Sunday 19 August 2012

Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa

Ndugu yangu Achengula umefanya vizuri kutuelimisha kuhusu swala zima
la madhara ya kula nyama ya nguruwe isipopikwa vizuri. Elimu ya
vyakula ni pana sana na hivyo kwa watu wa kawaida ni vyema kuijua
kiujumla. Swala la kuhakikisha nyama inapikwa vyema linahusu nyama za
aina zote (ya ng'ombe, mbuzi, kondoo, sungura, nguruwe, nyama pori nk)
nyama zote zinauwezekano wa kuwa na minyoo ya aina mbalimbali ikiwemo
tegu(tapeworm) pia wapo bacteria na amoeba hatari (harmful organisms)
wa aina nyingi.

Hapa nina maana kwamba inabidi tuelewe kwamba kabla ya kula nyama au
vyakula vingine ni budi tujihakikishie kama vimepikwa kwa moto na kwa
muda wa kutosha. Vyakula kama mboga za majani na matunda viwe
vimesafishwa barabara kwa maji yaliyo safi na salama. Tunatakiwa pia
kuelewa kama vimelimwa sehemu salama ambako hakuna sumu(poisonous
chemicals).

Kwa wenzetu Ulaya na Amerika elimu kuhusu nini unakula inatolewa kwa
msisitizo na kwa kila mtoto na hivyo wanaitoa kupitia masomo kama Home
Economics na mengine. Kwetu hapa msisitizo hatuna na badala yake
tunaangalia masomo kama tulivyoyaridhi toka kwa mkoloni(mathematics,
physics, chemistry, biology, history, geography, english nk). Siyo
kwamba masomo hayo hayana umuhimu ila umuhimu wake unaongezeka sana
tunapotumia maarifa ya masomo hayo kwenye maisha ya kila siku. Umefika
wakati wa kuangalia applications ya elimu tunayowapa wanafunzi wetu.
Kwamba wakimaliza elimu mfano ya msingi au sekondari wataonyesha
tofauti gani katika maisha yao ya kila siku (katika kujali
wanachokula, kulima, kufanya biashara, ushiriki katika mambo yote ya
kijamii, kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa na kimaendeleo kwa ujumla

Siku zote utasikia watu wakisema uridhi mzuri tunaotakiwa kuwaachia
watoto wetu ni ELIMU japo wengi elimu wanayokuwa wakisema ni ile ya
kumpeleka mtoto shule akasome traditional subjects kama history,
hesabu, geography, biology nk bila kujua kwamba ata yeye mwenyewe ni
mwalimu wa kutoa elimu kwa mwanae. Kwanza kwa kuwa mfano bora kwa
watoto wake na wa jirani ili watoto waweze kumuiga mzazi baadaye,
kumsaidia kusoma masomo, kumpa mahitaji muhimu ya shule, kumfundisha
maadili na ata kuhusika kutoa mawazo yake shuleni yatakayosaidia
walimu pamoja na serikali kutoa elimu bora. Ni wazazi wachache
wanaowajibika katika nyanja hizi na badala yake utasikia wakilalamika
elimu imeshuka, watoto wa siku hizi hawana adabu nk bila kujua kwamba
wao ni wahusika wakubwa katika uotaji elimu isiyokidhi haja.

Ni sisi wazazi tunaokwenda kwenye bar na kula kitomoto ambayo hatujui
kama imepimwa au la na pia mapishi yake pia haujui. Yote hiyo ni
kuishi kwa mazoea tu. Ninaamini huko tuendako mfumo mzima wa elimu
utabadilika na hivyo watu tunakuwa macho na tunachokula na vyuo
vinavyofundisha uduma za bar na hotel vitakuwa vimezalisha wahudumu wa
kutosha ili huduma bora iweze kupatikana sehemu nyingi za bar na
hotel. Swali moja la kizushi hivi ndugu Chengula kwa nini umetoa hoja
hii siku ya EID MUBARAKA?

Nawatakia EID njema wote

2012/8/18 Augustino Chengula <achengula@gmail.com>:
> Kwa wale wanofuga nguruwe, wanaokula kiti moto lakini na wale
> wasiohusika na lolote kati ya hayo bado wanaweza kupata ugonjwa
> unatokana na minyoo wanaoitwa tegu (tapeworm) unaoweza kukupelekea
> kuwa na kifafa. Kwa muda mrefu watu wameamini ndugu zao wenye kifafa
> wamelogwa au wameurithi, wengi hawajajua kuwa unaweza kupata ugonjwa
> wa kifafa kwa kula nyama ya nguruwe ikiwa mbichi au haijapikwa vizuri
> (kitimoto jina maarufu nyakati hizi za sasa) yenye lava wa tegu.
> Lakini pia kula mboga za majani zisizooshwa vizuri au kupikwa vizuri.
> Kwa kujielimisha zaidi soma hapa http://achengula.blogspot.com/
> --
>
>
>
>
> *To all the questions of your life YOU are the most possible answer. To
> all the problems of your life YOU are the best solution. Trust yourself*
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment