Monday 20 August 2012

Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa

Kuhusu uhusiano wa nyama ya nguruwe na tegu na kifafa, jambo hili inafaa lichunguzwe kwa makini. Nguruwe alitunzwa vizuri hawezi kuwa na hicho inachokiita tegu na kisha kumuambukiza mulaji na kupata matezi kwenye ubongo na kisha kupata kifafa. Jambo la kuepuka hapa ni kuhukumu kwa ujumla kuwa kula nyama ya nguruwe kunasababisha kupata kifafa. Nguruwe anayepata dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu hawezi kuwa na hiyo minyoo katika mwili wake. Nakubaliana na hoja kuwa binadamu anapopata madhara kwa kula nyama ya nguruwe ni pale tu ambapo nguruwe hakufugwa kitaalam na kupewa matunzo sahihi.

----------
Sent via Nokia Email

------Original message------
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, August 19, 2012 5:01:40 PM GMT+0100
Subject: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa

Ni kweli kabisa nyama ya nguruwe isiyopikwa vizuri minyoo ya tegu inaweza kukuletea kifafa kutokana na matezi inayotengeneza katika ubongo inayoathiri mishipa ya fahamu (nerves). Ila, watu ni wabishi kukubali. Data ya kijiji kimoja milimani Morogoro ilionyesha kupanda kwa kifafa baada ya kuanzisha ufugaji wa nguruwe ktk kuongeza kipato cha wananchi. Nyama inauzwa vibaya sana vilabuni. Licha ya kuwapatia fedha, imewapatia maradhi.
 
Pia, wale wafanyao kazi za fumigation, kupaka rangi, treatment ya mbao na hao wa saluni za akina mama na baba wanakopaka dawa za kubadili nywele. Hawavai protective gear. mafundi utawaona wanapuliza rangi za magari; au za katika ujenzi kupaka rangi; sprays za madawa saluni ambapo hafungi pua anavuta hewa ndani. hao nao baadhi yao wakija kuumwa magonjwa ya kushindwa kupumua au ya kifafa-wanatafuta mchawi. Huku anapuliza madawa au rangi anaongea, anavuta sigara. Bado hao ambao hupiga madawa mashambani kwa kutumia babomba huku havai kuziba mdomo wala pua au miwani. au wa melini na fumigation kisha amekaa humo ndani anavuta na sigara. hao baadhi hupata kifafa.
 
Bado hawa ktk jamii ambao hutumia dawa za mbu na za aina nyingine kupiga ktk kabeji na mboga nyingine ambapo dawa hizo si za matumizi hao bali hutumia kuua wadudu.Tunakula madawa unakuja kuumwa maradhi yasiyojulikana. Wengine huiba mboga na matunda yaliyopigwa madawa ya kilimo ambayo yanasema-usivune na kula mpaka baada ya wiki au wiki 2 za kupiga dawa. Lakini vibaka huja kuiba mboga, matunda au mnyama aliyepigwa dawa kabla ya muda kuisha na kuuza nyama au matunda keshoyake. Haya huingia sokoni na kuliwa na watu halafu kuanza kuugua pumu na magonjwa mengine ya mfumo wa hewa. Kwa jinsi wabongo tulivyo na dharau, hivi vyakula vya kununua migahawani ya kukaangia mafuta ya transfoma za umeme, maziwa wanachemshwa na kuwekwa katika chupa za plastiki yakiwa yamoto na unaiona imejikunja; ugali unapikwa ili uwe wa moto unatiwa katika mfuko wa plastiki hizi za madukani na kuwekwa katika sururia liwekwalo ktk sufuria lingine la maji ya moto na kupewa mteja ale wa
moto. Plastiki nyingine huyeyuka na kuingia ktk ugali na ni sumu mwilini hazipo kwa kupashia moto vyakula. Tunapunguza umri wa kuishi, kuleta kansa na kusababisha vizazi vyt vilema fulani kwa kutokuzingatia misingi ya afya.Ukijaribu kumuelekeza mtu unapomkuta hakuvaa protective gear, anapaka madawa makali ya kubadili nywele mtu havai gloves anamsugua kwa vidole tupu na makucha hata kama gloves zipo anaona zinamchelewesha ufanisi, havai. Kusemasema anakuona kama kero, unajidai atakufa anyway maana maradhi yapo mengi.
 
Mungu atusaidie. Haya ni ya nyongeza ya kumegeana mkate.


________________________________
From: Mashaka Mgeta <mgeta2000@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, 19 August 2012, 16:48
Subject: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa


Ni angalizo zuri INGAWA inawezekana ikawa rahisi kuvumilia maumivu yanayotokana na kuchomwa kwa ncha ya sindano kwenye mboni ya jicho kuliko kuacha kukitumia kitoweo hicho.

Ni mtazamo tu
------------------------------
On Sat, Aug 18, 2012 7:21 AM PDT Augustino Chengula wrote:

>Kwa wale wanofuga nguruwe, wanaokula kiti moto lakini na wale
>wasiohusika na lolote kati ya hayo bado wanaweza kupata ugonjwa
>unatokana na minyoo wanaoitwa tegu (tapeworm) unaoweza kukupelekea
>kuwa na kifafa. Kwa muda mrefu watu wameamini ndugu zao wenye kifafa
>wamelogwa au wameurithi, wengi hawajajua kuwa unaweza kupata ugonjwa
>wa kifafa kwa kula nyama ya nguruwe ikiwa mbichi au haijapikwa vizuri
>(kitimoto jina maarufu nyakati hizi za sasa) yenye lava wa tegu.
>Lakini pia kula mboga za majani zisizooshwa vizuri au kupikwa vizuri.
>Kwa kujielimisha zaidi soma hapa http://achengula.blogspot.com/
>--
>
>
>
>
>*To all the questions of your life YOU are the  most possible answer. To
>all the problems of your life YOU are the best solution. Trust yourself*
>
>--
>Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
>Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
>Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment