Tony,
Hoja zako hazina tofauti hata kidogo na hoja za mwanaCCM mmoja katika hao walionihoji. Kwa kifupi, watu wa aina yako hamkutaka haya mambo yasemwe popote hadharani. 'Kuheshimiana miongoni mwa vyombo vya dola' ni lugha ya waliozoea kufanya maovu gizani bila kuhojiwa kwa sababu uchafu wao hauonekani. Kuwasema hadharani watu wa aina hii ni njia pekee ya kuanza kuchukua hatua za kuondoa uozo huu na kuwaondoa wachafu wenyewe. Bunge halina wajibu wa 'kuheshimu' mihimili mingine kwa maana yako, lina wajibu wa kuisimamia na kuiadabisha inapotoka nje ya mstari wa kikatiba. Ndio maana Bunge lina mamlaka ya kumwondoa Rais madarakani kama anafanya matendo yanayoenda nje ya kiapo chake cha kuilinda, kuitetea na kuihifadhi Katiba. Bunge halitakaa litimize wajibu wake huo kama linafundishwa 'kuheshimu' maovu ya mihimili mingine linalopaswa kuisimamia kwa kuogopa kuyasema maovu hayo hadharani!
Uchafu niliouonyesha kwenye Addendum yangu umekuwepo siku nyingi. Kila anayetaka kujua uchafu huu anafahamu. Ikulu ya Kikwete inafahamu. Mwanasheria Mkuu wake anafahamu. Mahakama yenyewe inafahamu. Majaji wote wanafahamu. Mawakili wanafahamu. Kila mwenye macho anafahamu. Wote hawa wanaofahamu wamenyamaza kimya kwa sababu ya 'kuheshimiana.' Ni kulindana. Wako kimya kwa sababu wana maslahi ya kuwa kimya. Hawajali haki, wanajali maslahi yao. Hawajali kwamba mhimili wa Mahakama ukioza namna hii watu watalazimika kuchukua sheria mikononi mwao na nchi haitatawalika. wanajali maslahi yao ya sasa hivi. Kesho itajiju yenyewe.
Kwa bahati mbaya kabisa, Bunge letu sio la maCCM pekee yao tena. Bunge letu sio la waoga na wanaojipendekeza tu ili wapate trip za nje ya nchi za Spika. Bunge letu sio la wasiojua Kanuni tena au wasiojali kama kuna Kanuni au la. Kwa kifupi, Bunge letu sio la wajinga na wachumia tumbo tu. Bunge letu pia ni la wanaharakati wanaojali na wanaochukia uovu na kuchukua hatua za kuuondoa vile vile. Unafikiri kuitwa 'mwanaharakati' ni tusi. Mimi nadhani mwanaharakati, katika mazingira halisi ya nchi yetu, ni mtu pekee mwenye akili! Wengine wote ni wale wale wenye mtazamo ule ule wa chama kile kile! Nchi hii inahitaji mabadiliko, nay, mapinduzi makubwa! Mapinduzi hayo hayataletwa na watu wanaoogopa kuwaumbua waovu kwa kisingizio cha 'kuheshimiana.'
Na kwa taarifa yako, kwa sababu nilishakusikia ukihoji kama mambo haya yalipelekwa kwenye Kamati ya Katiba na Sheria kabla hayajafikishwa Bungeni. Hilo pia lilikuwa swali la Chiligati kwenye Kamati. Yalikwenda siku nyingi kabla ya kuzungumzwa Bungeni. Nilishawa-serve notice Karimjee Hall tangu mwezi Juni. Waziri na Naibu wake walikuwepo, Attorney General na Naibu wake na maafisa wao karibu wote walikuwepo. Wasajili kadhaa wa Mahakama Kuu na Mahakama va Rufani walikuwepo. They'd have seen it coming. Of course kwa sababu ya utamaduni wa kulindana na kuogopana, nay, 'kuheshimiana', wote walifikiri natania. I never joke on matters of this importance. Neither should you!
Now that the Djein is out of the bottle all cowards are waxing lyrical about 'kuheshimiana kwa mihimili ya dola'! Give me a break! Rais anapojaza Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani na Majaji wa aina hii anaonyesha wazi kwamba haheshimu muhimili wa Mahakama. Rais wa aina hii hapaswi kuheshimiwa, anapaswa kuwajibishwa kwa kuvunja Katiba. Impeachment is his due dessert. Majaji feki aliowajaza Mahakamani hawapaswi kuendelea kupokea mshahara wa umma wakati sio Majaji 'kwa mujibu wa Katiba.' Wanapaswa kujiuzulu au kuondolewa kama hawana uadilifu wa kuachia ngazi wenyewe. Tunapaswa kujifunza kwa wanavyofanya Wakenya kusafisha Mahakama yao baada ya miaka mingi ya uozo wa aina ya wa kwetu.
Kwa hiyo kaka Tony, I make no apologies whatsoever for having played my small part in this mighty contest. Castro said nearly sixty years in 'History Will Absolve Me', his defence speech after the unsuccessful assault on Moncada Garrison: "A true man chooses the side of duty, a true man does not choose the side of advantage." I've chosen my side, to do my duty, however unpleasant, and to do it thoroughly! You obviously have chosen the side of advantage, of 'kuheshimiana', etc. I wish you luck.
Tundu
From: Tony PT <tony_uk45@yahoo.co.uk>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, August 16, 2012 11:01 AM
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Thursday, August 16, 2012 11:01 AM
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
Weston,Unachosema ni sahihi, spika angeweza kuliona hilo na kuamua jambo hilo lirudishwe kwenye kamati husika. Lakini hilo unalolisema haliwezekani maana hoja za tundu lisu ziliwasilishwa kama hoja ya kambi ya upinzani, yeye akiwa msemaji wake mkuu wa wizara kivuli ya sheria na katibu.Wasiwasi wangu tukiendelea na utaratibu wa mhimili mmoja kuumbua mhimili mwingine ni kukosekana kwa staha ya kuheshimiana na kufikia kusambaratisha utawala mzima! Kila mhimili una madudu yake, bunge limejaa uozo, mahakama usiseme na serikalini ndio kilio! Sasa wakiumbuana wenyewe kitakachofuata ni taasisi zote kukosa legitimacy ya wananchi! Ndicho mnachokitaka? Hatari zake ni mbaya sana mithili ya Somalia.
-- Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.comPata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.comBlogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com Kujiondoa Tuma Email kwenda wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma Disclaimer:Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
-- Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.
From: weston mbuba <matutetz@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 16 Aug 2012 07:49:20 -0700 (PDT)
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge
Tony, Hoja yako binafsi nimeielewa sana tu. Hupingi mapungufu ya uteuzi wa majaji. hupingi ushahidi wa Tundu Lissu (Mh.) na hupingi kuwa vyombo hivi vya dola havina matatizo. Tatizo lako ni namna ya uwasilishaji wa ushahidi kamaulivyofanywa na Mh. TL. Msingi wa hofu yako ni kuwa chombo cha dola kimoja kinaonekana kufedhehesha vyombo vingine vya dola, yaani Bunge linaviumbua Mahakama na Serikali. Hoja yako ni kuwa vyombo hivi viwekeane staha. Hoja yako ina mantiki. Ila ulipaswa kutambua chanzo cha tatizo hili. Mh.TL alituhumiwa kwa uzushi. Alichokuwa anajaribu kufanya ni kuthibitisha kuwa hakusema uongo. Na mahali pa kuthibitishia ni Bungeni. Hata hivyo Spika alipaswa kutumia busara kuona ushahidi huu hautoki nje, na hasa ungeishia katika kamati. Kumlaumu mh. ni kumuonea. Alidhalilishwa sana siku ile. Kuambiwa kichwa ni kwa ajili ya kufikiri si kufuga tu nywele au wengine mnajifanya ni wasomi zaidi ya wengine si maneno mazuri kuambiwa mtu mzima. Baeleze babunge ba CCM baache kutoa kashfa. bajenge hoja.
|
0 comments:
Post a Comment