Tuesday 14 August 2012

RE: [wanabidii] Fw: JAJI WARIOBA MNAVUNA MLICHOPANDA

Bwana Matinyi,
Nakubaliana na wewe kwamba kimsingi, (licha ya kwamba nao ni wadau) viongozi wa dini hawapaswi kujiingiza moja kwa moja katika harakati ambazo kimsingi ni za kisiasa.
Huo ni upande mmoja. Lakini, upande wa pili, ni kwamba wanasiasa nao hawapaswi kubeba ajenda ambazo kimsingi ni za kidini.
Ukishafumbia macho suala la serikali, vyama vya siasa au wanasiasa mmoja mmoja kubeba ajenda ambazo moja kwa moja ni za kidini, huwezi kuwaondoa viongozi wa dini kwa namna yoyote ile katika masuala ambayo moja kwa moja ni ya kisiasa.
 

From: matinyi@hotmail.com
To: wanabidii@googlegroups.com
CC: abdulugone@yahoo.com; hudaeditor@hotmail.com; ammychekanae@yahoo.com; bkimwanga@yahoo.com; mhariri@habarileo.co.tz; nkizitto@mwananchi.co.tz; majira@majira.co.tz; kimesha07@yahoo.com; mkingamkinga@yahoo.com; mobinsons@yahoo.com; muhibu72@yahoo.co.uk; nipashe_gazeti@hotmail.com; minnalove40@yahoo.com; salimli2006@yahoo.co.uk; tzdaima@freemedia.co.tz; news@thecitizen.co.tz; lipumba@yahoo.com; juliusmtatiro@yahoo.com; jussa29@hotmail.com; jussa30@hotmail.com; abu_zahir1945@yahoo.com
Subject: RE: [wanabidii] Fw: JAJI WARIOBA MNAVUNA MLICHOPANDA
Date: Tue, 14 Aug 2012 12:27:39 +0000

Watanzania wenzangu,
 
Kuhusu vyama vya siasa na asasi za kiraia sina tatizo lakini kuhusu viongozi wa dini na ghasia zao zote napinga mno ushiriki wao kwenye kila aina ya shughuli ya kisiasa kuanzia na huu mchakatio wa kuelekea kwenye katiba mpya. Dini zikae mbali na siasa. Dini ni sumu kwa mustakabali wa taifa lolote, siyo Tanzania tu, labda kama watu wanakubaliana kwamba wawe na taifa la kidini. Hakuna kutumia akili kwenye dini - watu wanaweza kufanya mambo yasiyofaa kwa sababu tu kiongozi wa dini (binadamu mdhambi kama wao) amewaambia hivyo kwa kusingizia sauti ya Mungu. Kwenye jamii ya watu kama siye wenye njaa na tusiokuwa na elimu ama upeo mkubwa, ni hatari mno kuachia viongozi wa dini na asasi zao kuwa na sauti. Hili si jambo la kufanyia mchezo wala mzaha - dini ni suala la mtu binafsi na libaki huko ndani ya moyo wa kila mtu na familia yake.
 
Mobhare Matinyi.
 

Date: Tue, 14 Aug 2012 03:37:17 -0700
From: mobinsons@yahoo.com
Subject: [wanabidii] Fw: JAJI WARIOBA MNAVUNA MLICHOPANDA
To: wanabidii@googlegroups.com


----- Forwarded Message -----
From: abdulrahman Lugone <abdulugone@yahoo.com>
To: Alhuda <hudaeditor@hotmail.com>; Amina Chekanae <ammychekanae@yahoo.com>; Bakari Kimwanga <bkimwanga@yahoo.com>; Habarileo <mhariri@habarileo.co.tz>; Kizitto Noya <nkizitto@mwananchi.co.tz>; majira <majira@majira.co.tz>; Meshack Kitunzi <kimesha07@yahoo.com>; Mkinga Mkinga <mkingamkinga@yahoo.com>; mobini sarya <mobinsons@yahoo.com>; Muhibu Said <muhibu72@yahoo.co.uk>; nipashe <nipashe_gazeti@hotmail.com>; Rabia Bakari <minnalove40@yahoo.com>; Salim Said <salimli2006@yahoo.co.uk>; Tanzania Daima <tzdaima@freemedia.co.tz>; The Citizen <news@thecitizen.co.tz>
Cc: Ibrahim Haruna Lipumba <lipumba@yahoo.com>; Julius Mtatiro <juliusmtatiro@yahoo.com>; Jussa Ladhu <jussa29@hotmail.com>; Jussa Ladhu <jussa30@hotmail.com>; Salim Bimani <abu_zahir1945@yahoo.com>
Sent: Friday, August 10, 2012 4:34 PM
Subject: Fw: JAJI WARIOBA MNAVUNA MLICHOPANDA



--- On Fri, 8/10/12, Jumuiya Vijana <juvicuf@yahoo.com> wrote:

From: Jumuiya Vijana <juvicuf@yahoo.com>
Subject: Fw: JAJI WARIOBA MNAVUNA MLICHOPANDA
To: abdulugone@yahoo.com
Date: Friday, August 10, 2012, 7:36 AM



--- On Fri, 8/10/12, Jumuiya Vijana <juvicuf@yahoo.com> wrote:

From: Jumuiya Vijana <juvicuf@yahoo.com>
Subject: JAJI WARIOBA MNAVUNA MLICHOPANDA
To: ismaelygodfrey@gmail.com, "Majira Editor" <bteditor@btl.co.tz>, jamboleonewspaper@yahoo.com, "MWANANCHI MHANDO MWANANCHI MHANDO" <aidanmhando@yahoo.com>, "Mtanzania News papers" <mtanzania@newshabari.com>, mtanzania95@yahoo.co.uk, "Dailynews Tanzania" <newsdesk@dailynews-tsn.com>, "maulid ahmed" <mauahmed@yahoo.com>, "HABARI LEO KAMPUNI" <habarileo@dailynews-tsn.com>, "JULIUS MTATIRO" <juliusmtatiro@yahoo.com>, "Ismail Jussa" <jussa30@hotmail.com>, juvicuf@yahoo.com
Date: Friday, August 10, 2012, 4:12 AM

