Monday 6 August 2012

Re: [wanabidii] Fw: Re:WABUNGE KUJADILI MIFUKO YA JAMII NSSF/PPF

Provident Funds za Tanzania ni scheme zinazolenga kumuibia mfanyakazi.
Kama hiyo haitoshi,mfanyakazi ameongezewa mzigo mwingine - SSRA.
Michango ya mfanyakazi ndio inalipa mishahara minono ya wafanyakazi wa
SSRA

On 8/6/12, Pius Makomelelo <makomelelopius@yahoo.co.uk> wrote:
> haraka haraka ninavyoona tutaanza kukatwa perecent fulani kuchangia
> uendeshaji wa SSRA kila mwezi kutoka kwenye mafao yetu!
>
>
> From: mutabaazi lugaziya <mjlugaziya@mail.com>
> To: wanabidii@googlegroups.com
> Sent: Monday, 6 August 2012, 15:07
> Subject: [wanabidii] Fw: Re:WABUNGE KUJADILI MIFUKO YA JAMII NSSF/PPF
>
>
>
>
>
>
> ----- Original Message -----
>>From: mutabaazi lugaziya
>>Sent: 08/04/12 04:15 PM
>>To: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>>Subject: Re: [Mabadiliko] Wabunge kujadili MIFUKO YA JAMII NSSF/PPF kesho
>>
>>
>>
>>
>>
>>-Kwa Waheshimiwa Wabunge wote mliomo humu,wanamabadiliko wengine na wadau
>> wote!
>>>
>>>Kusema kuwa sheria hii ni mbaya, ni "gross understatement.!!"
>>>
>>>Sheria hii, kipengele kinachozuia mafao ya kujitoa, ni wizi wa mchana,
>>> inakiuka haki ya kikatiba ya mtu kumiliki na kutawala mali yake.
>>>
>>>Kwa kuanzia, tunalazimishwa, kwa mujibu wa sheria, kuwa wanachama wa
>>> mifuko hii. Hela tunazochanga kule ni mali yetu binafsi, ambazo kwa
>>> mujibu wa haki za asili na za kikatiba, hakuna mtu anayeweza kutuzuia
>>> kuzichukua, tunapozihitaji. Ni kama vile tumeweka hela benki.
>>>
>>>Pili, wakati mtu anaingia kwenye mifuko hii, mkataba wake na tambo za
>>> mifuko hii, ilikuwa kwamba mfanyakazi husika, atakapojitoa atakuwa na
>>> haki ya kuchukua mafao yake kipindi hicho. Pamoja na kuwepo na sheria ya
>>> kulazimisha kujiunga na mifuko hii, ukweli kwamba unaahidiwa uhuru wa
>>> kuchukua fedha zako ni moja ya vishawishi. Kubadili kipengele kama hicho,
>>> ni kubadilisha mkataba bila ridhaa ya mmoja wa wahusika wa mkataba, a.k.a
>>> mfanyakazi. Sheria ya mikataba(Law of Contract Act) na maamuzi mbali
>>> mbali ya mahakama ya rufaa na ile iliyokuwa ya Afrika Mashariki, yanasema
>>> mikataba ni "sacrosanct", yaani ni vitu ambavyo vina hadhi ambayo haiwezi
>>> kuchezewa. Mbona kwenye "uamuzi wa Dowans" serikali yetu hii hii na Jaji
>>> Werema huyu huyu alisema eti "tunabanwa na mkataba kuheshimu maamuzi ya
>>> mahakama ya usuluhishi wa kimataifa? Kwani hawajui, au wametugeuza
>>> mazoba?
>>>
>>>Kumekuwepo na hisia kwamba hiyo ni janja kwa sababu ama mifuko iko katika
>>> hati hati ya kufilisika, au serikali yenyewe inazihitaji fedha hizi kwa
>>> sababu zake anuai.
>>>
>>>Kwa namna serikali inavyochota fedha za mifuko hii, kwa nini isipate shida
>>> katika uendeshaji? Kwa kukumbushia tu, mifuko hii imeikopesha fedha zetu
>>> serikali kwa ajili ya mambo mbali mbali. Lililo zaidi, ni ujenzi wa Chuo
>>> Kikuu cha Dodoma. NSSF(234.1bn/=), PSPF(105.9bn/=). PPF(39.99bn/=),
>>> LAPF(22bn/=), NHIF(13.4/=). Na huo ni mradi mmoja tu! Kufuatia wimbi
>>> kubwa la wanaostaafu, fedha chekwa hizi haiyumkiniki zitamalizika, huku
>>> serikali ikiwa haina hata mpango wa kulipa fedha hiyo. Waswahili wengi,
>>> hata kama ana biashara ya kukopa hawezi kupata shida, hata kama hana
>>> hela, atachota humo kwenye biashara. Si zake?
>>>
>>>Hivi kazi ya "Regulatory Authority" ni nini? Hiki kinachoitwa SSRA na huyo
>>> mdada mremboCEO wake, kazi yao ni nini? Regulatory Authority anasimamia
>>> makampuni au taasisi zilizowekwa chini yake ili kampuni hizo au taasisi
>>> hizo:
>>>
>>>1.Zisiwanyanyase wateja wanaopata huduma zake.
>>>
>>>2.Zitoe huduma bora.
>>>
>>>3. Zisinyanyaswe na mamlaka za serikali.
>>>
>>>Kwa kuwa kuna mifuko mingi ya jamii, Mamlaka hii kazi yake ya kwanza
>>> ingekuwa kuhakikisha kuwa kuna a "level playing field" kwa watoa huduma
>>> hao na watumiaji huduma hizo. Hii ingekuwa, kwa mfano, kuweka ukomo
>>> "ceiling" ya kiasi cha pesa ambazo mfuko unaweza kutumia kufanya
>>> investment, badala ya utaratibu wa sasa ambao jamaa wakiamua tu, utasikia
>>> wanajenga sijui nyumba za viega uchumi, sijui za bei nafuu etc.
>>>
>>>Kwa kushirikiana na pande zote, mamlaka hii ingefikiria namna ya
>>> wachangiaji wanavyoweza kurejeshewa hela zao na riba juu.
>>>
>>>Au kushauri kama kuna haja ya kuwa na utitiri huu wa mifuko, na uwezekano
>>> wa kuanzishwa kwa mifuko ya binafsi, ambapo hapo sasa ndiyo SSRA ingekuwa
>>> na manufaa zaidi. Hili la ku-regulate mifuko ya Serikali ni ghilba tu.
>>>
>>>Kwa hali ilivyo, SSRA ni mzigo mwingine kwa walipa kodi. Ingawa hatujajua
>>> huko mbeleni kutakuwa na nini, lakini kwa namna lilivyoanza, SSRA ni
>>> janga kama mengine.
>>>
>>>Nitarudi baadae!
>>>
>>>Wenu mwaminifu,
>>>
>>>MJL
>>>
>>>
>> --
>>Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
>>Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
>>
>>Kujiondoa Tuma Email kwenda;
>> mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com
>>Utapokea Email ya kudhibitisha kujiondoa kwako.
>>
>>TEMBELEA Facebook yetu:
>>http://www.facebook.com/MabadilikoForums?ref=hl
>>
>>For more options, visit this group at:
>>http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
>>
>>
>>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
> --
> Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
> Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
> Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>
>

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

0 comments:

Post a Comment