Tuesday 21 August 2012

Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa

On Aug 21, 8:14 pm, denis Matanda <denis.mata...@gmail.com> wrote:
> Samaki wanachinjwa?
> On 21 Aug 2012 19:04, "rashid martin" <rashi...@hotmail.com> wrote:
>
>
>
>
>
>
>
>
>
> > kwangu sili nguruwe sababu na feel pinch sana maana hachinjwi anabondwa na
> > shoka kichwani, this touches alot my heart and my mind
> > it is maltreatment to animal, na mungu nahisi hapendi
> > ------------------------------
> > From: hil...@ira.udsm.ac.tz
> > To: wanabidii@googlegroups.com
> > Subject: Subject: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata
> > kifafa
> > Date: Tue, 21 Aug 2012 17:22:23 +0300
>
> > Kuhusu uhusiano wa nyama ya nguruwe na tegu na kifafa, jambo hili inafaa
> > lichunguzwe kwa makini. Nguruwe alitunzwa vizuri hawezi kuwa na hicho
> > inachokiita tegu na kisha kumuambukiza mulaji na kupata matezi kwenye
> > ubongo na kisha kupata kifafa. Jambo la kuepuka hapa ni kuhukumu
> > (Nyabenda).
>
> > Angalia picha attached uone jinsi baadhi ya minyoo inavyoweza kumuingia
> > mnyama kutokana na chakula alacho au kama atatembea katika mazingira yenye
> > uchafuzi.Na mnyama anaweka minyoo katika udongo kwa kupitia mwili wake au
> > kinyesi chake. Huweka uchafuzi katika maji na hata ktk mboga za majani
> > minyoo ikamuingia binadamu. Licha hiyo ya nyama isiyopikwa ikaliwa
> > haijaiva, kuna maambukizi ya aina nyingi na minyoo ya aina nyingi mibaya
> > sio hiyo tu ya nguruwe. Baadhi ya nguruwe wafugwao huachiwa huru (Mfano ni
> > kijiji cha Laela -Sumbawanga.Kukiwa na mikutano ya kitaifa au kiwilaya
> > wanavijiji huambiwa wafungie nguruwe wao siku hiyo ya mkutano. Tuzingatie
> > kukosha vyakula na vipikwe viive.
>
> > Aliyeongea juu ya Tapeworm na nguruwe na kifafa nami nikamsapoti hakukosea
> > alisema suala zuri la ukweli la kuzingatiwa kwa afya zetu. Wengi pia
> > wametoa hoja muhimu. Nyabenga ameonyesha hapo juu kuwa nguruwe wakitunzwa
> > vizuri nyama haina matatizo. Lakini kwa uhakika pika iive. Pia, sio wote
> > walao nyama ya nguruwe wamewafuga wao wenyewe na kuhakikisha usafi ktk
> > matunzo.Wengi hununua na hawatojua matunzo ya mnyama huyo huko alikotoka.
>
> > Hata hivyo-pamoja na kuwa nguruwe haliwi na baadhi ya madhehebu, ni mnyama
> > wa mafao sana. Utafiti wa kisayansi kwa wenzetu umegundua kuwa akipata
> > mafunzo ni mnyama hodari wa kunusa hata cocaine iliyofichwa na ni mnyama
> > pekee aliyoonekana kuwa kama akiwekewa damu ya binadamu anaweza kutumika
> > katika blood bank. Akiwekewa viungo vya binadamu na hiyo damu anakuwa mtu
> > nguruwe na ukaweza kuhabishia baadhi ya viungo kwa watu wenye shida mfano
> > figo, ini kusaidia utata kwa wasioweza kupata msaada au kugharimia kwa bei
> > kubwa kuvinunua. PIG, anaweza pia akatumika kama atumikavyo mbwa ktk
> > kusindikiza vipofu. Hii ina utata. Sijui kwa madhehebu mengine kukubali
> > kupanda naye katika bus la abiria au ndege akiwa ni msindikizaji kipofu. Na
> > sijui itakuwaje kama mtoa figo wako ndio huyo Pig nawe huna mwingine
> > wakukupa na umebakiza siku chache figo yako itaishia na damu ya aina yako
> > haipo hospitali bali itolewe ilikotengenezwa kwa kundi la wahisani hao pig
> > na  mnyama huyo kwako ni najis. Itakuwa kama wakati ule wa ubaguzi S.Afrika
> > ambapo hutokea mtu mweusi akatoa figo kumpa mweupe (kwa hiari au nguvu)
> > wakati kimaisha walikuwa hata kiti jirani au mtaa hapakaliki.
