibadilishe, ni sawa kama ungekuwa upo mahakamani ili kushinda kesi.
Ni tafakuri yangu tu!

Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

From: Tundu Lissu <lissubulali@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Sun, 19 Aug 2012 23:57:49 -0700 (PDT)
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Tony,

Nilichokisema bungeni kinaitwa na Kanuni za Kudumu za Bunge 'Maoni ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.' Kwa sababu hiyo, hayo ni maoni yangu. Lakini kwa kuwa yametolewa in my official capacity kama Msemaji wa Kambi, ni maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Tumejenga utamaduni mzuri katika Kambi yetu ambapo Maoni ya Msemaji wa Kambi hujadiliwa kwanza kabla ya kuwasilishwa Bungeni. Of course, kama Msemaji wa Kambi amefanya kazi yake sawa sawa, what's eventually presented in Parliament will bear a very strong imprint, if not style, of the author. Mimi huandika hotuba zangu mwenyewe, nafanya research mwenyewe na kwa hiyo whatever you see presented in the House bears my unmistakeable style and ideological bent hata kama kimejadiliwa na kupitishwa kwenye Kambi.

Kuhusu kuchanganya uanaharakati na siasa, n.k., nadhani uelewa wako wa historia ya Western democracies ni too limited kuweza kutusaidia kwenye mjadala huu. Kwa vile unaelekea kutokujua nitakuelekeza kwa wanaharakati wakubwa wa siasa za kimapinduzi wa karne iliyopita, Vladimir Lenin na Rosa Luxemburg ambao, licha ya ku-dedicate maisha yao yote kwenye harakati za kuupindua mfumo wa demokrasia ya kiliberali, waliandika sana juu ya haja, na namna, ya kutumia uwanja wa siasa za kibunge kwa malengo ya kimapinduzi. Rosa Luxemburg wrote a beautiful pamphlet titled 'Reform or Revolution'. Nakushauri ukitafute ukisome. Lenin, perhaps the greatest revolutionary mind since Marx, aliandika kijitabu kiitwacho 'Left Wing Communism or an Infantile Disorder?' ambapo alizungumzia sana umuhimu wa parliamentary politics. Kwa hiyo kaka, unachokisema kuhusu kutokupeleka uanaharakati Bungeni kinatoka zaidi kwenye kichwa chako na sio historia halisi ya demokrasia za Magharibi.

Tundu


From: deogratius temba <deojkt@yahoo.com>;
To: wanabidii@googlegroups.com <wanabidii@googlegroups.com>;
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
Sent: Fri, Aug 17, 2012 6:35:45 AM

Utamaduni wa kuendelea kulindana na kupena anafasi za kazi kwa wanaojulikana au waliotufanyia mambo fulani kama sehemu ya kulipana fadhila unaendelea. Taifa hili halitakaa libadilike kwa kuendelea kuwaajiri watu vihiyo, wasio na uwezo huku wenye uwezo wakikimbilia nchi za nje na wengine kujifanyia shughuli zao binafsi. kuna kundi la watanzania weledi, waadilifu na wenye uwezo mkubwa wa kubadilisha taifa hili lakini hawapewi nafasi kwasbabu tunataka watakaotulinda.
Suala la majaji ni la kusitikisha,  Rais anapoingia madarakani anataka kudfanya kazi na safu ya watu atakao watumikisha bila kuhojiwa, wasaidizi wa 'ndiyo mzee' ambao watafanya wanachoamabiwa bila kuhoji au kukataa, ambao wataamriwa kuvunja sheria, katiba au haki za binadamu na kukubali. hili linahitaji mabadiliko makubwa na ni Kuwa na katiba mpya nzuri itakayompokonya Rais wa Tanzania madaraka ya kuteua kila mtendaji wa serikali. Vinajana wanaohitimu vyuo vikuu sasa wataenda wapi? kama wazee wanateuliwa hata baada ya kupoteza uwezo wa kuona?
Hivi tujiulize Tume ya utumishi wa mhakama inafanya nini? kazi yke ni nini?  macommisner wa Tume nao wanakula mishara na posho bila kufanya kazi kumbe rais anateua majaji na watendaji wakuu wa mhakama peke take. Tubadilike, na tujitokeze kutoa maoni kwenye mchakato wa katiba mpya kama haturidhiki na hili.
 
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

"By faithfulness we are collected and wound up into unity within ourselves, whereas we had been scattered abroad in multiplicity"
Saint Augustine (354-430) Theologian


From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Friday, August 17, 2012 9:05 AM
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Flano;

Sidhani majadiliano ya wanachana wa mtandao yanaweza kuchapishwa bila kuvunja privacy na hatimilki ya wanachama. Watu huchangia hapa kwa sababu ya limited exposure principle; huenda wangejua kuwa wanachochangia hapa kitachapishwa magazetini wasingefanya hivyo.

Pia wanachama wa jukwaa wanachangia sio kwa nia ya kufanyia biashara maongezi yao. Na akichapisha mazungumzo haya kibiashara watafaidika vipi kutokana na mauzo ya nakala za gazeti hilo?


Mimi siafiki!

Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

From: flano mambo <flein47@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 16 Aug 2012 21:45:42 -0700 (PDT)
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Balile umelonga, ni vema wananchi wenzetu wanaoweza kununua gazeti wajue jinsi wenzao walivyopata fursa ya kubadilishana mawazo watawezajifunza namna watu wanavyotoa hoja na kuzitetea lakini pia mwelekeo wa mitazamo ya kisasa. Kaprint mazungumzo


From: "deobalile@yahoo.com" <deobalile@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com; Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Sent: Friday, August 17, 2012 7:37 AM
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Laurean, Katu, Tonya, Lissu, moderator na wanabidii wote,

Pamoja na salaam za gazeti la JAMHURI na kwa kuwa mjadala unaoendelea hapa umetokana na hatua ya gazeti letu kuchapisha habari hii ya Majaji Vihiyo Watajwa, na kwa kukuwa mjadala huu ni mtamu, naomba ruhusa yenu majadiliano haya niyachapishe katika toleo la JAMHURI Jumanne ijyayo na wananchi wasio na access ya mtandao wafaidi uhondo huu.

Naamini ombi langu litakubaliwa kwani maelezo haya tunayotoa kutoka kwenye sakafu za mioyo yetu na tungependa Watanzania watuelewe hivyo.

Asanteni kwa kunikubalia ombi langu.

Mtanzania mwenzenu,

Balile, D.
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

-----Original Message-----
From: "Laurean Rugambwa B. " <rugambwa@hotmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Fri, 17 Aug 2012 03:59:28
To: Tony PT<tony_uk45@yahoo.co.uk>; Wanabidii Group<wanabidii@googlegroups.com>
Reply-To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki,
maadili ya bunge

Tony,
Sijibu hoja zako maana umezielekeza kwa Mh. Lissu.
Naomba nichangie tena kwenye huu mjadala: itafute CV ya current CJ; then uje urudi hapa tuongee. Ukisha soma useme bila woga kama mtu kama huyo alifaa au alistahili kuwa CJ kati ya majaji wengine lukuki wenye sifa za kipee kwenye mahakama kuu na rufaa!

Wewe unajua ila unafanya makusudi kuwa suala la kuteuliwa kuwa jaji haliishii kwenye sifa za kikatiba za mtu anayefaa kuteuliwa kuwa jaji, hata maandishi yangu haya yanaweza kunifanya nisichaguliwe kuwa jaji hata kama nina sifa.

Maana wakati unawatetea watu  ujue mambo ya hivi yanavyoweza kumfanya mtu wa kawaida tu hata sio wewe mchambuzi wa mambo kuona kuwa kuna shida sana kwenye chombo cha kutoa haki.

Unasema Somalia, kwa utaratibu wa sasa usiporekebishwa nchi itakuwa Somalia.Hapa ndipo utaona madhara ya kutosema.

Uliona Jaji mtu mzima Kenya wakati wa Moi aliulizwa kwenye interview juzi kwanini hukumu zake zimekuwa zinaitetea serikali mara zote hakuwa na jibu wale jamaa tena vijana wakamnyima kazi ya Ujaji!

Asubuhi njema.
LR
Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.

-----Original Message-----
From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Date: Thu, 16 Aug 2012 20:09:25
To: <wanabidii@googlegroups.com>
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki,
maadili ya bunge

TL

Nimekuelewa na nafurahi kwa kunijuza kuwa ulishapeleka mambo haya kwenye kamati husika! Ninachotaka kufahamu toka kwako ni je, hoja hii ni ya kwako kama mbunge au ni ya kambi ya upinzani kama ilivyosomwa nawe bungeni?

Unachokisema ni sahihi, uozo ni mkubwa karibu kila sehemu! Lakini unadhani uanaharakati utaweza kuondosha uozo huu bila kufumua katiba na baadhi ya sheria zilizopo? Nasema hivi kwani ulichokisema kinaweza kupuuzwa kama CJ Ramadhani alivyofanya na pia CS Luhanjo alivyofanya na kufaulisha mikataba ya majaji licha ya taarifa ya kamati mkakati?

Tatizo la uanaharakati katika misingi ya kutumia mhimili mmoja wa dola unayoiona kuwa inafaa haileti matunda mema sana na haijafaulu sana kuleta mabadiliko unayoyaeleza sehemu nyingine za dunia hii. Uanaharakati wa nje ya mihili ya nchi ndiyo husaidia kwenye mabadiliko ya tawala na kurejesha utawala bora.

Kwa baadhi ya mataifa hususan ya magharibi, uanaharakati nje ya mihimili ya nchi husaidiwa sana na vyombo vya habari ambavyo havina maslahi ya wanaharakati hao au toka kwingine kati ya mihimili ya nchi. Napata taabu sana kuona kama uonavyo wewe, yaani kuchanganya siasa na uanaharakati na kutumia mhimili kama meza ya kuendesha harakati za kuumbua mihimili mingine!

Pia napata tatizo kukubali kama bunge kazi yake ni kuadabisha serikali. Dhana ya trinity of interdependence ndiyo inazaa taifa imara kila mhimili ukiheshimu mwingine kwa kufuata mipaka ya kazi inayoeleweka na inayotokana na katiba.
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.
From:  Tundu Lissu <lissubulali@yahoo.com>
Sender:  wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 16 Aug 2012 12:02:19 -0700 (PDT)
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo:  wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge



Tony,
 
Hoja zako hazina tofauti hata kidogo na hoja za mwanaCCM mmoja katika hao walionihoji. Kwa kifupi, watu wa aina yako hamkutaka haya mambo yasemwe popote hadharani. 'Kuheshimiana miongoni mwa vyombo vya dola' ni lugha ya waliozoea kufanya maovu gizani bila kuhojiwa kwa sababu uchafu wao hauonekani. Kuwasema hadharani watu wa aina hii ni njia pekee ya kuanza kuchukua hatua za kuondoa uozo huu na kuwaondoa wachafu wenyewe. Bunge halina wajibu wa 'kuheshimu' mihimili mingine kwa maana yako, lina wajibu wa kuisimamia na kuiadabisha inapotoka nje ya mstari wa kikatiba. Ndio maana Bunge lina mamlaka ya kumwondoa Rais madarakani kama anafanya matendo yanayoenda nje ya kiapo chake cha kuilinda, kuitetea na kuihifadhi Katiba. Bunge halitakaa litimize wajibu wake huo kama linafundishwa 'kuheshimu' maovu ya mihimili mingine linalopaswa kuisimamia kwa kuogopa kuyasema maovu hayo hadharani!
 
Uchafu niliouonyesha kwenye Addendum yangu umekuwepo siku nyingi. Kila anayetaka kujua uchafu huu anafahamu. Ikulu ya Kikwete inafahamu. Mwanasheria Mkuu wake anafahamu. Mahakama yenyewe inafahamu. Majaji wote wanafahamu. Mawakili wanafahamu. Kila mwenye macho anafahamu. Wote hawa wanaofahamu wamenyamaza kimya kwa sababu ya 'kuheshimiana.' Ni kulindana. Wako kimya kwa sababu wana maslahi ya kuwa kimya. Hawajali haki, wanajali maslahi yao. Hawajali kwamba mhimili wa Mahakama ukioza namna hii watu watalazimika kuchukua sheria mikononi mwao na nchi haitatawalika. wanajali maslahi yao ya sasa hivi. Kesho itajiju yenyewe.
 
Kwa bahati mbaya kabisa, Bunge letu sio la maCCM pekee yao tena. Bunge letu sio la waoga na wanaojipendekeza tu ili wapate trip za nje ya nchi za Spika. Bunge letu sio la wasiojua Kanuni tena au wasiojali kama kuna Kanuni au la. Kwa kifupi, Bunge letu sio la wajinga na wachumia tumbo tu. Bunge letu pia ni la wanaharakati wanaojali na wanaochukia uovu na kuchukua hatua za kuuondoa vile vile. Unafikiri kuitwa 'mwanaharakati' ni tusi. Mimi nadhani mwanaharakati, katika mazingira halisi ya nchi yetu, ni mtu pekee mwenye akili! Wengine wote ni wale wale wenye mtazamo ule ule wa chama kile kile! Nchi hii inahitaji mabadiliko, nay, mapinduzi makubwa! Mapinduzi hayo hayataletwa na watu wanaoogopa kuwaumbua waovu kwa kisingizio cha 'kuheshimiana.'
 
Na kwa taarifa yako, kwa sababu nilishakusikia ukihoji kama mambo haya yalipelekwa kwenye Kamati ya Katiba na Sheria kabla hayajafikishwa Bungeni. Hilo pia lilikuwa swali la Chiligati kwenye Kamati. Yalikwenda siku nyingi kabla ya kuzungumzwa Bungeni. Nilishawa-serve notice Karimjee Hall tangu mwezi Juni. Waziri na Naibu wake walikuwepo, Attorney General na Naibu wake na maafisa wao karibu wote walikuwepo. Wasajili kadhaa wa Mahakama Kuu na Mahakama va Rufani walikuwepo. They'd have seen it coming. Of course kwa sababu ya utamaduni wa kulindana na kuogopana, nay, 'kuheshimiana', wote walifikiri natania. I never joke on matters of this importance. Neither should you!
 
Now that the Djein is out of the bottle all cowards are waxing lyrical about 'kuheshimiana kwa mihimili ya dola'! Give me a break! Rais anapojaza Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani na Majaji wa aina hii anaonyesha wazi kwamba haheshimu muhimili wa Mahakama. Rais wa aina hii hapaswi kuheshimiwa, anapaswa kuwajibishwa kwa kuvunja Katiba. Impeachment is his due dessert. Majaji feki aliowajaza Mahakamani hawapaswi kuendelea kupokea mshahara wa umma wakati sio Majaji 'kwa mujibu wa Katiba.' Wanapaswa kujiuzulu au kuondolewa kama hawana uadilifu wa kuachia ngazi wenyewe. Tunapaswa kujifunza kwa wanavyofanya Wakenya kusafisha Mahakama yao baada ya miaka mingi ya uozo wa aina ya wa kwetu.
 
Kwa hiyo kaka Tony, I make no apologies whatsoever for having played my small part in this mighty contest. Castro said nearly sixty years in 'History Will Absolve Me', his defence speech after the unsuccessful assault on Moncada Garrison: "A true man chooses the side of duty, a true man does not choose the side of advantage." I've chosen my side, to do my duty, however unpleasant, and to do it thoroughly! You obviously have chosen the side of advantage, of 'kuheshimiana', etc. I wish you luck.
 
Tundu





From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, August 16, 2012 11:01 AM
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge


Weston,Unachosema ni sahihi, spika angeweza kuliona hilo na kuamua jambo hilo lirudishwe kwenye kamati husika. Lakini hilo unalolisema haliwezekani maana hoja za tundu lisu ziliwasilishwa kama hoja ya kambi ya upinzani, yeye akiwa msemaji wake mkuu wa wizara kivuli ya sheria na katibu.Wasiwasi wangu tukiendelea na utaratibu wa mhimili mmoja kuumbua mhimili mwingine ni kukosekana kwa staha ya kuheshimiana na kufikia kusambaratisha utawala mzima! Kila mhimili una madudu yake, bunge limejaa uozo, mahakama usiseme na serikalini ndio kilio! Sasa wakiumbuana wenyewe kitakachofuata ni taasisi zote kukosa legitimacy ya wananchi! Ndicho mnachokitaka? Hatari zake ni mbaya sana mithili ya Somalia.
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

From: weston mbuba <matutetz@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 16 Aug 2012 07:49:20 -0700 (PDT)
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge



Tony,
Hoja yako binafsi nimeielewa sana tu. Hupingi mapungufu ya uteuzi wa majaji. hupingi ushahidi wa Tundu Lissu (Mh.) na hupingi kuwa vyombo hivi vya dola havina matatizo. Tatizo lako ni namna ya uwasilishaji wa ushahidi kamaulivyofanywa na Mh. TL. Msingi wa hofu yako ni kuwa chombo cha dola kimoja kinaonekana kufedhehesha vyombo vingine vya dola, yaani Bunge linaviumbua Mahakama na Serikali. Hoja yako ni kuwa vyombo hivi viwekeane staha.
 
Hoja yako ina mantiki. Ila ulipaswa kutambua chanzo cha tatizo hili. Mh.TL alituhumiwa kwa uzushi. Alichokuwa anajaribu kufanya ni kuthibitisha kuwa hakusema uongo. Na mahali pa kuthibitishia ni Bungeni. Hata hivyo Spika alipaswa kutumia busara kuona ushahidi huu hautoki nje, na hasa ungeishia katika kamati. Kumlaumu mh. ni kumuonea. Alidhalilishwa sana siku ile. Kuambiwa kichwa ni kwa ajili ya kufikiri si kufuga tu nywele au wengine mnajifanya ni wasomi zaidi ya wengine si maneno mazuri kuambiwa mtu mzima.
 
Baeleze babunge ba CCM baache kutoa kashfa. bajenge hoja.--- On Thu, 8/16/12, Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:
From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thursday, August 16, 2012, 7:16 AM



Anael,Mbona arguments zenu hazizingatii uti wa hoja! Tatizo sio kutosema, na sijasema hivyo kwenye hoja yangu! Hoja ni unatumia utaratibu gani kusema kero hii! Tatizo lenu ninaloliona hapa jukwaani mara nyingi ni ushabiki wa kiitikadi! Akiongea lolote na kwa vyovyote vile mtu huyu ruksa, lakini akiongea mwingine wa itikadi ile na kwa njia ile, ni dhambi! Hiyo ni misguided fanaticism; tuachane nayo! Jukwaa ni la kuelimishana na sio kuenezea itikadi ya vyama.
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

From: Anael Macha <kowiri@hotmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 16 Aug 2012 16:43:11 +0300
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Sasa Tony, mhe Lissu asingesema haya ulitaka afenyeje? Afukuzwe/asimamishwe? Kwa msingi huu ulioueleza bora asingepelekwa kamati ya maadili. Au?Sent from my iPhone
On Aug 16, 2012, at 6:49, "Tony PT" <http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:

Martin,Unachokisema hapa ni sawa lakini sio jibu la nilichokisema. Matumizi ya lugha kufanana sio hoja na kama nilivyosema sitetei uozo kama alivyoueleza kwa ufanisi mkubwa Mhe TL. Tatizo langu nililosema hapa ni utaratibu alioutumia. Pia sioni ajabu kushambuliwa kwake na baadhi ya wabunge kwani wabunge walichokuwa wakikisema (ukiacha baadhi yao), ni pia utaratibu uliotumika. Mara nyingi mimi hutoa mchango hapa kuzingatia jambo mbele yetu na siendeshwi kirahisi na ushabiki wa kikundi fulani. Nimetoa maoni yangu sio kwa kuangalia ni nani amesema jambo.
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

From: martin pius <http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=malagila01@yahoo.co.uk>
Sender: http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 16 Aug 2012 03:33:14 +0100 (BST)
To: <http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Tony,

Shina la tatizo hapa sio Lissu "kuumbua mahakama". Ingawa nakushangaa unatumia neno lile lile walilotumia baadhi ywa wabunge kumshutumu mpaka akaambiwa alete ushahidi.

Tatizo niushabiki Bungeni. Kwa kuwa Mbunge anatoka upinzani, akisema jambo la maana lenye tija lakini linagusa ipasavyomhimili mmoja, anaonekana kichwa chake ni cha kufuia nywele tu, mchonganishi, ... Kama wangemwelewa mapema, wala isingefika hapo.

Huu ni ushahidi, na ushahidi unapaswa kupita vikwazo vyote vinavyoweza kuleta shaka. Jamaa kawasilisha. Tumeona.

Hii ni fundisho pia kwa wale wabunge ambao kazi yao ni kuomba miongozo na ushahidi wanapoona mtu anawasilisha jambo sensitive. Wawe wanatafakari kwanza na kupima weredi wao kwenye sualahusika!

Nadhani turejee kwenye mchakato wa Katiba Mpya tufanye kitu. Haya ni mapungufu ya Katiba Hii ya 1977 iliyorekebishwa mara 14.



--- On Wed, 15/8/12, Tony PT <http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:

From: Tony PT <http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=tony_uk45@yahoo.co.uk>
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
To: http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com
Date: Wednesday, 15 August, 2012, 23:49



Rama,Tundu kajieleza vizuri sana, lakini tatizo ni kama mbunge, hususan Mhe je, blatant attack aliyoifanya inakubalika kwa hali ya kiungwana ya bunge? Jibu mimi nasema ni hapana! Najua kuna watu watasema huu ni wakati wa uwazi na ukweli, sawa, lakini naona mie approach aliyoitumia tena akiwa na ushahidi wa kilo nyingi kama alio nao ni utaratibu wa uanaharakati zaidi ya Ubunge.Kama uanaharakati utakubalika bungeni ina maana dhana muhimu ya taifa kama taasisi unganiki (State institutional unity) inakwisha maana mihimili ya taifa inaheshimiana na kuogopana! Dhana hii ndiyo inaweka taifa kwenye misingi ya amani, uungwana na ustahimilivu. Hapa nina maana polisi lazima wawaheshimu jeshi, na jeshi vivyo hivyo waheshimu polisi na mahakama iheshimu utawala na utawala uheshimu mahakama. Hivyo hivyo bunge lazima liheshimiane na utawala na pia bunge liheshimu mahakama na kadhalika. Siku hizi vyombo vya dola navyo vinatarajiwa kuheshimu press na kutambua uwepo wake.Kuheshimina huku kunaleta doctrine ya "utenganifu wa vyombo vya dola" kuogopana na hivyo kuzuia uwezekano wa kujiona chombo kimoja ndicho muhimu kuliko kingine! Wanategemeana.Sasa nikirudi kwenye speech ya Mhe Tundu Lisu, kwanza nakubali kuwa amefanya utafiti wake vizuri (naturally as a reseacher of human rights issues), ni halali kabisa. Sasa, lakini nia yake kwa kuyasemea bungeni hadharani (public) ilikuwa ni ipi? Kuumbua utawala na Mahakama au kusisitiza? Je, kamati yake ya bunge ilishapata fursa kuyajua haya na hawakuona umuhimu wa kumuomba Mhe spika kufuatilia tuhuma hizi na kukataliwa? Sina jibu...Hili naliona kuwa sawa na uumbuaji uliofanywa na mamlaka ya vitambulisho vya taifa kwa jeshi la wananchi n.k. Nacho hakikuwa kitu sahihi ingawa mhusika aliachwa na mwajiri huenda kutokana na udhaifu wa mwajiri wake unaofahamika kwetu. Naelewa kuna watu hapa ni wana harakati watapinga taratibu zinazolinda kuheshimiana kwa dhana ya uhuru wa kutoa na kupata habari! Lakini je, hii dhana inayochanganya uanaharakati na misingi ya mfumo wa taifa lenye utengamano ni mzuri au kupotoka? Uanaharakati ni dhana inayojulikana kwetu kama huendeshwa na maslahi binafsi au ya kikundi. Hata funding yake duniani kote huhusishwa na maadui wa taifa husika, kwa hiyo ni maslahi ya eaqual-minded dudes for a certain fulfillment of interested objectives. Uanaharakati wa Tanzania upo sio kusahihisha paliposhindikana isipokuwa kuumbua hata pale wahusika ni hao hao wenyewe! Hapa naweza kuandika maelfu ya kurasa za ushahidi wa maoni yangu haya. Kwa mahitaji ya maoni-hoji ya mada hii, vyema kuishia hapa! Najaribu tu kuangalia alternative solutions za kuwa na utawala bora katika misingi ya falsafa ya siasa (political philosophy) na uhuru binafsi usiolalia maslahi ya wengi tu (utilitarian) na uhuru unaolalia haki za msingi za mtu (liberalism). Katika kutafuta muafaka wa mawazo yangu (huru na wajibishi, au free and responsible), naona kuwa kuna dosari kubwa ya uelewa wa majukumu yetu katika ngazi tofauti zinazotumikia umma au jamii! Tafakari...tunaelekea kubaya! Tukikubali kuumbuana, usione ajabu Tundu Lissu akakamatwa na kosa la traffic, mfano over-speeding, akapelekwa mahakamani na kupata kifungo cha miezi saba. Akikata rufaa, mahakama ya juu inaongeza kuwa mwaka mmoja! Sababu kubwa ni kuumbuana na kudharauliana! Tunakwenda kusiko, na sisi hapa jukwaani tunashabikia bila kuona mbele ya pua zetu! Naogopaaaaaaa!
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

