Monday 20 August 2012

Re: [wanabidii] DEMOKRASIA!!!!!!!!

asante mheshimiwa kwa shairi,lazima tujikumbushe asili yetu.

--- On Tue, 6/12/12, Dr Peter D Kafumu <kafumu@yahoo.com> wrote:

From: Dr Peter D Kafumu <kafumu@yahoo.com>
Subject: [wanabidii] DEMOKRASIA!!!!!!!!
To: wanabidii@googlegroups.com
Date: Tuesday, June 12, 2012, 1:46 PM

Wanabidii,
 
Ni siku nyingi kweli, nimeingia mitini nawapongezaa kwa mijadala yenye mizania.
Nawaletea Ushairi wa Ng'wizukulushilinde ambayo ni tafakari kuhusu madhara ya hii demokrasia ya kimagharibi katika nchi masikini. haya endelea....
 
 

DEMOKRASIA!!!!!!!!

 

1.         Tamaduni za mwafrika, ujamaa asilia,

Jamiini twasifika, siasa zilotulia,

Mfumo gawanyi fika, kutokea uropia,

Mfumo wa vyama vingi, mfumo hatarishi.

 

2.      Hapa kwetu Tanzania, vyama vingi ni maafa,

Umoja wetu vyaua, kuligawanya Taifa,

Mfumo demokrasia, unaoleta maafa,

Mfumo wa vyama vingi, mfumo hatarishi.

 

3.      Vyama vingi shabikia, vurugu na utengano,

Sakama na singizia, kurushiana maneno,

Vinazidi kutupia, matusi masengenyano,

Mfumo wa vyama vingi, mfumo hatarishi.

 

4.      Vyombo vya habari pia, vyashabiki utengano,

Wananchi wanashangaa, kuwepo mafarakano,

Watahayari sawia, kuwepo kwa mapigano,

Mfumo wa vyama vingi, mfumo hatarishi.

 

5.      Enyi ndugu waungwana, dhana demokrasia,

Ni sisi kuchaguana, madaraka kupokea,

Utawala achiana, tukitunza Tanzania,

Mfumo wa vyama vingi, mfumo hatarishi.

 

6.      Vyama hivi vingi nchini, ni demokrasia mpya,

Wananchi shirikini, kwenye itikadi mpya,

Kupeana usukani, na kuanza mambo upya,

Mfumo wa vyama vingi, mfumo hatarishi.

 

7.      Tuanze vumiliana, kuanza katika vyama,

Watu bila kupigana, viongozi kusimama,

Pasipo kubaguana, siasa ziwe za dhima,

Mfumo wa vyama vingi, mfumo hatarishi.

 

8.      Tuache kutukanana, tuonyane kwa staha,

Bila kusingiziana, tutafikia furaha,

Siasa kutukanana, haileti kamwe siha,

Mfumo wa vyama vingi, mfumo hatarishi.

 

9.      Viongozi nawasihi, hamasisheni amani,

Tumieni tasibihi, raia wafundisheni,

Kufanya siasa sahihi, kwa upendo na amani,

Mfumo wa vyama vingi, mfumo hatarishi.

 

1 .  Mola atawahukumu, viongozi fitinishi,

Uacheni udhalimu, na maneno hatarishi,

Kuchochea kwa hatamu, na kuleta kashikashi,

Mfumo wa vyama vingi, mfumo hatarishi.

 

1  .  Kumbukeni kwa makini, maneno yao wahenga,

Kwa upanga hatamuni, taondoka kwa upanga,

Tafuteni kwa amani, tawaleni kwa kukinga,

Mfumo wa vyama vingi, mfumo hatarishi.

 

1  .  Tamati nimefikia, viongozi kumbukeni,

Mfumo demokrasia, usiondoe amani,

Vyama vya kushindania, bila vurugu na kani,

Mfumo wa vyama vingi, mfumo hatarishi.

   

DPK (Ng'wizukulushilinde)

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment