Thursday 16 August 2012

Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Moses,

Siwezi kutetea blindly! Wewe ndiye unayeshabikia blindly!

Tumia maneno mengine kwa kujenga hoja ya kuonyesha wapi unadhani natetea blindly! Huenda naona mbali kuliko unavyodhani wewe.

Tafakari!
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

From: moses <mosesgasana@yahoo.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Thu, 16 Aug 2012 12:46:06 +0300
To: wanabidii@googlegroups.com<wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Tony,
Kuwa mkweli bro usitetee tu watawala wetu so blindly kama kawaida yako! Issue ya majaji kama ingeelezwa kama unavyofikiria wewe public isingejua.Mwache Lissu amkosoe Le Prezidaa huko huko Parliament huenda itaweka pressure na kunyoosha mambo

Sent from my iPhone

On Aug 16, 2012, at 10:52 AM, "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk> wrote:

Ezekiel,

Tupambane na weakness kwa njia muafaka! Mapambano ya kusababisha vifo sio ya kidemokrasia ila ni kiana-harakati! Kama njia ndiyo hiyo ni sawa lakini kinyume chake njia nyingine zikitumiwa, zinapelekea uvurugaji wa dhana ya utawala bora!
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

Date: Thu, 16 Aug 2012 04:15:21 +0000
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Tony

Huo utaratibu unaousema ungewzekana kama tungekuwa na mifumo mizuri ya utawala au mihimili yenyewe ingekuwa inafanya kazi sawa sawa, lakini kwa hali ilivyo sasa hivi mambo ni magumu, Bunge ndilo hilo! Mahakama ndiyo hiyo! Na Serikali ndiyo hiya! Nani afanye hiyo process????

Nakubaliana na wewe kabisa kwamba kwa sasa Mh T akipata tatizo la trafic anaweza kuhukumiwa kwenda Jela bila faini, lakini kwenye vita huwezi kuogopa kufa. Labda tutakapopata Katiba mpya uwajibikaji kwenye mihimili unaweza kubadilika.




Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

From: "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Date: Wed, 15 Aug 2012 21:25:33 +0000
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Ezekiel,

Nazumgumzia process ya kusahihishana na sio kufichiana uovu! Nakuamini kwa uelewa mkubwa, sidhani unapata shida kuelewa lugha au mantiki ya nilichokisema.

Nazungumzia utaratibu usiozingatia misingi ya kuumbuana! Wanaweza kuogopana kwa sababu nyingi; mojawapo ni hiyo ya kuumbuana ambayo inazaa visasi na mwisho wake ni mbaya kwa taifa na dhana ya utawala bora. Ya pili ni ya kutumia vitengo ndani ya taasisi moja kama vile kamati na kanuni zake ndani ya taasisi ya bunge. Nchi nyingi zinatumia utaratibu huu, za presidential na parliamentary systems.

Lakini nyingine ni iliyokuwepo hapa tangu uhuru ya kutumia mwimbisha kwaya mmoja ambaye ni Rais na taasisi yake. Hii hata mie siipendi!

Sijui nimeeleweka!
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

Date: Wed, 15 Aug 2012 21:08:13 +0000
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Tony sijui kama nimekuelewa vizuri, nikijumuisha maelezo yako kwa kifupi unasema kwamba inabidi mihimili mitatu ya Bunge, Serikali na Mahakama viheshimiane kwa maana kwamba Mhimili mmoja ukibaini matatizo ya Mhimili mwingine umezee au utafute njia ya kificho kuwasiliana na hii ni kwa faida ya mihimili yenyewe.

Naomba nitofautiane nawe kwamba ikifanyika hivyo atakayeumia ni mwananchi. Fikiria katika yaliyosemwa kwenye ripoti ya Mheshimiwa kuhusu uteuzi wa watu wenye kutiliwa mashaka kushika nyadhifa nyeti huko mahakamani, huu ni mzigo mkubwa sana kwa mwananchi mlipa kodi. Uwezo mdogo wa jaji au hakimu waweza kumfanya atoe hukumu kimakosa au asitoe hukumu kwa wakati au kwa kujua udhaifu wake ampendelee aliyemteua.

Mambo yakitoka wazi namna hii yanaweza kuzuia au kupunguza uwezekano wa kutokea tena. Maelezo yako kuhusu wanaharakati na nafasi yao katika jamii naona yanahitaji masahihisho pia.



Nawasilisha
Sent from my BlackBerry® smartphone from Vodacom

From: "Tony PT" <tony_uk45@yahoo.co.uk>
Date: Wed, 15 Aug 2012 20:49:30 +0000
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Rama,

Tundu kajieleza vizuri sana, lakini tatizo ni kama mbunge, hususan Mhe je, blatant attack aliyoifanya inakubalika kwa hali ya kiungwana ya bunge? Jibu mimi nasema ni hapana! Najua kuna watu watasema huu ni wakati wa uwazi na ukweli, sawa, lakini naona mie approach aliyoitumia tena akiwa na ushahidi wa kilo nyingi kama alio nao ni utaratibu wa uanaharakati zaidi ya Ubunge.

Kama uanaharakati utakubalika bungeni ina maana dhana muhimu ya taifa kama taasisi unganiki (State institutional unity) inakwisha maana mihimili ya taifa inaheshimiana na kuogopana! Dhana hii ndiyo inaweka taifa kwenye misingi ya amani, uungwana na ustahimilivu. Hapa nina maana polisi lazima wawaheshimu jeshi, na jeshi vivyo hivyo waheshimu polisi na mahakama iheshimu utawala na utawala uheshimu mahakama. Hivyo hivyo bunge lazima liheshimiane na utawala na pia bunge liheshimu mahakama na kadhalika.
Siku hizi vyombo vya dola navyo vinatarajiwa kuheshimu press na kutambua uwepo wake.

Kuheshimina huku kunaleta doctrine ya "utenganifu wa vyombo vya dola" kuogopana na hivyo kuzuia uwezekano wa kujiona chombo kimoja ndicho muhimu kuliko kingine! Wanategemeana.

Sasa nikirudi kwenye speech ya Mhe Tundu Lisu, kwanza nakubali kuwa amefanya utafiti wake vizuri (naturally as a reseacher of human rights issues), ni halali kabisa. Sasa, lakini nia yake kwa kuyasemea bungeni hadharani (public) ilikuwa ni ipi? Kuumbua utawala na Mahakama au kusisitiza? Je, kamati yake ya bunge ilishapata fursa kuyajua haya na hawakuona umuhimu wa kumuomba Mhe spika kufuatilia tuhuma hizi na kukataliwa? Sina jibu...

Hili naliona kuwa sawa na uumbuaji uliofanywa na mamlaka ya vitambulisho vya taifa kwa jeshi la wananchi n.k. Nacho hakikuwa kitu sahihi ingawa mhusika aliachwa na mwajiri huenda kutokana na udhaifu wa mwajiri wake unaofahamika kwetu.

Naelewa kuna watu hapa ni wana harakati watapinga taratibu zinazolinda kuheshimiana kwa dhana ya uhuru wa kutoa na kupata habari! Lakini je, hii dhana inayochanganya uanaharakati na misingi ya mfumo wa taifa lenye utengamano ni mzuri au kupotoka? Uanaharakati ni dhana inayojulikana kwetu kama huendeshwa na maslahi binafsi au ya kikundi. Hata funding yake duniani kote huhusishwa na maadui wa taifa husika, kwa hiyo ni maslahi ya eaqual-minded dudes for a certain fulfillment of interested objectives.

Uanaharakati wa Tanzania upo sio kusahihisha paliposhindikana isipokuwa kuumbua hata pale wahusika ni hao hao wenyewe! Hapa naweza kuandika maelfu ya kurasa za ushahidi wa maoni yangu haya. Kwa mahitaji ya maoni-hoji ya mada hii, vyema kuishia hapa!