From: RAMADHANI Selemani <http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=ramson34@gmail.com>
Sender: http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com
Date: Wed, 15 Aug 2012 23:04:01 +0300
To: <http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Mheshimiwa Tundu lissu kafunguka vizuri sana..nimeipenda sana hii...
On Aug 15, 2012 5:51 PM, "jacob towa" <towa.jacob@yahoo.com <> > wrote:




 Kwa kifupi kama yote haya aliyoyaeleza Mheshimiwa Tundu Lisu ni kweli basi wale jamaa waliokuwa wanasema anahadaa umma na serikali basi wao ndio waliokuwa wanahadaa wananchi nakuficha uovu. Hii taarifa imejitosheleza imetaja kila kitu kama ile taarifa ya kubenea hazina majibu mbele ya seriakali bali kinachofuata ni aibu kwa serikali na hata kwa wabunge waliokuwa wana mzomea Mheshimiwa Lisu.
Eng.Towa,Jacob Jeremiah
Hohai University
No.1 xikang Road
Nanjing 210098, Jiangsu Province,
People Republic Of China
phone:+8613813924107 <>
email:towa.jacob@yahoo.com <>
      towa.jacob@gmail.com <>
skype:jacobtowa




From: Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com <> >
To: wanabidii@googlegroups.com <> 
Sent: Wednesday, August 15, 2012 9:33 PM
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Duh! Bariki, Kazi ipo hapo...
2012/8/15 Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com <> > Hamis

Haya maelezo kama ni ya kweli kabisa pasipo na shaka sioni sababu ya hao wabunge waliosema kwamba Msemaji wa Upinzani kafanya hili na lile kwa Majaji, kuendelea kukalia viti na kupita kwenye lile zulia jekundu. Waachie tu ngazi kwani sioni mantiki ya mtu kukurupuka kusema bila kuwa na uhakika wa kile usemacho


2012/8/15 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com <> > UTANGULIZI


Julai 13, 2012 Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliwasilisha Maoni yake kuhusu Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Pamoja na mambo mengine, Maoni ya Kambi yalihusu utaratibu wa uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Tanzania.

Maoni ya Kambi yalizua mjadala mkubwa ndani na nje ya Bunge huku wachangiaji wengi wakimtuhumu Msemaji wa Kambi kwa "kuidhalilisha" Mahakama na/au "kuwadhalilisha majaji" (Gosbert Blandes-Karagwe CCM); "kuwavunjia heshima majaji" (Naibu Spika Job Ndugai); kuwatukana na kuwadhalilisha majaji (Murtaza Mangungu-Kilwa Kaskazini); "kuwa-offend, kuwadhalilisha na kuwanyanyasa majaji" (Assumpter Mshama-Nkenge CCM); "kufedhehesha Mahakama na majaji" (Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema).

Aidha, Msemaji wa Kambi alishambuliwa kwa kudaiwa kuwa mfitini na asiye na akili timamu (Muhammad Chomboh- Magomeni CCM)); na "kujiamini kwamba yeye anajua zaidi kuliko watu wengine wote" (Mangungu). Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alilihakikishia Bunge kwamba "... haijatokea hata siku moja katika nchi hii Rais akamteua Jaji wa Mahakama Kuu bila kuzingatia mapendekezo yaliyopelekwa kwake na hii Tume ya Uajiri wa Mahakama." Zaidi ya hayo, "... labda Mheshimiwa Lissu anamjua Jaji angalau mmoja na anaweza akamtaja aseme Jaji huyu ametolewa tu mitaani na Mheshimiwa Rais, yupi hakuna. hawa majaji wote walioteuliwa wamepitia mchakato huu wa kikao kizito sana cha watu ambao ndiyo wenye sheria ya nchi hii."

Baadaye Msemaji wa Kambi alitakiwa kufuta kauli yake kuhusu uteuzi wa majaji usiofuata utaratibu uliowekwa na Katiba. Msemaji wa Kambi alikataa kufuta kauli hiyo ambako Mwenyekiti wa Kikao alielekeza Msemaji wa Kambi apelekwe kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa hatua zaidi. Alichukua uamuzi huo ili masuala hayo yapatiwe ufafanuzi ili wananchi wapate picha kamili na ya kweli kuhusu jambo hili muhimu. Maelezo haya yana lengo la kutoa ufafanuzi huo.

Katika maelezo yake kwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya BUnge, Lissu alisema, "Nitajitahidi kwa kadri inavyowezekana kutoa ushahidi unaothibitisha kwamba siyo tu kwamba utaratibu wa kikatiba katika uteuzi wa majaji umekiukwa mara nyingi, bali pia majaji wengi walioteuliwa kwa utaratibu wa nje ya Katiba wamekuwa hawana 'uwezo, ujuzi na kwa kila hali hawakufaa kukabidhiwa Madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu."

TATIZO LA MUDA MREFU

Kuna ushahidi mkubwa kuthibitisha kwamba kuna watu wameteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu "... wakiwa wamekaribia muda wao wa kustaafu kwingineko katika utumishi wa umma (na) wanapewa 'zawadi' ya ujaji ili kuwawezesha kupata mafao ya majaji wastaafu ambayo yameboreshwa sana katika miaka ya karibuni." Ni muhimu kuweka wazi hapa kwamba utamaduni huu haukuanza baada ya Rais Jakaya Kikwete kuchaguliwa kuwa Rais, bali ni tatizo la muda mrefu. Kwa mfano, marehemu Jaji Kulwa Masaba na Jaji Madina Muro na majaji Stephen Ihema, Juxton Mlay, Augustine Shayo na Vincent Lyimo waliteuliwa majaji wa Mahakama Kuu baada ya utumishi wa muda mrefu kwingineko katika utumishi wa umma.

Majaji Masaba na Muro waliteuliwa huku wakiwa wagonjwa mahututi na - kwa kadri ninavyofahamu - hawakuwahi kuandika hukumu hata moja kabla ya mauti kuwafika! Jaji Lyimo aliteuliwa Machi 28, 2007 mwaka mmoja kabla ya muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo, ilipofika Oktoba 26, 2007 Katibu Mkuu Kiongozi wakati huo Phillemon Luhanjo alimtaarifu Jaji Mkuu kwamba Rais Kikwete "... ameamua kusogeza mbele muda wa kustaafu wa Mheshimiwa Jaji Vincent Kitubio Damian Lyimo kwa miaka mitatu kuanzia Machi 28, 2008 siku ambayo angestaafu kwa lazima"!

Kwa upande wao, Majaji Ihema, Mlay na Shayo walijizolea umaarufu kwa kuwa majaji wasioandika hukumu na hivyo kuwa wacheleweshaji wakubwa wa kesi katika Mahakama Kuu. Jaji Ihema alitia fora kwenye jambo hili kiasi kwamba Juni 16, 2003 Mwenyekiti wa sasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Mzee Joram Allute, alilazimika kumwandikia Rais Benjamin Mkapa maombi ya kumwondoa Jaji Ihema kama Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania "kwa uzembe na kukosa maadili."

Mzee Allute alikuwa na kesi kwa Jaji Ihema ambapo Jaji huyo 'alikalia' uamuzi kwa zaidi ya miaka minne hadi aliponyang'anywa faili la kesi hiyo na kukabidhiwa Jaji mwingine aliyeandika uamuzi ndani ya wiki tatu! Mwezi mmoja kabla ya barua ya Mzee Allute kwa Rais Mkapa, mawakili wake walikuwa wamemwandikia Jaji Mkuu Barnabas Samatta kulalamikia ucheleweshaji wa uamuzi wa kesi hiyo. Mawakili hao walidai: "Hadhi na heshima ya Mahakama inaporomoka vibaya kama inachukua zaidi ya miaka mitatu kwa Jaji kutafakari na kutoa uamuzi kwa jambo jepesi kama maombi ya pingamizi." Licha ya malalamiko haya dhidi yake, Jaji Ihema alipatiwa mkataba wa ajira wa miaka miwili mara baada ya kustaafu mwaka 2005.