>
> > Ifahamike pia wapo wale ambao hawachinji na kula nyama mpaka mnyama afe au
> > wanavizia mfugo umekufa wanakatakata na kupiga au kuuza kwa watu wataumiza
> > walaji. Suala la mfugo kutunzwa vizuri si hoja hapa, hitaji ni usalama wa
> > nyama na lazima isafishwe vyema, ipikwe iive ili uwe na uhakika. Maana hata
> > wanunuao nyama buchani, gulioni au kula nyama iliyochomwa bar sio hao
> > wafugao mnyama husika. Wengi ni wanunuzi tu hata hao nguruwe.
>
> > Kukataa ukweli ni kuongeza tatizo kama yatufikayo katika kutoa dawa za
> > kuzuia na kutibu NTDs (neglected diseases) nyingi na magonjwa mengi ya
> > minyoo mfano Usubi ambao vimnyoo nyake hunogewa kula mboni za macho;
> > matende na mabusha, kichocho, minyoo ya kamba, mduara, hydatit disease
> > itokayo kwa mbwa,   na minyoo ya tepe (tapeworm).Vurugu hutokea wanafunzi
> > wapewapo dawa mashuleni wakati wa deworming program za mpango wa afya
> > mashuleni TZ. Pia, kukataa kula dawa watu wazima zile za matende kwa
> > kuhofia masuala yasiyo kweli. Imani na kutokukubali kuelimishwa kuhusu
> > maradhi na kudhania dawa zipo kuvunja uzazi (Bush-Obama plans.) ni tatizo.
> > Mwenzetu katuelimisha kuhusu minyoo inavyoweza kuleta kifafa tusikatae ni
> > kweli.Nenda google uangalie madhara ya tapeworm unaweza ukapata taarifa.
>
> > Mnyama anamuambukiza binadamu maradhi hata minyoo na binadamu kuambukiza
> > mnyama kupitia njia mbali mbali pia (kinyesi katika maji, udongo, chakula
> > cha mifugo. Unapomwaga zebaki (mercury)ktk kuchekesha dhahabu na maji yake
> > akanywa mnyama-unajimaliza nawe pia ulapo nyama yake na maziwa ya mfugo
> > huyo. Hata gono lilitoka kwa mnyama likaja kwa binadamu.Haya ni maambukizo
> > machache tu yapo mengi. Kiroboto na papasi wa ng'ombe/mbwa wanaambukiza
> > magongwa ya homa kali lakini papasi anasababisha kupooza kiungo akiuma na
> > kutoa ute kwa mtoto wa binadamu chini ya umri fulani. Na kipindi hiki mwaka
> > huu, viroboto vya mbwa/ng'ombe vimezagaa vinapanda kuta za nyumba na
> > kusumbua imekuwa kama wamemwagwa. Pamoja na climate change minyoo hata ya
> > tepe hiyo nguruwe itasumbua mno na kuzagaa.Na bado mingine haijaibuliwa na
> > climate change ianze kumalizawatu kama gonjwala ebola. Ni majuzi tu
> > wanasayansi wamegundua minyoo kutoka ndani ya mwili wa Paka isababishayo
> > kichaa kwa binadamu ikiingia sehemu ndani ya ubongo wa binadamu. Hapa
> > binadamu hachinjwi akapikwa ila mnyoo wa paka unammaliza.
>
> > Minyoo ikizidi hutoka ktk maeneo yake ya maskani ipendapo kukaa ndani ya
> > binadamu na kuzagaa na kuharibu maini, mfumo wa neva, uti wa mgongo na
> > ubongo au kuziba mishipa ya damu na mingine kupasua hata utumbo (ona
> > kiambata). Serikali katika vertical program ya school health hutoa dawa
> > zinazotibu minyoo yote mara moja kwa mwaka kwa wanafunzi shule za msingi
> > ili kupunguza athari hizi. Huu ni mpango chini ya WHO na mashirika mengine
> > yanayosaidia na GVT ina mfumo maalum kutoka wizara ya afya, Mkoa, Wilaya,
> > Kata, kijiji na shule.Utaahira mwingine na upungufu wa damu na matatizo
> > mengine huletwa na minyoo ambayo ni mamilioni ktk mazingira yetu ya uchafu.
>
> > Bwana afya mkaguzi wa nyama anatakiwa aikague aone ishara na magonjwa
> > fulani mabaya katika nyama kupitia matezi ktk nyama au utumbo, rangi ya
> > maini yake, etc kuona dalili za magonjwa Zoonotic. Hata hivyo kama
> > walivyosema wengine-anakagua chache sio zote ambazo nyingine huuzwa mtaani
> > hazikaguliwi. Twaona ktk TV wengine huuza nyama na supu ya mbwa, nyama
> > zilizooza, machinjio machafu. Sasa usipopika ikaiva sio utapata minyoo tu
> > na maradhi mengine.
>
> > Na mara nyingi wachomaji nyama ukimwambia bado choma iive anaona usumbufu
> > unampotezea mudawa wateja wengine anasema hii tayari imeiva kumbe bado
> > mbichi utapata mnyoo mbaya.
>
> > Kawaida yetu wabongo kubishia wataalamu watufundishavyo na ndio maana hata
> > kesi za kunywa gongo na kupofuka au kufa zinatokea na zinaendelea pamoja na
> > mifano yake mibaya.
>
> > Tujiulize na kuangalia pia toka nyama au mboga (kabichi,mboga za
> > majani) tunda (embe, nanasi), nafaka, maharage etc yalipotoka kwa
> > mkulima-yamepitia mtandao gani? kukanyangwa na maviatu machafu ya wabeba
> > mizigo huku wakipenga kamasi, kujikuna ukurutu na kushika mboga, matunda,
> > nyama etc. Kulalia mizigo hiyo nyuma ya gari na magwanda yao machafu, viatu
> > vilivyoganyaka uchafu na kinyesi porini mashambani. Uchafuzi wa vyakula
> > hivyo hadi kutua sokoni Tandale, Kariakoo (ambako nako kuchafu)hadi
> > utakapoinunua mtaani imepagwa na vumbi la makohozi ya TB na uchafu
> > mwingine. Na hapo butchani (km ni nyama) fashion ni kuning'iniza nyama wazi
> > kutwa ionekane sio kuifungia ktk kabati la usalama inzi wasilambe.juu hadi
> > hapo jikoni itakapoangushwa na housegirl asiyezingatia misingi ya afya
> > unapokuwa haupo anafanya atakavyo jikoni.
>
> > PIKA NYAMA IIVE, kosha matunda sana kwa maji mengi na suuza mara ya mwisho
> > angalau kwa maji ya uvuguvugu kama sio ya moto.Zingatia usafi wa vyombo na
> > mikono na hivyo vitambaa vya kufutia vyombo utaona cha meza hicho hicho
> > kupangusia, kupangusa mikono na kukaushia vyombo hicho
> > hivyo.Tatizo-matumbo, kukohoa hakuishi. Tuzingatie kanuni za usafi kitabia,
> > kwa chakula salama na mazingira safi.
>
> > Kiwasila
>
> > *From:* Nyabenda Juma <jng...@yahoo.co.uk>
> > *To:* khildega...@yahoo.co.uk; wanabidii@googlegroups.com
> > *Sent:* Monday, 20 August 2012, 10:35
> > *Subject:* Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa
>
> > Kuhusu uhusiano wa nyama ya nguruwe na tegu na kifafa, jambo hili inafaa
> > lichunguzwe kwa makini. Nguruwe alitunzwa vizuri hawezi kuwa na hicho
> > inachokiita tegu na kisha kumuambukiza mulaji na kupata matezi kwenye
> > ubongo na kisha kupata kifafa. Jambo la kuepuka hapa ni kuhukumu kwa ujumla
> > kuwa kula nyama ya nguruwe kunasababisha kupata kifafa. Nguruwe anayepata
> > dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu hawezi kuwa na hiyo minyoo katika
> > mwili wake. Nakubaliana na hoja kuwa binadamu anapopata madhara kwa kula
> > nyama ya nguruwe ni pale tu ambapo nguruwe hakufugwa kitaalam na kupewa
> > matunzo sahihi.
>
> > ----------
> > Sent via Nokia Email
>
> > ------Original message------
> > From: Hildegarda Kiwasila <khildega...@yahoo.co.uk>
> > To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
> > Date: Sunday, August 19, 2012 5:01:40 PM GMT+0100
> > Subject: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa
>
> > *From:* achengula <acheng...@gmail.com>
> > *To:* "khildega...@yahoo.co.uk" <khildega...@yahoo.co.uk>; "
> > wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>; "
> > jng...@yahoo.co.uk" <jng...@yahoo.co.uk>
> > *Sent:* Monday, 20 August 2012, 10:56
> > *Subject:*
>
> ...
>
> read more »

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment