Monday 6 August 2012

Re: [wanabidii] Re: NDOA YA DR SLAA ILIFANYIKA?

Ndugu wanabidii, hebu tusome makala hii hapa chini ili mjue ni kwa vigezo gani ndoa hii ilifungwa badala ya kuanza kuspeculate sababu za kutupilia mbali amri ya mahakama. Makala hii iliandikwa na Joseph Magata, mwandishi wa gazeti la Tanzania daima.
 

JULAI 12 mwaka huu baadhi ya magazeti yalipambwa na vichwa vya habari juu ya ndoa tarajiwa ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa.

Moja ya gazeti liliandika kuwa kiongozi huyo alifunguliwa kesi ya kumzuia asifunge ndoa kanisani, leo sitazumgumzia madai yasiyo ya kiimani na yale ya kiimani nitakuwa makini katika uandishi kiasi kwamba itanilazimu kutumia maneno ya Kilatini au Kiingereza.

Uendeshaji wa mahakama duniani unahitaji ushahidi. Je, ushahidi kuhusu imani ya Kanisa Katoliki ni upi?

Ushauri wangu kwa wanasheria, wanahabari, wanasiasa na yeyote anayetaka kuielewa imani ya Kanisa Katoliki, basi walau awe na hivi vinne vifuatavyo: 1: Biblia, 2: Katekisimu ya Kanisa Katoliki, 3: Sheria za Kanisa 4: Hati za Mikutano Mikuu ya Maaskofu Duniani.

Ushahidi wa kwanza ni Biblia. Wa pili ni Katekisimu ya Kanisa Katoliki. Katekisimu ndiyo mafundisho rasmi ya Kanisa. Katekisimu ya kwanza ilichapishwa mwaka 1566, jina lake halisi lilikuwa "Katekisimu ya Mkutano wa Trent".

Kila jimbo duniani lilichukua mambo machache humo na kuchapisha Katekisimu nyingine ndogo zilizotafsiriwa kwenye lugha asili. Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere, alitafsiri Katekisimu katika lugha ya Kizanaki kuanzia Aprili 1955 hadi Oktoba 1955.

Baada ya miaka 446 yaani Oktoba 11, 1992, Katekisimu mpya ikazinduliwa huko Vatican ili isambazwe kote duniani. Katekism hii imeandikwa kwa vifungu kuanzia cha kwanza hadi cha 2854. Hii inaitwa "Katekisimu Kanisa Katoliki".

Ushahidi wa tatu ni hati za Mikutano ya Maaskofu wakiwa na Papa. Mkutano wa kwanza ulifanyika Jerusalem kama inavyoshuhudia Biblia {Matendo 15:1-21}. Hadi leo imeshafanyika mikutano 21. Mara ya mwisho ni ule uliofanyika Vatican mwaka 1962 hadi 1965 ukaitwa Vatican II.

Ushahidi wa nne ni Sheria za Kanisa yaani, uhusiano wa Wakatoliki duniani unaongozwa na sheria hizi. Mahakama za kesi za Kikanisa zimeelezwa ndani ya Sheria hizi kuanzia Kanuni ya 1419 hadi 1752.

Hizi ni aina nne tu za ushahidi unaoweza kutumika kuthibitisha linaloaminiwa na Kanisa Katoliki. Pia kuna mafundisho yaitwayo "Dogma". Novemba 1, 1950, Papa Pius XII alitangaza "Dogma", ifundishayo kwamba Bikira Maria yaani Mama wa Yesu alipalizwa mbinguni.

Hivyo, wingi wa ushahidi unaotakiwa unafanya kesi zinazohusu jambo la imani ni ngumu kuliko unavyoweza kudhani.

Mfano, ukiuliza swali kwamba, je, hili Kanisa linaitwaje? Wengi watakimbilia kutaja maneno "Roman Catholic Church" au "Kanisa Katoliki la Roma". Na wengine huwaita Wakatoliki kwa neno "Waroma". Je, kwa nini litajwe neno Roma wakati hatuko Italia?

Wapo watakaotaja tu "Kanisa Katoliki". Lakini, bado utata unaotokana na ukweli kwamba Kanisa Katoliki ni jumla ya makanisa 23 ndani yake yanayojiendesha yaani "sui juris".

Kanisa lenye waumini wengi ni hili mnalolijua wengi na linaitwa "Catholic Church Latin Rite". Maskofu wake ni hawa kina Polycarp Pengo (D'Salaam), Jude Thadaeus (Mwanza) na wenzao wote 34 hapa Tanzania.

Yale makanisa 22 yaliyobaki, licha ya kutamkwa kila moja kwa jina lake, pia yote kwa ujumla wao hutambulishwa kama "Eastern Catholic". Matano kati ya hayo ni Ethiopian, Armenian, Maronite, Coptic, Chaldean.