Taarifa kwa vyombo vya Habari
JAJI WARIOBA ACHA KULALAMIKA MNAVUNA MLICHOPANDA
Imetolewa na Shaweji Mketo,
Naibu Mkurugenzi Mipango, Uchaguzi na Bunge
Agosti 10, 2012
CUF – Chama cha Wananchi tumesikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ya kuwataka Viongozi wa vyama vya siasa, asasi za kiraia, vikundi vya kidini na wanaharakati kutowafundisha wananchi maoni ya kuchangia kwenye mikutano ya Tume.
Jaji Warioba aliyasema hayo Jijini Dar es salaam jana alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari kwa lengo la kuwapatia mrejesho wa mikutano iliyofanywa na tume yake kwa kipindi cha mwezi mzima katika mikoa minane, alifafanua kuwa vyama vya siasa vimekuwa vikitoa kauli na maelekezo kwa wanachama wao ili wafuate misimamo ya vyama, jambo ambalo linawanyima uhuru wa kutoa maoni yao.
CUF – Tunalaani lengo baya la siri walililokuwa nalo Tume hiyo ya kuratibu maoni la kutarajia kuwakuta wananchi wanaochangia ni mambumbu wasiojua lolote kwa makusudi, na hili linathibitishwa kwa kudharau ushauri tulioipa Tume hiyo ya kuwataka kutoa elimu ya Katiba kwa Wananchi kabla ya kuanza zoezi la kukusanya maoni hayo.
CUF – Tunawapongeza na kuwashukuru Viongozi wa Vyama vya siasa,Taasisi mbambali zilizojitolea kutoa elimu ya Katiba kwa wanachama wao na wananchi wengine ili angalau kuwa na uelewa juu ya mapungufu na mazuri yaliyomo ndani ya katiba iliyopo kabla ya kuchangia maoni kwa Katiba mpya ijayo.
Ni muhimu Jaji Waioba akatambua kuwa vyama vya siasa moja ya jukumu lake ni kujenga ushawishi kwa wananchi ili wapate kuungwa mkono kwa lengo la kukamata dola. Kwa kuwa Katiba itakayopatikana itakuwa mwongozo kwa vyama vyote kwa ujumla lakini ikiwa ndiyo dira kuu kwa chama kitakachopata mamlaka ya kuongoza nchi ni jambo lisilo epukika kwa vyama kujiweka kando na mchakato huo mbele ya wananchi wanaotarajia kuwapa ridhaa.
Inatia mashaka zaidi ikiwa Tume inatambua na inahimiza maoni ya taasisi mbalimbali kuhusu mabadiliko ya Katiba hii, iweje leo anasema haipaswi kwa vyama kuwashawishi wananchi juu utoaji wa maoni ya Katiba? Au vyama inaongoza akina nani, kwani Jaji anataka katiba iwe na mambo gani pekee ambayo yanaweza kuharibiwa na vyama?
Hatutoacha kuwaelekeza wadau wetu juu ya mapungufu na mazuri yaliyomo katika Katiba na yanayohitajika kuwemo katika Katiba mpya kwa mustakabali mwema wa Taifa letu.
HAKI SAWA KWA WOTE
Kwa mawasiliano zaidi 0716 226642/0718 717364
Taarifa kwa vyombo vya Habari
IGP DHIBITI JESHI LAKO LA USALAMA WA BARABARANI LITAMALIZA WANANCHI
Imetolewa na Abdul Kambaya,
Naibu Mkurugenzi Habari, Uenezi na Haki za Binadamu,
Agosti 10, 2012
 
CUF – Chama cha Wananchi tumepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za ajali za barabara zinazoendelea kutokea mara kwa mara hapa nchini, ikiwemo ajali iliyotokea juzi eneo la Kitunda, wilayani Sikonge mkoani Tabora ambapo basi la Sabena lilipinduka na kuua watu 17 na wengine 78 kujeruhiwa.
Basi hilo aina ya Scania lenye namba ya usajili T 570 AAM, lililokuwa likitokea Tabora kwenda Mbeya, na kwa mujibu wa vyombo vya Habari vilivyohoji baadhi ya abiria waliosalimika katika ajali hiyo, walisema kuwa basi hilo lilikuwa limebeba zaidi ya abiria 110 na dereva wa basi hilo alikuwa akiendesha kwa mwendo kasi, licha ya abiria kulalamika kwa Polisi wa Usalama barabarani ambao nao hawakujali, dereva wa basi hilo aliendelea kuendesha kwa mwendo kasi hadi lilipomshinda na kupindukua.
CUF – Chama cha Wananchi tunamtaka IGP Said Mwema kulikagua jeshi lake la Polisi, hususan kitengo cha usalama barabarani, ambapo uzembe umekithiri na kuna kila dalili ya rushwa kushamiri katika kitengo hicho, kuwawajibisha vinginevyo yeye mwenyewe awajibike kwa maafa ya wananchi yanayoendelea kutokea siku hadi siku ambayo yanaweza kuepukika, ili hali hizi ni nguvu kazi za Taifa.
CUF – Tunawasihi madereva kutambua kuwa mwendo kasi unamaliza binadamu wenzao na  wengine kupata ulemavu wa kudumu, ukiachia wale wanaoteseka kwa maumivu makali hospitalini.  Lakini pia tunawapa pole wale waliojeruhiwa na kumuomba Mwenyezi Mungu awape ahueni mapema na kuwataka wale wote waliopoteza ndugu na jamaa zao kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, AMIN!!!
 
HAKI SAWA KWA WOTE
 
Kwa mawasiliano zaidi 0718 717364/0719 566567
 
 



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment