Monday 20 August 2012

RE: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Tatizo ni kwamba mabaya ya serikali yanasikika zaidi kuliko mazuri, sijui kama sababu ni kuwa mazuri hayapo, hayaonekani au hayasemwi, i mean for a reason or another serikali imekuwa branded na taswira mbaya, hivyo inakuwa rahisi kwa watu kuamini kila baya linalosemwa kwa serikali. Nakubaliana na wewe kuwa mapinduzi ya kifikra yanahitajika, lakini sio kwa wapokea habari (wananchi) kama ambavyo ungependa wewe, bali kwa watendaji wenyewe.


From: kailima kombwey <kailima.kombwey@googlemail.com>
Sent: Monday, August 20, 2012 16:09
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Ndugu zangu nadhani hapa kuna mambo mawili 1. kwanza TL ana nafasi ya kuwasilisha utetezi wake kwenye Kamati. Swali je amewasilisha utetezi huu kwenye Kamati kisha akaupeleka kwenye  vyombo vya habari au aumefanya kinyume chake i.e kuwasilisha utetezi kwenye vyombo vya habari kabla ya kuuwasilisha kwenye Kamati? 2. Hivi sasa Watanzania tumefikia sehemu kwamba akitoa hoja mtu Nayoisema Serikali hata kama hoja ni sahihi au siyo sahihi na akawa hakutumia utaratibu unaopaswa na akatokea mtu akaweka utaratibu basi huyo mtu wa pili huonekana kama hana akili vile. Lakini wanasias wengi wanatumia uwezo wetu mfinyu wa kutafakali mambo kutufanya tuamini wanachosema kwa kuwa hatuna muda w kutafakali. Kunahutakika MAPINDUZI YA KIFIKRA

On Aug 20, 2012 3:48 PM, "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:
Edgar,

Soma thru posting zangu!
Ninachopinga sio maneno au utetezi wake, ninapinga approach au utaratibu alioutumia! Uozo upo, lakini sio mahakama au majaji wote hawajui kiingereza, kuandika hukumu n.k. Kwa kutangazia umma ili uelewe hivyo! Kuna majaji wazuri, qualified na waadilifu!

Ukumbuke utetezi wa TL kwenye kamati ndio umetaja mifano michache na akaeleweka. Mimi naongelea approach ya kutuhumu mhimili wote kwenye bunge zima. Bungeni hakutoa mifano aliyotoa kwenye kamati. Aliyoyasema ni kweli yametokea. Ninachosisitiza ni kuwa uozo huu angepeleka ombi kwa spika (kwa maandishi) ili kuomba aieleze kamati husika kuhusu uozo wa majaji. Spika angekataa, hapo ilikuwa halali kufanya alichofanya!
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

From: Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>


[The entire original message is not included]

0 comments:

Post a Comment