Baadhi ya maaskofu wao wakuu huitwa "Patriarch". Wakati majimbo yetu huitwa "Diocese", yao baadhi huitwa
"eparchy".

Je, kama Ukatoliki una makanisa 23 tofauti, je, ni lipi kati ya hayo hapa Tanzania, ambalo waumini wake wana haki ya kujitambulisha kwa maneno (Roman Catholic Church), (Catholic Church), (Mkatoliki)? Ukweli ni kwamba yote yale 23 yana haki hiyo.

Hakika, kwenye hati zinazotutaka kujaza dhehebu, basi tunatakiwa kutaja maneno "Catholic Church Latin Rite" wakati huo tukubaliane tafsiri ya maneno hayo kwa Kiswahili. Hata magazetini tunapaswa tuukumbatie usahihi huu.

Lakini pia, ukisoma Katekisimu, Sheria za Kanisa, Vatican II, hakuna hata sentensi moja inayotaja jina "Roman Catholic Church".

Hivyo, hakuna Kanisa linaloitwa "Roman Catholic Church" au kwa kifupi RC au "Kanisa Katoliki la Roma". Kwa hiyo, jina la Kanisa tu, linaweza kuwa kesi inayojitegemea mahakamani! Wangapi walikuwa wanalijua hili!

Tunapoandika makala huwa tunapata meseji nyingi za simu. Naweza kuulizwa, mbona tuna Sala iitwayo Sala ya Imani yenye sehemu isemayo "..nasadiki maneno yote linayosadiki, na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma.." {Misale ya Waumini, 2004, uk. 1078}.

Kwa kifupi jibu ni kwamba, vitabu vyetu Tanzania vizingatie marekebisho kama wenzetu wanavyozingatia duniani. Ukitaka kujua kwamba jina "Roman Catholic Church" lilipigwa marufuku na maaskofu tangu mwaka 1870 pitia tovuti hii {www.ewtn.com/faith/teachings/churb3.htm}.

Tuone kesi moja iliyoendeshwa na mabingwa wa sheria wa dunia hii huko Marekani. Kesi ambayo mwanasheria William McMurry aliwatetea watoto walionyanyaswa na mapadri.

Msingi wa kesi ile ilikuwa ni kwamba Papa ndiye anayeendesha Kanisa Katoliki duniani, ndiye anayeteua maaskofu. Anaposhindwa kumtimua askofu au padri mbovu, basi wa kuwajibishwa ni yeye mwenyewe Papa.

Wanasheria hao wakajiridhisha kwamba mfanyakazi wa Vatican au balozi zake akifanya uhalifu nchini Marekani, basi Papa anaweza kuitwa mahakamani.

Dunia ikatetemeka mwaka 2010 kuona kama Papa Benedict XVI ataingia mahakamani ili awajibishwe kwa uzembe na ikibidi ajiuzuru upapa.

Lakini wakili wa Vatican kwenye kesi ile, Edward Peters, aliwashinda Wamarekani hawa kwa hoja. Kwanza alikubaliana nao kwamba uzembe wa wafanyakazi wa Vatican na balozi zake hata kama ni maaskofu, unaweza kufanya ofisi ya Papa iwajibike.

Lakini Peters akaleta hoja kwamba kiimani Kanisa Katoliki haliwachukulii maaskofu kama wafanyakazi au waajiriwa au wasaidizi wa Papa. Wala maaskofu hawaongozi majimbo yao kama wawakilishi wa Papa, bali wanayaendesha kwa mamlaka yao kamili.

Ushahidi aliotumia Peters ni hati ya Mkutano wa Vatican (Vatican II). Hati iitwayo Lumen Gentium (LG). Ibara ya 27 ya hati hii inatamka kwamba askofu ndiye msaidizi na mwakilishi wa Yesu katika eneo lake.

Ukiisoma ibara hicho (LG27), utaona kwamba Kanisa linalosimamiwa na askofu huitwa "Particular Church". Kwa Kiswahili hutafsiriwa kama "Kanisa Mahalia" japo wengi hupenda kutumia neno "Diocese" au "Jimbo".

Hivi ndivyo vigezo vya kiimani vilivyoimaliza kesi ile. Ni dhahiri wataalamu wale wa sheria huko Marekani waliaibika mbele ya uso wa dunia kwamba wamezidiwa uelewa na wanasheria wa Vatican.

Sasa, tujadili na tuone kama huduma za Kanisa zinaweza kuwekewa pingamizi. Kanisa lina utaratibu wake wa kutunza rekodi ya muumini kadiri anavyoendelea kupata huduma za kiroho.

Huduma ya kwanza kabisa unayoweza kuipata ni Ubatizo ndipo zifuate zingine sita zifuatazo: Kitubio, Ekaristi, Kipaimara, Ndoa, Daraja (upadri), Mpako wa Wagonjwa. Huduma zote hizi saba huitwa Sakramenti.

Kanisa lina wajibu wa kumlinda asiye na kizuizi, asizuiwe kuipata huduma yoyote kati ya hizo kwani ni huduma za Mungu, na huduma ya Mungu haizuiwi na mamlaka za kibinadamu.

Tujiulize. Hivi hata mahakama za dunia hii zingepewa mamlaka kuzuia mtu asipate Sakramenti hizi, hivi zuio hilo lingetekelezwa vipi? Tuchambue kidogo ugumu wa kuizuia Sakramenti moja baada ya nyingine.

Kanuni ya 861(2) ya Sheria za Kanisa Katoliki inaonyesha kwamba Mwislamu mwenye nia njema anaruhusiwa kumbatiza mtu aliye katika hatari ya kufa kwa ubatizo wa Kikatoliki. Je, mamlaka zitazuiaje ubatizo wa aina hii unaoweza kutokea popote duniani inapoweza kutokea hatari ya kifo?

Marehemu bibi yangu alipofika umri wa kutoweza kwenda kanisani, ulifanywa utaratibu mapadri wakawa wanakuja kumpa Ekaristi pale nyumbani.

Sasa, utazuiaje Sakramenti ya Ekaristi asipelekewe Mkatoliki kama kweli amenuia kuipata na si lazima mumuone ameingia kanisani?

Kwa mtindo huohuo, ndivyo unaweza kupata Sakramenti za Kitubio au Mpako wa Wagonjwa ikawa siri yako na padri au askofu na mwingine asijue.

Ukardinali siyo Sakramenti. Lakini Askofu Ignatius Kung Pin-mei wa Shanghai , China, alipewa ukardinali wa siri uitwao "Cardinal in pectore" Juni 30, 1979 wakati hana habari, tena akiwa gerezani akitumikia kifungo kutoka serikali ya China iliyokuwa haiutaki Ukatoliki nchini humo.

Kwa ujumla, kwa sakramenti zote zile saba na huduma zozote za kiimani, haishindikani kuzifanya kwa siri kama kufanyika kwake hadharani kunaonekana dhahiri kutaleta mtafaruku unaotokana na kutoielewa imani Katoliki.

Sasa, ndoa yaani moja ya Sakramenti zile saba, waumini yaani wawili wameihitaji, iweje Kanisa liache kazi lililotumwa na Mungu na liwazuie huduma hiyo, kwa sababu tu kuna moja ya mahakama za dunia hii, imezuia kwa vigezo vyake wala si vigezo vya Kanisa Katoliki?

Hivi, hata parokia moja ikizuiwa kwa nguvu kutoifungisha ndoa fulani, je, hiyo nguvu itawezaje kuzuia maaskofu wote duniani kuwaita wanandoa hao kwenye nchi zao na kuwafungisha ndoa huko nje?

Uadhimishaji wa Sakramenti ya ndoa, padri au askofu huwa anabaki kama shahidi tu kwani wanaoiadhimisha ni wafunga ndoa wenyewe. Sasa hapa atakamatwa nani kwa kukaidi zuio la mamlaka?

Ukweli ni kwamba, mahakama hazipaswi na haziwezi kuweka au kutekeleza zuio kwa binadamu asipate moja ya Sakramenti zile saba ikiwemo ya ndoa.

Wapo watakaohoji, sasa hiyo ndoa itasajiliwa wapi kama ina zuio la mahakama hata kama imebarikiwa kanisani?

Ukisoma Sheria za Kanisa, yaani {Can. 895, 1054, 1122(1)} utaona kwamba Sakramenti za Kanisa Katoliki zinasajiliwa kwenye orodha iitwayo "Baptismal Register". Sakramenti ya kwanza kujazwa huwa ni Ubatizo.

Unavyozidi kupata huduma nyingine ndivyo orodha hii inavyoongezeka. Ukipata usista, orodha inarekebishwa. Ukifa orodha hii inaongezwa tarehe uliyokufa.

Orodha hii hutunzwa kanisani na Mkatoliki hupewa nakala yake kwenye cheti kiitwacho "Kitambulisho Cha Ukatoliki". Wengi hukiita "Cheti Cha Ubatizo".

Orodha ya namna hii imesaidia watafiti wengi duniani kujua rekodi za watu na matukio ya miaka ya mwanzo sana ambako hata elimu ilikuwa haijaenea.

Hivyo, cheti cha ndoa cha kiserikali hakina msaada mkubwa kikanisa kwani vyeti hivi vimekuja baada ya dola nyingi kuzaliwa au kupata uhuru wakati utaratibu huu wa Kikatoliki una muda zaidi ya miaka 1500.

KanisaKatoliki duniani, halilazimiki kumzuia mtu asifunge ndoa kama yeye na mwenzake hawataona faida wala haja ya kuwa hicho na cheti cha ndoa.

Inapotokea kwamba Mkatoliki yeye binafsi hahitaji cheti cha ndoa, basi huyo ameridhika kwamba mashauri yake ya ndoa atayamaliza kwenye Mahakama ya Kanisa ambayo Jaji wa kwanza ni askofu wake na Jaji Mkuu ni Papa.

Tanzania tuna matangazo ya kondomu tu na sheria zinaruhusu talaka. Hatujafika hatua ya kuruhusu haki za ushoga, usagaji na utoaji mimba.

Kanisa Katoliki linajua na wote tunajua kwamba, Mkatoliki yeyote duniani, mwenye kesi inayohusu talaka, ushoga, usagaji, utoaji mimba, kamwe hawezi kuthubutu kupeleka kesi ya namna hiyo kwenye Mahakama ya Kanisa.

Hivyo, cheti cha ndoa kinaweza kumsaidia Mkatoliki pale tu atakapokihitaji akitumie kwa masuala ya ndoa yanayotambuliwa na serikali ya nchi anayoishi.

Juni 10, 2011 iliripotiwa kwamba, ilitoka amri ya kuzuia kusimikwa uaskofu katika Kanisa la Anglican huko Kilimanjaro. Pamoja na amri ile, ibada ya kuwekwa wakfu askofu ikaendelea. Askofu Dk. Valentino Mokiwa alipoulizwa kuhusu hati ya kumkamata kwa kukaidi zuio lile, alijibu "...njooni mnikamate...".

Papa John Paul II, alizoea kuwaita mapadri na kuwapa uaskofu hukohuko Vatican kila Januari 6. Katika rekodi aliyoweka ya kutoa Daraja la Uaskofu kwa watu 327, saba kati yao ni Watanzania wafuatao: Aloyce Balina, Norbert Mtega, Justine Samba, Tarcisius Ngalalekumtwa, Polycarp Pengo, Paul Ruzoka na Bruno Ngonyani.

Alichokifanya John Paul II kwa hawa Watanzania ni sawa na alichokifanya Askofu Mokiwa na baadaye akatamka ".. njooni mnikamate..". Wote Askofu Mokiwa na Papa John Paul II walifanya kitendo cha kutoa Sakramenti kwa Mtanzania. Kiimani ni kitendo kilicho juu ya mamlaka za duniani.





--- On Mon, 8/6/12, gm26may@gmail.com <gm26may@gmail.com> wrote:

From: gm26may@gmail.com <gm26may@gmail.com>
Subject: Re: [wanabidii] Re: NDOA YA DR SLAA ILIFANYIKA?
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Monday, August 6, 2012, 3:34 AM


Mke wa kwanza alikuwa hajafunga naye ndoa ya Kikatoliki!

Just 4 ua info
Sent from my BlackBerry® smartphone on the Tigo Tanzania Network

From: Edgar Sakaya <sakaya.edgar@gmail.com>
Sender: wanabidii@googlegroups.com
Date: Mon, 6 Aug 2012 13:30:19 +0300
To: <wanabidii@googlegroups.com>
ReplyTo: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Re: [wanabidii] Re: NDOA YA DR SLAA ILIFANYIKA?

Nadhani hiyo ni kwa Regional Commissioner

On Mon, Aug 6, 2012 at 1:23 PM, Dahlia Majid <dahliamajid@yahoo.com> wrote:
 
Heeee!
Kikatoriki, Kikristo 'inaswihi?'
what a shame...?!!!

From: denis Matanda <denis.matanda@gmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, August 6, 2012 2:06 AM
Subject: Re: [wanabidii] Re: NDOA YA DR SLAA ILIFANYIKA?

gm26may alitoa mrejesho humu ndani kuwa lile zuio lilitupiliwa mbali na mzee slaa akajivutia jiko kwenye tarehe ile iliyopangwa!

On Mon, Aug 6, 2012 at 10:49 AM, morphine <eddymak9@gmail.com> wrote:
mhh sidhani si kulikua na pingamizi la mahakama nahisi.


On Monday, August 6, 2012 8:06:59 AM UTC+3, Jonas Kiwia wrote:
Naomba kuuliza kama,hii ndoa ilifungwa?

Regards,
 
Jonas Kiwia  |  Director
Speedy Computers
Tel:+255 754882825  |  Cell: +255 715882825
P.O.Box: 55133  |  Dar esSalaam  |  Tanzania
Email:jonaskiwia39@gmail.com  URL:www.speedycomputersonline.com
 
    

--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
mailto:wanabidii%2Bunsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Wasalaam
 
Denis Matanda,
Mine Supt,
Nzega - Tanzania.
 
" Low aim, not failure, is a crime"

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment