Monday 27 August 2012

Re: [wanabidii] Eti CHADEMA kama TANU ?

Leila naomba nichangie moja pengine kujaribu kuweka historia sawia: TANU hakikuungana na chama chochote cha ushindani ama upinzani, ASP ni habari tofauti kabisa maana kilikuwa chama tawala pia kwa upande wa Zanzibar. TANU pia ndicho kilichoielekeza serikali kupiga marufuku vyama vingine vyovyote kuogopa ushindani na upinzani na kuifanya Tanzania kuwa na mfumo wa CHAMA KIMOJA Chenye kushika Utamu (waliita hatamu).
Ahsante.

From: Leila Abdul <hifadhi@gmail.com>
To: wanaBidii <wanaBidii@googlegroups.com>
Sent: Monday, August 27, 2012 6:09 PM
Subject: [wanabidii] Eti CHADEMA kama TANU ?

Ukipitia vyombo vya habari kama magazeti na Mitandao ya kijamii wako watu wanaofananisha CHADEMA na TANU .

Mi nahoji hivi ni kweli jamani ? kwani TANU waliwahi kufanya maandamano popote nchini kudai Uhuru ?

TANU walikubali kufa kwa ajili ya Kuungana na ASP ili kuwa na CCM   Haiwezi kulinganishwa na CHADEMA inayoogopa kuungana na vyama vya upinzani ili kupata nguvu .

TANU haijawahi kutuhumiwa kwa ukabila wala dini hata na serikali ya kikoloni .
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 


0 comments:

Post a Comment