MAJAJI WA MIKATABA

Agosti 2, 2005 Jaji Kiongozi Hamisi Msumi alitoa taarifa kwa majaji wote wa Mahakama Kuu kwamba Jaji Ihema alikuwa amepewa mkataba mpya baada ya kustaafu kama Jaji wa Mahakama Kuu. Taarifa hiyo ilimfanya Jaji Bernard Luanda, wakati huo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, kuhoji 'Uhalali Kikatiba kwa Majaji Kufanya Kazi kwa Mkataba Baada ya Kustaafu.' Katika taarifa yake kwa Jaji Kiongozi Msumi, Jaji Luanda alisema kwamba "... suala la majaji kupewa mikataba ... linaenda kinyume na Katiba." Jaji Luanda alifafanua: "Kwa kuwa Jaji amestaafu, basi kiapo chake nacho kimeondoka. Kwa bahati mbaya hawaapishwi ili washike kazi hizo za ujaji.... Ni hoja yangu kwamba Majaji waliostaafu na kupewa mikataba si Majaji kwa mujibu wa Katiba."

Msimamo wa Jaji Luanda uliungwa mkono mwaka mmoja baadaye na Jaji wa Rufaa, Augustino Ramadhani wakati huo akiwa Kaimu Jaji Mkuu. Katika 'Mawazo Kuhusu Vifungu Vinavyohusu Mahakama na Majaji' aliyomwandikia Jaji Mkuu Samatta na kunakiliwa kwa Majaji wa Rufaa wote, Jaji Ramadhani alisema kwamba "... sio sahihi kwa Jaji Mkuu kustaafu na kupewa mkataba wa kuendelea na wadhifa huo kupindukia umri wa miaka 65 (ambao ndio umri wa kustaafu kwa lazima kwa Jaji wa Rufaa na Jaji Mkuu)." Baadaye Jaji Luanda aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa wakati Jaji Ramadhani alikuja kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.

Kauli ya Kambi kwamba kuna ukiukaji mkubwa wa Katiba kuhusiana na uteuzi wa majaji inaungwa mkono na nyaraka za ndani ya Serikali na hasa Ofisi ya Rais, Ikulu yenyewe. Desemba 6, 2007, mkutano kuhusu ajira ya majaji waliostaafu ulifanyika Ikulu, Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu Kiongozi Luhanjo. Wajumbe wengine walikuwa pamoja na Mwanasheria Mkuu Johnson Mwanyika na Naibu wake Sazi Salula, Katibu Mkuu Utumishi George Yambesi, Msajili wa Mahakama ya Rufani, Sophia Wambura na Susan Mlawi wa Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri.

Kwa mujibu wa Kumbukumbu za Mkutano huo, "kwa utaratibu unaotumika sasa, baadhi ya Majaji wanaofikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa Ibara ya 110(1) kwa Majaji wa Mahakama Kuu na Ibara ya 120(1) ya Katiba wanaongezewa muda wa kuendelea na utumishi wao kwa mkataba baada ya wao kuwasilisha maombi rasmi." Baada ya mjadala juu ya jambo hili, wajumbe wa mkutano walikubaliana kwamba "utaratibu wa kuongeza muda kwa njia ya mkataba unakiuka masharti ya Katiba na kuleta mkanganyiko kama Majaji hao wanastahili kulipwa mshahara au pensheni au vyote kwa pamoja."

Matokeo ya mkutano wa Ikulu ilikuwa ni kuundwa kwa 'Kikundi Kazi kwa Ajili ya Kuchambua na Kushauri Kuhusu Ajira ya Majaji Baada ya Kustaafu' chini ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Kikundi Kazi kiliwasilisha Taarifa yake Machi 7, 2008. Katika Taarifa yake Kikundi Kazi kinakubaliana na msimamo wa kikatiba kwamba "kwa kuzingatia Ibara za 110 na 120 za Katiba inaonekana wazi kuwa suala la ajira za mikataba kwa Majaji ambao wamekuwa wakifanya kazi za Jaji baada ya kufikia umri wa kustaafu ni kinyume cha Katiba." Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, hadi mwezi Machi 2008, "... walikuwepo Majaji wawili ... wa Mahakama ya Rufani na Majaji tisa ... wa Mahakama Kuu, ambao wapo katika ajira za mkataba, na Jaji mmoja ... wa Mahakama Kuu aliyeongezewa muda wa ajira kwa mujibu wa masharti ya Katiba...."

Hii ina maana kwamba, kulikuwa na Majaji kumi na moja ambao walikuwa wanafanya kazi kinyume cha Katiba na - kwa maneno ya Jaji wa Rufaa Luanda - hawakuwa Majaji kwa mujibu wa Katiba! Aidha, kwa mujibu wa ushahidi wa nyaraka hizi, kulikuwa na Jaji mmoja tu ambaye alikuwa ameongezewa muda wa ajira ya ujaji kwa mujibu wa Katiba. Katika mapendekezo yake, Kikundi Kazi hakikumung'unya maneno:

"Mikataba iliyopo hivi sasa iko kinyume cha Katiba.... Hii ina maana kwamba Majaji hao wanafanya kazi ya Jaji kinyume cha Katiba, hivyo kazi zote ambazo wamezifanya na wanaendelea kuzifanya wakiwa chini ya ajira mpya za mikataba hazina uhalali wowote kisheria. Kazi hizo ni sawa kama vile zimefanywa na mtumishi mwingine yeyote asiye na madaraka ya Jaji. Hivyo basi, Rais ashauriwe kuifuta mikataba hiyo mara moja kwa vile ina madhara makubwa kwa jamii na katika uteuzi wa Majaji wapya kuchukua nafasi zao. Majaji waliofutiwa mikataba waendelee na pensheni zao kama kawaida."

Miaka minne imepita tangu Kikundi Kazi kiwasilishe mapendekezo yake Ikulu lakini hakuna hatua zilizochukuliwa kutekeleza mapendekezo hayo. Aidha, licha ya msimamo wa majaji Luanda na Ramadhani kuwa na umri wa takriban miaka saba, utaratibu wa uteuzi wa majaji wastaafu haujaachwa na mamlaka husika ya uteuzi. Ajira ya sasa ya Jaji Kiongozi Fakih Jundu iko katika kundi hili la watu wasiokuwa Majaji kwa mujibu wa Katiba.

JAJI KIONGOZI FAKIH JUNDU

Jaji Kiongozi Fakih Jundu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Rais Mkapa mwaka 2003. Julai 29, 2009, Jaji Jundu wakati huo akiwa Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Iringa, alitoa taarifa ya kustaafu kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo, mara baada ya kutoa taarifa hiyo, Jaji Jundu siyo tu alipewa mkataba wa ujaji kwa miaka mitatu, bali pia alipandishwa cheo na kufanywa Jaji Kiongozi.

Kama hiyo haitoshi, inasemekana sasa kwamba Jaji Kiongozi Jundu ameongezewa mkataba mwingine tena wa miaka miwili kuendelea kuwa Jaji Kiongozi kuanzia Julai 29, 2012! Huu ni ukiukaji wa Katiba. Kwanza, kwa mujibu wa Taarifa ya Kikundi Kazi, "... umri wa kustaafu wa Jaji Kiongozi ni miaka sitini.... Hivyo, iwapo Rais atamuongezea Jaji Kiongozi muda wa kufanya kazi, hatamuongezea kama Jaji Kiongozi."

Kwa maana nyingine, kama ilikuwa makosa kikatiba kumpa Jaji Jundu mkataba wa ajira kama Jaji wa kawaida, ilikuwa makosa makubwa zaidi kikatiba kumpandisha cheo na kumfanya Jaji Kiongozi wakati alikwishafikisha umri wa kustaafu wa Jaji Kiongozi! Pili, kwa utamaduni uliozoeleka Tanzania, majaji wamekuwa wanaongezewa kipindi kimoja cha miaka miwili ili wamalizie kesi walizokuwa nazo hadi muda wao wa kustaafu unawadia. Kwa msimamo wa kikatiba ulioelezwa na Jaji wa Rufaa Luanda, Jaji Mkuu Ramadhani na Kikundi Kazi, siyo sahihi kwa Jaji Kiongozi Jundu kustaafu na kupewa mkataba wa kuendelea na wadhifa huo kupindukia muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa Katiba!

