Monday 20 August 2012

Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

LK

Inawezekana nina kichaa kikali lakini sijaambiwa hivyo na daktari (psychiatrist), labda kama wewe unaweza nipe diagnosis. Hata hivyo nitakwenda kupata secondary opinion, ili nijue kama upo sahihi! Ukichaa upo kwa watu wote ila tunaziadiana tu, na kikiwa kikali unapelekwa kulazwa au unafungwa kamba!

Hata hivyo watu hawataki kubishiwa hasa wanapokuwa na kujiamini kuwa wanachosema ni sawa (nao ni ugonjwa). Hapa kuna wengine watabishia anything kitokacho kwa "Y" na kuunga mkono lolote la "X". Kwa misingi hii sioni shida ya kutokuwa akawaida (sub normality or abnormal) unayotaka kupendekeza maana nabishana na kundi kubwa linaloingia kwenye high degree ya biased and preconceived characters. Kwenye organizations kama hii, ni sawa kutofautiana ili mradi hatupigani.

Usipopenda ninachokisema, dawa yake usisome na usichangie! Kwa kufanya hivyo utakuwa na amani na huna sababu ya kuniweka kwenye kundi la dosari za akili! Ni walewale...; mkitawala nyinyi mtaua watu kwa kubishiwa au kupingwa mnachotaka!

Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

From: Lutgardk <lutgardk@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Mon, 20 Aug 2012 20:34:59 +0300
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Tony,
Kwa nia njema kabisa, naomba nikuulize; hivi wewe unaona ni kawaida kwa watu wote hawa kupingana na wewe? Unatumia muda mwingi sana kupambana na haya mabishano, kweli bado hujaona kuwa hapo kuna tatizo kwa upanda wako? Jitambue. LKK

Sent from my iPad

On 20 Ago 2012, at 7:19 alasiri, Tony <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:

Peter,

Soma thread zetu zote. Kwa bahati mbaya wachangiaji wengine hawafuati threading procedures ya blogs na forums, hivyo uunganishaji unaweza ukakupatia tabu kidogo.  Jitume kama tulivyojituma wakati wa michango yetu, sitaweza kurudia tena. Wanajukwaa walio na majibu zaidi watakusaidia.




From: Peter Lwegasira <petermakatu@yahoo.com>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, 20 August 2012, 19:09
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Tony,
 
Hii ni sehemu ya hotuba ya Mh. Tundu Lisu inayohusu hoja iliyoko ukumbini. Bado nauliza swali lile lile. Tuelimishane zaidi.
 