Najaribu tu kuangalia alternative solutions za kuwa na utawala bora katika misingi ya falsafa ya siasa (political philosophy) na uhuru binafsi usiolalia maslahi ya wengi tu (utilitarian) na uhuru unaolalia haki za msingi za mtu (liberalism).

Katika kutafuta muafaka wa mawazo yangu (huru na wajibishi, au free and responsible), naona kuwa kuna dosari kubwa ya uelewa wa majukumu yetu katika ngazi tofauti zinazotumikia umma au jamii!

Tafakari...tunaelekea kubaya! Tukikubali kuumbuana, usione ajabu Tundu Lissu akakamatwa na kosa la traffic, mfano over-speeding, akapelekwa mahakamani na kupata kifungo cha miezi saba. Akikata rufaa, mahakama ya juu inaongeza kuwa mwaka mmoja! Sababu kubwa ni kuumbuana na kudharauliana!

Tunakwenda kusiko, na sisi hapa jukwaani tunashabikia bila kuona mbele ya pua zetu!

Naogopaaaaaaa!
Sent from my BlackBerry® Porsche-9981 smartphone Thru Tigo Network, Tanzania.

From: RAMADHANI Selemani <ramson34@gmail.com>
Date: Wed, 15 Aug 2012 23:04:01 +0300
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Mheshimiwa Tundu lissu kafunguka vizuri sana..nimeipenda sana hii...

On Aug 15, 2012 5:51 PM, "jacob towa" <towa.jacob@yahoo.com> wrote:

 Kwa kifupi kama yote haya aliyoyaeleza Mheshimiwa Tundu Lisu ni kweli basi wale jamaa waliokuwa wanasema anahadaa umma na serikali basi wao ndio waliokuwa wanahadaa wananchi nakuficha uovu. Hii taarifa imejitosheleza imetaja kila kitu kama ile taarifa ya kubenea hazina majibu mbele ya seriakali bali kinachofuata ni aibu kwa serikali na hata kwa wabunge waliokuwa wana mzomea Mheshimiwa Lisu.
Eng.Towa,Jacob Jeremiah
Hohai University
No.1 xikang Road
Nanjing 210098, Jiangsu Province,
People Republic Of China
phone:+8613813924107
email:towa.jacob@yahoo.com
      towa.jacob@gmail.com
skype:jacobtowa


From: Dr. Hamisi A. Kigwangalla <hkigwangalla@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Wednesday, August 15, 2012 9:33 PM
Subject: Re: [wanabidii] Utetezi wa Mhe Tundu Lisu mbele ya kamati ya haki, maadili ya bunge

Duh! Bariki, Kazi ipo hapo...

2012/8/15 Bariki Mwasaga <bmwasaga@gmail.com>
Hamis

Haya maelezo kama ni ya kweli kabisa pasipo na shaka sioni sababu ya hao wabunge waliosema kwamba Msemaji wa Upinzani kafanya hili na lile kwa Majaji, kuendelea kukalia viti na kupita kwenye lile zulia jekundu. Waachie tu ngazi kwani sioni mantiki ya mtu kukurupuka kusema bila kuwa na uhakika wa kile usemacho


2012/8/15 Abdalah Hamis <hamisznz@gmail.com>
UTANGULIZI


Julai 13, 2012 Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliwasilisha Maoni yake kuhusu Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Pamoja na mambo mengine, Maoni ya Kambi yalihusu utaratibu wa uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Tanzania.

Maoni ya Kambi yalizua mjadala mkubwa ndani na nje ya Bunge huku wachangiaji wengi wakimtuhumu Msemaji wa Kambi kwa "kuidhalilisha" Mahakama na/au "kuwadhalilisha majaji" (Gosbert Blandes-Karagwe CCM); "kuwavunjia heshima majaji" (Naibu Spika Job Ndugai); kuwatukana na kuwadhalilisha majaji (Murtaza Mangungu-Kilwa Kaskazini); "kuwa-offend, kuwadhalilisha na kuwanyanyasa majaji" (Assumpter Mshama-Nkenge CCM); "kufedhehesha Mahakama na majaji" (Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema).

Aidha, Msemaji wa Kambi alishambuliwa kwa kudaiwa kuwa mfitini na asiye na akili timamu (Muhammad Chomboh- Magomeni CCM)); na "kujiamini kwamba yeye anajua zaidi kuliko watu wengine wote" (Mangungu). Kwa upande wake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alilihakikishia Bunge kwamba "... haijatokea hata siku moja katika nchi hii Rais akamteua Jaji wa Mahakama Kuu bila kuzingatia mapendekezo yaliyopelekwa kwake na hii Tume ya Uajiri wa Mahakama." Zaidi ya hayo, "... labda Mheshimiwa Lissu anamjua Jaji angalau mmoja na anaweza akamtaja aseme Jaji huyu ametolewa tu mitaani na Mheshimiwa Rais, yupi hakuna… hawa majaji wote walioteuliwa wamepitia mchakato huu wa kikao kizito sana cha watu ambao ndiyo wenye sheria ya nchi hii."

Baadaye Msemaji wa Kambi alitakiwa kufuta kauli yake kuhusu uteuzi wa majaji usiofuata utaratibu uliowekwa na Katiba. Msemaji wa Kambi alikataa kufuta kauli hiyo ambako Mwenyekiti wa Kikao alielekeza Msemaji wa Kambi apelekwe kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa hatua zaidi. Alichukua uamuzi huo ili masuala hayo yapatiwe ufafanuzi ili wananchi wapate picha kamili na ya kweli kuhusu jambo hili muhimu. Maelezo haya yana lengo la kutoa ufafanuzi huo.

Katika maelezo yake kwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya BUnge, Lissu alisema, "Nitajitahidi kwa kadri inavyowezekana kutoa ushahidi unaothibitisha kwamba siyo tu kwamba utaratibu wa kikatiba katika uteuzi wa majaji umekiukwa mara nyingi, bali pia majaji wengi walioteuliwa kwa utaratibu wa nje ya Katiba wamekuwa hawana 'uwezo, ujuzi na kwa kila hali hawakufaa kukabidhiwa Madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu."

TATIZO LA MUDA MREFU

Kuna ushahidi mkubwa kuthibitisha kwamba kuna watu wameteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama Kuu "... wakiwa wamekaribia muda wao wa kustaafu kwingineko katika utumishi wa umma (na) wanapewa 'zawadi' ya ujaji ili kuwawezesha kupata mafao ya majaji wastaafu ambayo yameboreshwa sana katika miaka ya karibuni." Ni muhimu kuweka wazi hapa kwamba utamaduni huu haukuanza baada ya Rais Jakaya Kikwete kuchaguliwa kuwa Rais, bali ni tatizo la muda mrefu. Kwa mfano, marehemu Jaji Kulwa Masaba na Jaji Madina Muro na majaji Stephen Ihema, Juxton Mlay, Augustine Shayo na Vincent Lyimo waliteuliwa majaji wa Mahakama Kuu baada ya utumishi wa muda mrefu kwingineko katika utumishi wa umma.

Majaji Masaba na Muro waliteuliwa huku wakiwa wagonjwa mahututi na – kwa kadri ninavyofahamu - hawakuwahi kuandika hukumu hata moja kabla ya mauti kuwafika! Jaji Lyimo aliteuliwa Machi 28, 2007 mwaka mmoja kabla ya muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo, ilipofika Oktoba 26, 2007 Katibu Mkuu Kiongozi wakati huo Phillemon Luhanjo alimtaarifu Jaji Mkuu kwamba Rais Kikwete "... ameamua kusogeza mbele muda wa kustaafu wa Mheshimiwa Jaji Vincent Kitubio Damian Lyimo kwa miaka mitatu kuanzia Machi 28, 2008 siku ambayo angestaafu kwa lazima"!

Kwa upande wao, Majaji Ihema, Mlay na Shayo walijizolea umaarufu kw

0 comments:

Post a Comment