Nyongeza hii ya pili ya mkataba wa Jaji Kiongozi Jundu imewafanya watu wanaojiita 'Watumishi wa Mhimili wa Mahakama' kumwandikia Msajili wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania kulalamikia jambo hilo. Kwa mujibu wa barua yao, ambayo pia ilinakiliwa kwa Mwanasheria Mkuu na Jaji Mkuu, watu hao wamesema yafuatayo kuhusu Jaji Kiongozi Jundu: "Sisi watumishi wa Mahakama tunafahamu udhaifu mkubwa kiutendaji alionao Jaji Kiongozi wetu wa sasa. Kimsingi hamudu madaraka haya. Ipo mifano mingi ya udhaifu wa Jaji Jundu. Mfano alimhamisha hakimu kutoka kituo chake cha kazi kama adhabu kwa vile hakimu huyo alitoa maamuzi ambayo yeye hakuyafurahiya kwenye ile kesi maarufu ya kibaragashia. Ni busara za Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman, ndizo zilizomsaidia hakimu huyo."

JAJI THOMAS MIHAYO

Thomas Bashite Mihayo aliteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Oktoba 8, 2003. Januari 16, 2006 Jaji Mihayo alitoa notisi ya kustaafu kwa mujibu wa Katiba kuanzia Juni 8, 2006 atakapokuwa ametimiza umri wa miaka sitini. Hata hivyo, Machi 8 ya mwaka huo, Jaji Mihayo alitaarifiwa na Jaji Mkuu kwamba Rais Kikwete alikuwa amempa "... mkataba wa miaka miwili kuanzia Juni 9, 2006." Mkataba huo ulifikia mwisho wake Juni 8, 2008. Hata hivyo, Jaji Mihayo alipatiwa mkataba mwingine tena wa mwaka mmoja ulioanzia Juni 9, 2008 hadi Juni 8, 2009 na baada ya hapo hakupatiwa mkataba mwingine.

Inaelekea Jaji Mkuu Ramadhani alisahau msimamo wake wa awali kuhusu ajira za mikataba kwani ndiye aliyependekeza Jaji Mihayo "... apewe mkataba mwingine wa mwaka mmoja..." Na wala si Jaji Mihayo pekee aliyepatiwa au kuongozewa mkataba katika mazingira tatanishi kama haya. Kwa mujibu wa nyaraka za Idara Kuu ya Utumishi, Jaji Donasian Mwita alipatiwa mkataba wa ujaji Juni 28, 2004. Mkataba huo wa miaka miwili ulianza kutumika Julai 1, 2004. Vile vile, Jaji Joseph Masanche alisaini mkataba wa aina hiyo hiyo na Idara Kuu ya Utumishi ulioanza kutumika kuanzia Machi 7, 2006.

MAADILI YENYE SHAKA

Msemaji wa Kambi hakuzungumzia masuala yanayohusu maadili ya majaji. Hata hivyo, kutokana na mjadala uliojitokeza ndani na nje ya Bunge kutokana na hotuba yake, ushahidi umepatikana unaoonyesha kwamba baadhi ya majaji wameteuliwa bila ya kwanza kuwafanyia uchunguzi juu ya maadili yao.

MAJAJI KASSIM NYANGARIKA NA ZAINAB G. MURUKE

Kassim Nyangarika alikuwa wakili wa kujitegemea na wakili mwenza wa Jaji Kiongozi Jundu kabla ya uteuzi wake kuwa Jaji wa Mahakama Kuu mwaka 2003. Kama wakili, Bwana Nyangarika aliwahi kumwakilisha mlalamikaji katika kesi ya Peter Muti dhidi ya CIELMAC Ltd., Kesi ya Madai Na. 314 ya 2003 iliyofunguliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni. Katika kesi hiyo mteja wa wakili Nyangarika alishinda.

Hata hivyo, kufuatia rufaa dhidi ya uamuzi huo, Mahakama Kuu ilifutilia mbali mwenendo wa kesi hiyo baada ya kugundua kwamba Wakili Nyangarika alikuwa amefanya vitendo vyenye kuashiria uvunjifu mkubwa wa maadili. Kwa mfano, Mahakama Kuu iligundua kuwa Wakili Nyangarika alimwelekeza hakimu - kwa kutumia 'kipande cha karatasi cha rafu na kilichoandikwa kirafiki' - namna ya kuendesha kesi hiyo. Mahakama Kuu iligundua makosa makubwa zaidi ya hilo. Kwa mujibu wa Jaji Kalegeya, "... kulikuwa na mawasiliano yasiyokuwa rasmi kati ya Mahakama na Wakili." Jaji Kalegeya alikuta ushahidi wa uwezekano mkubwa kwamba Wakili Nyangarika ndiye aliyeandaa uamuzi wa Mahakama katika kesi hiyo. Aidha, Mahakama Kuu iligundua kwamba Wakili Nyangarika "... aliielekeza Mahakama kutokutoa uamuzi kwa tarehe iliyopangwa badala yake aliielekeza itoe uamuzi huo tarehe nyingine."

Kwa mujibu wa Jaji Kalegeya, kama kilichoonyeshwa katika mawasiliano ya Wakili Nyangarika na Mahakama ya Wilaya kilikuwa cha kweli basi "... utoaji haki katika Mahakama hiyo uko katika hatari kubwa kama sio jina la Mahakama yote, kitu kinachohitaji marekebisho ya haraka." Kwa sababu hiyo, Jaji Kalegeya alielekeza kwamba "mamlaka husika zichukue hatua za kufichua ukweli kuhusu barua ya Wakili Nyangarika ya tarehe 18/03/2004." Hukumu na maelekezo ya Jaji Kalegeya yalitolewa tarehe 22 Julai, 2005. Miezi saba baadaye, Wakili Nyangarika aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania!

Wakili mwingine mwenye maadili ya mashaka yanayofanana na ya Jaji Nyangarika ambaye pia ameteuliwa Jaji Mahakama Kuu ni Zainab Muruke. Kama wakili, Zainab Muruke alimwakilisha Stephen Hill Forwood ambaye alikuwa amepatikana na hatia na kuhukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka miwili bila faini katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu. Baadaye kampuni ya mawakili ya Z.G. Muruke & Co. Advocates iliwasilisha Hati ya Mapitio (Memorandum of Review) katika Mahakama hiyo hiyo ikiomba Bwana Forwood abadilishiwe hukumu.

Ombi hilo lilikubaliwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Kabuta na tarehe 26 Julai, 2004, Bwana Forwood akabadilishiwa adhabu kuwa faini ya shilingi 20,000 au kifungo cha miaka miwili. Jambo hili liliripotiwa kwa Jaji Kiongozi ambaye aliamuru uchunguzi ufanywe uliopelekea kushushwa cheo cha Hakimu Mkazi Kabuta. Jaji Kiongozi pia aliamuru Wakili Muruke atoe maelekezo ya ushiriki wake katika sakata hilo. Hiyo ilikuwa tarehe 14 Desemba, 2004. Mwaka mmoja na miezi miwili baadaye, Zainab Muruke aliteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

MAJAJI PELAGIA B. KHADAY NA PATRICIA FIKIRINI

Bi. Pelagia B. Khaday ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania aliyeteuliwa mwaka 2009. Kabla ya uteuzi huo Bi. Khaday alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kabla ya hapo alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu na Msajili wa Wilaya, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha. Agosti 12, 2004, alipewa taarifa ya kusimamishwa kazi kama Msajili wa Wilaya na kuhamishiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na 'uzito wa shutuma' zilizotolewa dhidi yake kwa Jaji Mkuu.

Taarifa hiyo iliandikwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Edward Rutakangwa, kwa maelekezo ya Jaji Mkuu na ilieleza kwamba Bi. Khaday alikuwa anatuhumiwa kwa "kuwashinikiza au kuwashawishi baadhi ya mahakimu mkoani Arusha kushughulikia au kuamua kwa upendeleo mashauri yaliyowahusu ... jamaa au rafiki zake"; na "kuwaandalia sababu za rufaa baadhi ya washitakiwa waliotiwa hatiani na mahakama za mahakimu hapa mkoani."

Kabla ya kumsimamisha Bi. Khaday kazi, Jaji Mfawidhi Rutakangwa alikuwa amemteua Mheshimiwa Jacob Somi, wakati huo akiwa Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, kuwa Afisa Uchunguzi (Enquiry Officer) ili kuchunguza tuhuma dhidi ya Bi. Khaday. Taarifa ya Uchunguzi wa Awali ya Afisa Uchunguzi Somi inasema kwamba Bi. Khaday alikuwa amelalamikiwa na mahakimu kwa kuwashinikiza ili watoe maamuzi ya kesi zilizokuwa zinawakabili jamaa au marafiki zake.