 
UTEUZI WA MAJAJI

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inatambua ukweli kwamba Rais Kikwete ameteua Majaji wengi wa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano kuliko Marais wengine wote waliomtangulia kwa ujumla wao. Rekodi hii peke yake inaonyesha kwamba Rais anatambua umuhimu wa Mahakama Kuu kuwa na watendaji wa kutosha wa utoaji haki ili kutekeleza dira ya 'haki kwa wote na kwa wakati.' Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, kuteua Majaji wengi ni jambo moja. Kuteua Majaji wengi wenye uwezo, ujuzi na wanaofaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu ni jambo jingine kabisa. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inasikitishwa na dalili zinazoanza kuonekana wazi kwamba baadhi ya Majaji walioteuliwa na Rais hawana uwezo, ujuzi na/au hawakufaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji ya Mahakama Kuu. Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa ibara ya 109(6) ya Katiba, mtu anaweza kuteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu ikiwa ana 'sifa maalum', na amekuwa na mojawapo ya sifa maalum kwa muda usiopungua miaka kumi. Sifa hizo, kwa mujibu wa ibara ndogo ya (7), maana yake "ni mtu aliye na shahada ya sheria kutoka chuo kikuu kinachotambuliwa na mamlaka ya ithibati Tanzania na amekuwa hakimu; amefanya kazi katika utumishi wa umma akiwa na sifa za kufanya kazi ya uwakili au ni wakili wa kujitegemea; ana sifa ya kusajiliwa wakili, na amekuwa na sifa hizo mfululizo kwa muda usiopungua miaka kumi." Sharti la kuwa na sifa hizo kwa miaka kumi mfululizo linaweza kutenguliwa endapo Rais – baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahakama - atatosheka kwamba mhusika ana uwezo, ujuzi na kwa kila hali anafaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu na kuna sababu za kumfanya mtu huyo astahili kukabidhiwa madaraka hayo. (ibara ya 109(8) Tume ya Utumishi wa Mahakama inaundwa na Jaji Mkuu ambaye ni Mwenyekiti wake, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufaa atakayeteuliwa na Rais kwa kushauriana na Jaji Mkuu, Jaji Kiongozi na wajumbe wawili watakaoteuliwa na Rais. Jukumu la kwanza la Tume hii, kufuatana na ibara ya 113(1)(a), ni "kumshauri Rais kuhusu uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu." Ni wazi kwamba utaratibu huu wa uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu ulilenga kumwezesha Rais – ambaye sio lazima awe mwanasheria na/au mwenye ufahamu wa masuala ya kisheria – kuteua Majaji baada ya kupata ushauri kutoka kwa viongozi waandamizi wa Mahakama ya Tanzania na pia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye anawajibika kikatiba "... kutoa ushauri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu mambo yote ya kisheria...." (ibara ya 59(3) Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Rais hana mamlaka ya kufanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu nje ya utaratibu huu uliowekwa na Katiba. Hata hivyo, Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina taarifa kwamba utaratibu huu wa kuteua Majaji umeachwa kufuatwa. Kwa mujibu wa taarifa tulizo nazo, sasa watu wanateuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ambao hawajawahi kupendekezwa na Tume ya Utumishi wa Mahakama na - kwa sababu hiyo - hawajafanyiwa vetting yoyote na mamlaka hiyo ya kikatiba juu ya uwezo na ujuzi wao na kama 'wanafaa kwa kila hali kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu.' Inaelekea watu hao – wengi wao wakiwa wamekaribia muda wao wa kustaafu kwingineko katika utumishi wa umma – wanapewa 'zawadi' ya ujaji ili kuwawezesha kupata mafao ya Majaji wastaafu ambayo yameboreshwa sana katika miaka ya karibuni. Matokeo yake ni kuwa na majaji ambao wamechoka na hawawezi au hawajui namna ya kufanya kazi ya Jaji wa Mahakama Kuu. Mheshimiwa Spika, Madhara ya kukiuka utaratibu huu wa kikatiba wa uteuzi wa Majaji wa Mahakama Kuu ni makubwa na yameanza kujitokeza wazi. Kwanza, wapo Majaji ambao – kwa sababu ya kutokufanyiwavetting na Tume ya Utumishi wa Mahakama – hawana uwezo wa kuandika mwenendo wa mashauri na hukumu zinazosomeka kwa sababu ya, ama kutokuwa na uwezo na ujuzi wa sheria, au kutokuwa na weledi wa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo lugha rasmi ya mwenendo wa mashauri na hukumu. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inazo taarifa kwamba wapo Majaji ambao – kwa sababu hizo hizo za kutokufanyiwa vetting juu ya uwezo na ujuzi wao na mamlaka husika ya kikatiba – wameshindwa kabisa kuandika hukumu za kesi walizozisikiliza na hivyo kusababisha mlundikano wa kesi mahakamani usiokuwa na sababu yoyote ya msingi. Kazi ya Jaji wa Mahakama Kuu, kama ilivyo kazi ya mawakili na wanasheria kwa ujumla, ni kazi ya kisomi. Ni kazi inayohitaji watu wenye uwezo mkubwa kitaaluma na utafiti, weledi wa uchambuzi (analytical skills) na wa kuandika na kuzungumza kwa lugha ya kimombo fasaha. Watu hawa hawaitwi 'wanasheria wasomi' kama mapambo tu. Wanatakiwa kuwa wasomi kweli kweli. Kwa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kuwa na Majaji wasiokuwa na sifa hizi sio tu kunafifisha utoaji wa haki kwa wadaawa katika mashauri yaliyoko mahakamani, bali pia kunaifedhehesha taaluma nzima ya sheria, Mahakama ya Tanzania na mamlaka yao ya uteuzi, yaani Rais mwenyewe. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe ufafanuzi juu ya jambo hili na pia itoe kauli mbele ya Bunge hili tukufu kwamba utaratibu wa uteuzi wa Majaji uliowekwa na Katiba utaheshimiwa kwa Rais kuteua Majaji watakaotokana na ushauri wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ili kuondokana na aibu na fedheha hii ya kuwa na Majaji wasiojua wanachotakiwa kufanya.

From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, August 20, 2012 6:38 PM
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
Peter,
 
Hotuba ya mhe niliisikiliza tangua mwanzo hadi mwisho. Kama wewe hujaona dosari, naona nisijipe jukumu gumu la kueleza dosari zipo wapi na nimekwishaeleza kwa aina yote na kutumia maneno yote kwenye postings za awali. Jitume kidogo usikilize hotuba, halafu usome thread zote za wachangiaji na ujipime baada ya hapo kama utakuwa bado na swali tutajaribu kukusaidia kama utakuja open-minded bro.
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.
From: Peter Lwegasira <petermakatu@yahoo.com>
Date: Mon, 20 Aug 2012 08:31:16 -0700 (PDT)
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Tony,
 
Kama unalalamikia utaratibu alioutumia Mh. Tundu Lisu kuwasilisha bungeni hotuba yake na sio utetezi wake kwenye kamati, kuumbuana unakokusema kunatokea wapi?

From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, August 20, 2012 4:46 PM
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
Anael, Narudia kusema kuwa mie nalalamikia utaratibu alioutumia kuwasilisha hoja bungeni (hotuba yake) na sio utetezi wake kwenye kamati! Mbona mnakosa umakini wa kuelewa hoja nyieee? Ndio maana nasema ushabiki wa itikadi unawaponzaa! Siamini kama baadhi yenu ni vilaza kiasi hicho, mnafanya makusudi kutokana na kughubikwa na ulevi wa itikadi! Au hamsomi mtiririko wa uchangiaji, mnarukia katikati! Watanzania tuna ulemavu wa kutosoma na tunaposoma hatuzingatii yaliyoandikwa! Sitaki kuamini wewe ni mmoja wapo!
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.
From: Anael Macha <kowiri@hotmail.com>
Date: Mon, 20 Aug 2012 16:38:06 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Tony,

Naomba unisaidie, Mhe TL aliambiwa alete utetezi kaleta wewe unamlaumu. Ulitaka apeleke nini? Naomba unijibu as unalikwepa ukilalamikia ushabiki. Sina hakika kama unajua nina kadi ya chama gani.

Kama Jaji Werema au Spika wangekaa kimya baada ya kauli ya TL haya yangetokea? Kwanini tusione akina spika ndo wameamua kutoheshimu mihimili mingine?

Asante
Sent from my iPhone
On Aug 20, 2012, at 16:29, "Chambi Chachage" <chambi78@yahoo.com> wrote:
Tony, hiyo ni strategy ya muda mrefu ya kukimbia ama kuzima hoja; sisi ngoja tujikumbushie harakati za Clare Short kwenye Bunge la Uingereza:

31 Jan 2007: January 30 session: Former international development secretary Clare Short attacked the government, as it came under fire from all sides over the sale of a radar system to Tanzania.


-------
My mission is to acquire, produce and disseminate knowledge on and about humanity as well as divinity, especially as it relates to Africa, in a constructive and liberating manner to people wherever they may be.

Address: 41 Banks Street # 1, Cambridge, MA 02138 USA
Cellphone: US = +1 (857) 413 - 9521/TZ = +255754771763
Skype:

0 comments:

Post a Comment