Kwa mujibu wa Taarifa hiyo, Hakimu Mkazi Elvin Mugeta "alikiri kuwa-approached na Bi. Khaday ili atoe hukumu ya upendeleo kwa mshtakiwa Richard Bareto ambaye inasadikiwa kuwa ni jamaa wa rafiki yake wa karibu." Ijapokuwa Bi. Khaday alikanusha kufanya hivyo, Afisa wa Uchunguzi Somi aliridhika kwamba "Bi. Khaday alikuwa amejiwekea utaratibu, kama alivyodai mwenyewe, wa kuwasiliana na Mahakimu kwa lengo la kuwafahamisha pamoja na mambo mengine malalamiko yaliyokuwa yakimfikia dhidi yao ili kuwanusuru wasiharibikiwe."

Hata hivyo, Afisa Uchunguzi Somi aliridhika kwamba "utaratibu huu ulikuwa kero kwa mahakimu pale alipoutumia kwa kushinikizwa na jamaa zake na/au rafiki zake kwa lengo la kupata maamuzi ya upendeleo. Kitendo cha kumtoa mahakamani Hakimu kwa lengo la kutaka kujua hatima ya mshtakiwa Bareto aliyekuwa asomewe hukumu siku hiyo, ni mfano wa matumizi mabaya ya utaratibu huo."

Afisa Uchunguzi Somi hakupata uthibitisho wa madai ya Bi. Khaday kuwaandalia sababu za rufaa washtakiwa waliotiwa hatiani. Hata hivyo, kwa mujibu wa Taarifa yake, "... sikuridhishwa na utaratibu wake wa kupeleka nakala ya hukumu kwa Bi. Mushi na kumtaka aisome ili kuona kama kuna uwezekano wa mshtakiwa Hussein Ramadhani Kitema kukata rufaa Mahakama Kuu baada ya kufungwa jela na Bw. Mugeta." Afisa Uchunguzi Somi alipendekeza kwamba Bi. Khaday - "ambaye ni mtumishi wa Mahakama kwa kipindi kisichopungua miaka 20..." - apewe nafasi ya kujirekebisha.

Baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi, Jaji Mfawidhi Rutakangwa alimteua Mh. Samuel Karua, Msajili wa Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, kuwa Investigation Officer. Tarehe 23 Februari 2007, Investigation Officer Karua aliwasilisha Taarifa ya Uchunguzi wake kwa Jaji Mkuu. Taarifa ya Investigation Officer Karua ilimkosha Bi. Khaday kwa tuhuma zote dhidi yake.

Hata hivyo, Taarifa ya Investigation Officer Karua ina maeneo mengi yanayoleta mashaka. Kwanza, kama Investigation Officer Karua mwenyewe alivyosema, shahidi muhimu katika uchunguzi wake alikuwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mushi. Vile vile, shahidi huyu alikuwa 'star witness' katika uchunguzi wa awali mbele ya Afisa Uchunguzi Somi na ndiye aliyetoa ushahidi wa yeye na mahakimu wengine kuingiliwa katika kazi zao na Bi. Khaday.

Hata hivyo, mbele ya Investigation Officer Karua, shahidi huyu muhimu alikana kila kitu alichokisema mbele ya Afisa Uchunguzi Somi. Kwa kiasi kikubwa, Investigation Officer Karua aliitumia about turn hii kumkosha Bi. Khaday dhidi ya tuhuma zote zilizokuwa zinamkabili. Cha kushangaza ni kwamba Investigation Officer Karua hakujiuliza na hakumuuliza shahidi huyu sababu za kukana ushahidi wote alioutoa mbele ya Afisa Uchunguzi Somi.

Je, alirubuniwa au kutishwa ili amsaidie Hakimu na mtumishi mwenzake katika Mahakama ya Tanzania asifukuzwe kazi? Kama sio hivyo, je, ni sababu zipi zilizomfanya shahidi huyu muhimu kubadili ushahidi wake kwa kiasi hicho? Je, ushahidi alioutoa shahidi huyu mbele ya Afisa Uchunguzi Somi ulikuwa wa uongo? Na kama ulikuwa wa uongo, ushahidi wake wa pili kwa Investigation Officer Karua ni wa kweli kiasi gani mpaka kumfanya Investigation Officer Karua kutamka kuwa shahidi huyu 'anaweza ... kuwa anasema ukweli.'

Inaelekea Investigation Officer Karua, Hakimu Mkuu Mkazi mwenye uzoefu wa miaka mingi katika Mahakama, alifanya kazi yake kwa mtazamo wa kimahakama zaidi badala ya kutumia mtazamo wa kiupelelezi na/au kiuchunguzi ambayo hasa ndiyo ilikuwa kazi yake katika uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Bi. Khaday. Kwa mtazamo wa kimahakama, ukweli kwamba shahidi muhimu kama Hakimu Mkazi Mfawidhi Mushi alikana ushahidi wake wa awali mbele ya Afisa Uchunguzi Somi ilikuwa inatosha kumfutia Bi. Khaday hatia yote. Kwa mtazamo wa kiupelelezi/kiuchunguzi, about turn ya shahidi huyu ingemfanya Investigation Officer Karua kuchunguza zaidi sababu za kigeugeu hicho.

Pili, Investigation Officer Karua hakuipa uzito wa kutosha Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi. Kwa mfano, Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi - yenye kurasa 14 zilizochapwa - imeelezewa katika Taarifa ya Investigation Officer Karua kwa aya moja tu! Kwa sababu hiyo, ni vigumu kukubaliana na Investigation Officer Karua kwamba Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi 'ilikuwa muhimu sana' wakati umuhimu huo haujafafanuliwa wala kuelezewa hata kidogo katika Taarifa yake.

Aidha, Investigation Officer Karua alitakiwa kueleza sababu za kutofautiana na Afisa Uchunguzi Somi kwamba Bi. Khaday alikuwa anakera mahakimu kwa kuwasiliana nao baada ya kushinikizwa na ndugu au rafiki zake ili wapatiwe upendeleo katika kesi zilizokuwa zinawakabili. Investigation Officer Karua hakufanya hivyo. Vile vile, Investigation Officer Karua hakuona ajabu wala kujiuliza kama ilikuwa ni kitu cha kawaida kwa Bi. Khaday kumleta Richard Bareto - mshtakiwa aliyehusishwa na shinikizo la Bi. Khaday kwa Hakimu Mkazi Mugeta - kama shahidi wake wa utetezi.

Tatu, Investigation Officer Karua hakutoa sababu za maana za kutochukua ushahidi wa mahakimu wengine waliodaiwa kushinikizwa na Bi. Khaday. Katika aya moja tu iliyowahusu mahakimu hao, Investigation Officer Karua alisema kwamba siku ya kutoa ushahidi wao kwake, watu hao "... walishikilia msimamo wa kauli walizotoa mbele ya Bwana Somi ... na baada ya tafakuri ya muda ... mashahidi hawa waliachiwa."

Mbele ya Afisa Uchunguzi Somi, mashahidi hawa wawili, Hakimu Mkazi Msumi na Hakimu Mkuu wa Wilaya Mlay, walikuwa wamesema kwamba "... huko nyuma (Bwana Msumi) aliwahi kuitwa na mlalamikiwa baada ya wadhamini walioshindwa kukidhi masharti ya dhamana ... kumpelekea malalamiko ya kukataliwa dhamana, maelezo ambayo hayakuwa na ukweli wowote." Aidha, kwa mujibu wa Afisa Uchunguzi Somi, "... katika hali isiyokuwa ya kawaida Bw. Mlay, PDM hakuwa tayari kueleza kilichomsibu hadi kujiengua katika usikilizaji wa kesi ambayo Bi. Mushi alidai ilikuwa inamkabili rafiki yake wa karibu na Bi. Khaday." Investigation Officer Karua hakuona sababu yoyote ya kufuatilia ushahidi wa mahakimu hawa wawili!

Nne, Investigation Officer Karua anakubali kwamba hali ilikuwa tete katika Kituo cha Arusha: "Inaelekea mtuhumiwa alikuwa na mahusiano mabaya na baadhi ya mahakimu." Kama hivyo ndivyo ilivyokuwa, Investigation Officer Karua alikuwa na wajibu wa kuchunguza chanzo cha mahusiano hayo mabaya, hasa kwa vile kulikuwa sio tu na tuhuma bali pia ushahidi wa mahakimu husika kwamba Bi. Khaday alikuwa anawaingilia mahakimu katika kazi zao. Hakufanya hivyo. Badala yake Taarifa ya Investigation Officer Karua inaonekana kama jitihada za kumkosha Bi. Khaday dhidi ya tuhuma nzito za ukosefu wa maadili ya kimahakama. Jitihada hizi zilifanikiwa kwani miaka miwili baada ya Taarifa ya Investigation Officer Karua, Bi. Khaday aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Na wala siyo Bi. Khaday pekee aliyeneemeka na taarifa hiyo. Bi. Patricia Fikirini, ambaye Taarifa ya Afisa Uchunguzi Somi inamwelezea kama mmoja wa mahakimu waliosikiliza kesi ya mfanyabiashara maarufu wa Arusha, Justin Nyari iliyokuwa chanzo cha tuhuma dhidi ya Bi. Khaday - alihusishwa na tuhuma dhidi ya Bi. Khaday kwa maneno yafuatayo: "... Kama mtawala ... (Bi. Khaday) ... alisema aliwahi, tena kwa nia njema, kumweleza Bi. Fikirini ... kuhusu uvumi kwamba mume wake alikwenda gerezani na kuchukua mamilioni ya fedha kwa Bw. Nyari na hivyo kumshauri awe mwangalifu zaidi"! Katika uteuzi wa majaji uliofanywa na Rais Kikwete mwezi Juni mwaka huu, Bi. Patricia Fikirini naye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Wapo wanaoweza kusema kwamba Bi. Khaday hakupatikana na hatia yoyote na kwa hiyo haikuwa makosa kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu. Aidha, inaweza kudaiwa kwamba Bi. Fikirini hajawahi kutuhumiwa kwa kosa lolote la maadili na kwamba 'uvumi' pekee hautoshi kumnyima mtu mwenye sifa haki ya kuteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu. Kwa wenye hoja za aina hii jibu langu ni kwamba kiwango cha 'sifa maalum' kinachotakiwa na Katiba kwa mtu kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ni mtu ambaye "... kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu...." Kiwango hiki ni cha juu kiasi kwamba kutokuwa na hatia pekee haitoshi kumfanya mhusika kuwa 'kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu.' Kwa maoni yangu, mtu aliyeundiwa uchunguzi wa kimaadili au ambaye kuna uvumi unaomhusisha na rushwa 'hafai kwa kila hali' kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu. Majaji Khaday na Fikirini wapo kwenye kundi hili.

JAJI ALOYSIUS MUJULIZI

Jaji Aloysius Mujulizi alikuwa miongoni mwa watu ishirini walioteuliwa Majaji wa Mahakama Kuu mwezi Februari, 2006. Kabla ya uteuzi wake, Jaji Mujulizi alikuwa wakili wa kujitegemea katika kampuni ya mawakili ya Ishengoma, Masha, Magai & Mujulizi Advocates (IMMMA) ya Dar es Salaam. Kampuni hii ya mawakili ndiyo iliyoshiriki katika kuanzishwa kwa kampuni iitwayo Deep Green Finance Co. Ltd. mnamo tarehe 18 Machi 2004. IMMMA Advocates vile vile walikuwa mawakili wa Tangold Ltd.

Makampuni haya mawili yanatuhumiwa kutumika kupitishia mabilioni ya fedha zilizoibiwa Benki Kuu ya Tanzania kati ya mwaka 2005 na 2006. Kwa mfano, katika kipindi kifupi cha miezi minne kati ya Agosti 1 na Desemba 10, 2005 kampuni ya Deep Green Finance ilipokea jumla ya shilingi 10,484,005,815.39 kutoka akaunti ya kulipia madeni ya nje (EPA) iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania. Katika kipindi hicho hicho, kampuni ya Tangold Ltd. ililipwa dola za Marekani 13,736,628.73 kutoka kwenye akaunti hiyo ya EPA. Nyaraka zilizowasilishwa BRELA na mawakili wa IMMMA Advocates na kusainiwa na Gavana wa Benki Kuu wa wakati huo Daudi Ballali tarehe 20 Mei 2005 zinaonyesha kwamba Tangold Limited ilikuwa kampuni ya kigeni kutoka Jamhuri ya Mauritius. Haya yote yalitokea wakati Jaji Mujulizi akiwa wakili mwenza wa IMMMA Advocates.

'SIFA MAALUM' ZENYE SHAKA

JAJI WA RUFAA MBAROUK SALIM MBAROUK

Mbarouk Salim Mbarouk aliteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania mwaka 2008. Kabla ya uteuzi huo Jaji Mbarouk alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Sifa za mtu kuteuliwa kuwa Jaji wa Rufaa zimeainishwa katika ibara ya 118(3) ya Katiba: "Majaji ... wa Rufani watateuliwa na Rais, kwa kushauriana na Jaji Mkuu, kutoka miongoni mwa watu wenye sifa za kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ... zilizoainishwa katika Ibara ya 109 ya Katiba au kutoka miongoni mwa watu wanaoweza kuteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa mujibu wa sheria zinazotumika Zanzibar na wamekuwa na sifa hizo kwa muda usiopungua miaka kumi na tano."

Kwa mujibu wa Ibara ya 94(3) ya Katiba ya Zanzibar, 1984, "mtu hatoweza kuteuliwa kuwa Jaji au Kaimu Jaji wa Mahkama Kuu mpaka awe na shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu kinachotambuliwa au Chuo cha aina hiyo; au awe au amewahi kuwa Jaji wa Mahkama zilizofanana na hii kwa kesi zote za jinai na madai katika Tanzania au sehemu yoyote ya Jumuiya ya Madola au Mahkama ya Rufaa kutoka Mahkama hizo; au awe Mwanasheria wa Zanzibar au Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka saba; au awe na uzoefu wa Jaji au mwanasheria kwa pamoja usiopungua miaka saba." Jaji Mbarouk hajatimiza hata moja ya masharti hayo ya Katiba ya Zanzibar. Jaji huyu hana shahada yoyote ya sheria inayotambuliwa na mamlaka ya ithibati ya Tanzania kama inavyotakiwa na Ibara ya 109(7) ya Katiba. Jaji huyu ana stashahada ya juu ya sheria (Post Graduate Diploma in Law) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya Uzamili ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha nchini Uingereza.

Uteuzi wa Jaji Mbarouk kuwa Jaji wa Rufaa ulileta minong'ono mingi katika taaluma ya sheria kiasi kwamba marehemu Wakili Leopold Kalunga anasemekana kufungua shauri katika Mahakama Kuu ya Tanzania kutaka uteuzi huo utenguliwe. Hata hivyo, Wakili Kalunga alifariki kabla ya shauri lake kusikilizwa na kwa hiyo liliondolewa mahakamani. Aidha, monong'ono hiyo ilimfanya Jaji wa Rufaa Mbarouk kujiunga na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambako bado ni mwanafunzi hadi ninapoandika Addendum hii.

MAJAJI 'WALIOTOLEWA MITAANI'

Katika Maoni ya Kambi tulidai kwamba "... sasa watu wanateuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ambao hawajawahi kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na - kwa sababu hiyo - hawajafanyiwa vetting yoyote na mamlaka hiyo ya kikatiba...." Ukiacha uteuzi wa Jaji wa Rufaa Mbarouk ambao haubanwi na masharti ya Ibara ya 109(1) na 113(1)(a) ya Katiba, majaji wengine waliotajwa kwenye Addendum hii hawakupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama. Majaji wengine ambao pia hawajawahi kupendekezwa na Tume hiyo ni pamoja Fatuma Massengi, Mary Sumari, Imani Mkwawa-Aboud na Sekela Mushi. --
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com <>  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Bariki G. Mwasaga,
P.O. Box 3021,
Dar es Salaam, Tanzania
+255 754 812 387 <> 

-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com <>  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- "Vision is the ability to see the invisible!"Hamisi A. Kigwangalla, MD, MPH, MBAP.O.Box 22499,Dar es salaam.Tanzania.Phone No: +255 754 636963 <>                 +255 782 636963 <> website: http://www.peercorpstrust.org/ or http://www.hamisikigwangalla.com/Email: hamisi.kigwangalla@peercorpstrust.org <>  or info@hamisikigwangalla.com <> Skype ID: hkigwangallaBlog: blog.hamisikigwangalla.com <http://blog.hamisikigwangalla.com/>  -- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com <>  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com <>  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/ Kujiondoa Tuma Email kwenda http://us.mc1121.mail.yahoo.com/mc/compose?to=wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  -- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  -- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.  

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.




--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment