Wednesday 22 August 2012

RE: Subject: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa

no nimeleza hisia zangu kwa mheshimiwa nguruwe,namuonea huruma sana,thats why siri
hata ivo nazipenda sana precepts za imani ya kibiddha (budhism)ukimuona jinsi anavo andaliwa dah,usinishawishi

 

Date: Wed, 22 Aug 2012 01:15:02 -0700
From: ipyana75@yahoo.com
Subject: Re: Subject: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa
To: wanabidii@googlegroups.com

Rashid my Braza;
You are still leaving kwa "HISIA"???
Badilika fasta mana hujachelewa.
 Reuben
From: rashid martin <rashidtz@hotmail.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Tuesday, August 21, 2012 9:04 AM
Subject: RE: Subject: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa


kwangu sili nguruwe sababu na feel pinch sana maana hachinjwi anabondwa na shoka kichwani, this touches alot my heart and my mind
it is maltreatment to animal, na mungu nahisi hapendi
From: hildak@ira.udsm.ac.tz
To: wanabidii@googlegroups.com
Subject: Subject: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa
Date: Tue, 21 Aug 2012 17:22:23 +0300

Kuhusu uhusiano wa nyama ya nguruwe na tegu na kifafa, jambo hili inafaa lichunguzwe kwa makini. Nguruwe alitunzwa vizuri hawezi kuwa na hicho inachokiita tegu na kisha kumuambukiza mulaji na kupata matezi kwenye ubongo na kisha kupata kifafa. Jambo la kuepuka hapa ni kuhukumu (Nyabenda).
 
Angalia picha attached uone jinsi baadhi ya minyoo inavyoweza kumuingia mnyama kutokana na chakula alacho au kama atatembea katika mazingira yenye uchafuzi.Na mnyama anaweka minyoo katika udongo kwa kupitia mwili wake au kinyesi chake. Huweka uchafuzi katika maji na hata ktk mboga za majani minyoo ikamuingia binadamu. Licha hiyo ya nyama isiyopikwa ikaliwa haijaiva, kuna maambukizi ya aina nyingi na minyoo ya aina nyingi mibaya sio hiyo tu ya nguruwe. Baadhi ya nguruwe wafugwao huachiwa huru (Mfano ni kijiji cha Laela -Sumbawanga.Kukiwa na mikutano ya kitaifa au kiwilaya wanavijiji huambiwa wafungie nguruwe wao siku hiyo ya mkutano. Tuzingatie kukosha vyakula na vipikwe viive.
 
Aliyeongea juu ya Tapeworm na nguruwe na kifafa nami nikamsapoti hakukosea alisema suala zuri la ukweli la kuzingatiwa kwa afya zetu. Wengi pia wametoa hoja muhimu. Nyabenga ameonyesha hapo juu kuwa nguruwe wakitunzwa vizuri nyama haina matatizo. Lakini kwa uhakika pika iive. Pia, sio wote walao nyama ya nguruwe wamewafuga wao wenyewe na kuhakikisha usafi ktk matunzo.Wengi hununua na hawatojua matunzo ya mnyama huyo huko alikotoka.
 
Hata hivyo-pamoja na kuwa nguruwe haliwi na baadhi ya madhehebu, ni mnyama wa mafao sana. Utafiti wa kisayansi kwa wenzetu umegundua kuwa akipata mafunzo ni mnyama hodari wa kunusa hata cocaine iliyofichwa na ni mnyama pekee aliyoonekana kuwa kama akiwekewa damu ya binadamu anaweza kutumika katika blood bank. Akiwekewa viungo vya binadamu na hiyo damu anakuwa mtu nguruwe na ukaweza kuhabishia baadhi ya viungo kwa watu wenye shida mfano figo, ini kusaidia utata kwa wasioweza kupata msaada au kugharimia kwa bei kubwa kuvinunua. PIG, anaweza pia akatumika kama atumikavyo mbwa ktk kusindikiza vipofu. Hii ina utata. Sijui kwa madhehebu mengine kukubali kupanda naye katika bus la abiria au ndege akiwa ni msindikizaji kipofu. Na sijui itakuwaje kama mtoa figo wako ndio huyo Pig nawe huna mwingine wakukupa na umebakiza siku chache figo yako itaishia na damu ya aina yako haipo hospitali bali itolewe ilikotengenezwa kwa kundi la wahisani hao pig na  mnyama huyo kwako ni najis. Itakuwa kama wakati ule wa ubaguzi S.Afrika ambapo hutokea mtu mweusi akatoa figo kumpa mweupe (kwa hiari au nguvu) wakati kimaisha walikuwa hata kiti jirani au mtaa hapakaliki.
 
Ifahamike pia wapo wale ambao hawachinji na kula nyama mpaka mnyama afe au wanavizia mfugo umekufa wanakatakata na kupiga au kuuza kwa watu wataumiza walaji. Suala la mfugo kutunzwa vizuri si hoja hapa, hitaji ni usalama wa nyama na lazima isafishwe vyema, ipikwe iive ili uwe na uhakika. Maana hata wanunuao nyama buchani, gulioni au kula nyama iliyochomwa bar sio hao wafugao mnyama husika. Wengi ni wanunuzi tu hata hao nguruwe.
 
Kukataa ukweli ni kuongeza tatizo kama yatufikayo katika kutoa dawa za kuzuia na kutibu NTDs (neglected diseases) nyingi na magonjwa mengi ya minyoo mfano Usubi ambao vimnyoo nyake hunogewa kula mboni za macho; matende na mabusha, kichocho, minyoo ya kamba, mduara, hydatit disease itokayo kwa mbwa,   na minyoo ya tepe (tapeworm).Vurugu hutokea wanafunzi wapewapo dawa mashuleni wakati wa deworming program za mpango wa afya mashuleni TZ. Pia, kukataa kula dawa watu wazima zile za matende kwa kuhofia masuala yasiyo kweli. Imani na kutokukubali kuelimishwa kuhusu maradhi na kudhania dawa zipo kuvunja uzazi (Bush-Obama plans.) ni tatizo. Mwenzetu katuelimisha kuhusu minyoo inavyoweza kuleta kifafa tusikatae ni kweli.Nenda google uangalie madhara ya tapeworm unaweza ukapata taarifa.
 
Mnyama anamuambukiza binadamu maradhi hata minyoo na binadamu kuambukiza mnyama kupitia njia mbali mbali pia (kinyesi katika maji, udongo, chakula cha mifugo. Unapomwaga zebaki (mercury)ktk kuchekesha dhahabu na maji yake akanywa mnyama-unajimaliza nawe pia ulapo nyama yake na maziwa ya mfugo huyo. Hata gono lilitoka kwa mnyama likaja kwa binadamu.Haya ni maambukizo machache tu yapo mengi. Kiroboto na papasi wa ng'ombe/mbwa wanaambukiza magongwa ya homa kali lakini papasi anasababisha kupooza kiungo akiuma na kutoa ute kwa mtoto wa binadamu chini ya umri fulani. Na kipindi hiki mwaka huu, viroboto vya mbwa/ng'ombe vimezagaa vinapanda kuta za nyumba na kusumbua imekuwa kama wamemwagwa. Pamoja na climate change minyoo hata ya tepe hiyo nguruwe itasumbua mno na kuzagaa.Na bado mingine haijaibuliwa na climate change ianze kumalizawatu kama gonjwala ebola. Ni majuzi tu wanasayansi wamegundua minyoo kutoka ndani ya mwili wa Paka isababishayo kichaa kwa binadamu ikiingia sehemu ndani ya ubongo wa binadamu. Hapa binadamu hachinjwi akapikwa ila mnyoo wa paka unammaliza.
 
Minyoo ikizidi hutoka ktk maeneo yake ya maskani ipendapo kukaa ndani ya binadamu na kuzagaa na kuharibu maini, mfumo wa neva, uti wa mgongo na ubongo au kuziba mishipa ya damu na mingine kupasua hata utumbo (ona kiambata). Serikali katika vertical program ya school health hutoa dawa zinazotibu minyoo yote mara moja kwa mwaka kwa wanafunzi shule za msingi ili kupunguza athari hizi. Huu ni mpango chini ya WHO na mashirika mengine yanayosaidia na GVT ina mfumo maalum kutoka wizara ya afya, Mkoa, Wilaya, Kata, kijiji na shule.Utaahira mwingine na upungufu wa damu na matatizo mengine huletwa na minyoo ambayo ni mamilioni ktk mazingira yetu ya uchafu.
 
Bwana afya mkaguzi wa nyama anatakiwa aikague aone ishara na magonjwa fulani mabaya katika nyama kupitia matezi ktk nyama au utumbo, rangi ya maini yake, etc kuona dalili za magonjwa Zoonotic. Hata hivyo kama walivyosema wengine-anakagua chache sio zote ambazo nyingine huuzwa mtaani hazikaguliwi. Twaona ktk TV wengine huuza nyama na supu ya mbwa, nyama zilizooza, machinjio machafu. Sasa usipopika ikaiva sio utapata minyoo tu na maradhi mengine.
 
Na mara nyingi wachomaji nyama ukimwambia bado choma iive anaona usumbufu unampotezea mudawa wateja wengine anasema hii tayari imeiva kumbe bado mbichi utapata mnyoo mbaya.
 
Kawaida yetu wabongo kubishia wataalamu watufundishavyo na ndio maana hata kesi za kunywa gongo na kupofuka au kufa zinatokea na zinaendelea pamoja na mifano yake mibaya.
 
Tujiulize na kuangalia pia toka nyama au mboga (kabichi,mboga za majani) tunda (embe, nanasi), nafaka, maharage etc yalipotoka kwa mkulima-yamepitia mtandao gani? kukanyangwa na maviatu machafu ya wabeba mizigo huku wakipenga kamasi, kujikuna ukurutu na kushika mboga, matunda, nyama etc. Kulalia mizigo hiyo nyuma ya gari na magwanda yao machafu, viatu vilivyoganyaka uchafu na kinyesi porini mashambani. Uchafuzi wa vyakula hivyo hadi kutua sokoni Tandale, Kariakoo (ambako nako kuchafu)hadi utakapoinunua mtaani imepagwa na vumbi la makohozi ya TB na uchafu mwingine. Na hapo butchani (km ni nyama) fashion ni kuning'iniza nyama wazi kutwa ionekane sio kuifungia ktk kabati la usalama inzi wasilambe.juu hadi hapo jikoni itakapoangushwa na housegirl asiyezingatia misingi ya afya unapokuwa haupo anafanya atakavyo jikoni.
 
PIKA NYAMA IIVE, kosha matunda sana kwa maji mengi na suuza mara ya mwisho angalau kwa maji ya uvuguvugu kama sio ya moto.Zingatia usafi wa vyombo na mikono na hivyo vitambaa vya kufutia vyombo utaona cha meza hicho hicho kupangusia, kupangusa mikono na kukaushia vyombo hicho hivyo.Tatizo-matumbo, kukohoa hakuishi. Tuzingatie kanuni za usafi kitabia, kwa chakula salama na mazingira safi.
 
Kiwasila
 
 
 
From: Nyabenda Juma <jngama@yahoo.co.uk>
To: khildegarda@yahoo.co.uk; wanabidii@googlegroups.com
Sent: Monday, 20 August 2012, 10:35
Subject: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa

Kuhusu uhusiano wa nyama ya nguruwe na tegu na kifafa, jambo hili inafaa lichunguzwe kwa makini. Nguruwe alitunzwa vizuri hawezi kuwa na hicho inachokiita tegu na kisha kumuambukiza mulaji na kupata matezi kwenye ubongo na kisha kupata kifafa. Jambo la kuepuka hapa ni kuhukumu kwa ujumla kuwa kula nyama ya nguruwe kunasababisha kupata kifafa. Nguruwe anayepata dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu hawezi kuwa na hiyo minyoo katika mwili wake. Nakubaliana na hoja kuwa binadamu anapopata madhara kwa kula nyama ya nguruwe ni pale tu ambapo nguruwe hakufugwa kitaalam na kupewa matunzo sahihi.

----------
Sent via Nokia Email

------Original message------
From: Hildegarda Kiwasila <
khildegarda@yahoo.co.uk>
To: "
wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, August 19, 2012 5:01:40 PM GMT+0100
Subject: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa






 
From: achengula <achengula@gmail.com>
To: "khildegarda@yahoo.co.uk" <khildegarda@yahoo.co.uk>; "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>; "jngama@yahoo.co.uk" <jngama@yahoo.co.uk>
Sent: Monday, 20 August 2012, 10:56
Subject: RE: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa
 
Ndugu Nyabena,
Tahadhari ni lazima kuchukuliwa na haina maana nguruwe wote wana tegu, la hasha. Lakini haiharalishi kutopika nyama vizuri, mbali na ugonjwa yapo magonjwa mengine ambayo unaweza kupata. Mlaji una uhakika gani kuwa huyu nguruwe alikuwa anatunzwa kwa utaratibu unaotakiwa, amepimwa na mtaalamu wa mifugo kwa kuangalia nyama? Tuwe makini tu hasa kwa nchi yetu ambapo mambo mengi yanachakachuliwa. Mfanyabiashara ni pesa tu, angalia mtu anapima nguruwe mmoja au wawili lakini anauza hata watano wasiopimwa, wewe ,laji utajuaje? Tunapozungumza rushwa au kukosekana kwa maadili Tanzania tusisahau hata upande huu nao ni watanzania wale wale yanaweza kujitokeza. Tuache ubishi bali tufuate kanuni za usafi, tunawe mikono yetu mara baada ya kutoka chooni, kabla ya kuandaa vyakula (kitimoto pia), mboga za majani zioshwe vizuri bila kusahau kupika kwa ustadi. Hii ni tahadhari lakini pia yamewakuta wenzetu hata kama wewe bado. Acha ubishi.

 On 20/08/2012 10:35:05, Nyabenda Juma Wrote on Gmail(jngama@yahoo.co.uk):
Kuhusu uhusiano wa nyama ya nguruwe na tegu na kifafa, jambo hili inafaa lichunguzwe kwa makini. Nguruwe alitunzwa vizuri hawezi kuwa na hicho inachokiita tegu na kisha kumuambukiza mulaji na kupata matezi kwenye ubongo na kisha kupata kifafa. Jambo la kuepuka hapa ni kuhukumu kwa ujumla kuwa kula nyama ya nguruwe kunasababisha kupata kifafa. Nguruwe anayepata dawa ya minyoo kila baada ya miezi mitatu hawezi kuwa na hiyo minyoo katika mwili wake. Nakubaliana na hoja kuwa binadamu anapopata madhara kwa kula nyama ya nguruwe ni pale tu ambapo nguruwe hakufugwa kitaalam na kupewa matunzo sahihi.

----------
Sent via Nokia Email

------Original message------
From: Hildegarda Kiwasila <khildegarda@yahoo.co.uk>
To: "wanabidii@googlegroups.com" <wanabidii@googlegroups.com>
Date: Sunday, August 19, 2012 5:01:40 PM GMT+0100
Subject: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa

Ni kweli kabisa nyama ya nguruwe isiyopikwa vizuri minyoo ya tegu inaweza kukuletea kifafa kutokana na matezi inayotengeneza katika ubongo inayoathiri mishipa ya fahamu (nerves). Ila, watu ni wabishi kukubali. Data ya kijiji kimoja milimani Morogoro ilionyesha kupanda kwa kifafa baada ya kuanzisha ufugaji wa nguruwe ktk kuongeza kipato cha wananchi. Nyama inauzwa vibaya sana vilabuni. Licha ya kuwapatia fedha, imewapatia maradhi.
 
Pia, wale wafanyao kazi za fumigation, kupaka rangi, treatment ya mbao na hao wa saluni za akina mama na baba wanakopaka dawa za kubadili nywele. Hawavai protective gear. mafundi utawaona wanapuliza rangi za magari; au za katika ujenzi kupaka rangi; sprays za madawa saluni ambapo hafungi pua anavuta hewa ndani. hao nao baadhi yao wakija kuumwa magonjwa ya kushindwa kupumua au ya kifafa-wanatafuta mchawi. Huku anapuliza madawa au rangi anaongea, anavuta sigara. Bado hao ambao hupiga madawa mashambani kwa kutumia babomba huku havai kuziba mdomo wala pua au miwani. au wa melini na fumigation kisha amekaa humo ndani anavuta na sigara. hao baadhi hupata kifafa.
 
Bado hawa ktk jamii ambao hutumia dawa za mbu na za aina nyingine kupiga ktk kabeji na mboga nyingine ambapo dawa hizo si za matumizi hao bali hutumia kuua wadudu.Tunakula madawa unakuja kuumwa maradhi yasiyojulikana. Wengine huiba mboga na matunda yaliyopigwa madawa ya kilimo ambayo yanasema-usivune na kula mpaka baada ya wiki au wiki 2 za kupiga dawa. Lakini vibaka huja kuiba mboga, matunda au mnyama aliyepigwa dawa kabla ya muda kuisha na kuuza nyama au matunda keshoyake. Haya huingia sokoni na kuliwa na watu halafu kuanza kuugua pumu na magonjwa mengine ya mfumo wa hewa. Kwa jinsi wabongo tulivyo na dharau, hivi vyakula vya kununua migahawani ya kukaangia mafuta ya transfoma za umeme, maziwa wanachemshwa na kuwekwa katika chupa za plastiki yakiwa yamoto na unaiona imejikunja; ugali unapikwa ili uwe wa moto unatiwa katika mfuko wa plastiki hizi za madukani na kuwekwa katika sururia liwekwalo ktk sufuria lingine la maji ya moto na kupewa mteja ale wa
moto. Plastiki nyingine huyeyuka na kuingia ktk ugali na ni sumu mwilini hazipo kwa kupashia moto vyakula. Tunapunguza umri wa kuishi, kuleta kansa na kusababisha vizazi vyt vilema fulani kwa kutokuzingatia misingi ya afya.Ukijaribu kumuelekeza mtu unapomkuta hakuvaa protective gear, anapaka madawa makali ya kubadili nywele mtu havai gloves anamsugua kwa vidole tupu na makucha hata kama gloves zipo anaona zinamchelewesha ufanisi, havai. Kusemasema anakuona kama kero, unajidai atakufa anyway maana maradhi yapo mengi.
 
Mungu atusaidie. Haya ni ya nyongeza ya kumegeana mkate.


________________________________
From: Mashaka Mgeta <mgeta2000@yahoo.com>
To: wanabidii@googlegroups.com
Sent: Sunday, 19 August 2012, 16:48
Subject: Re: [wanabidii] Kula nyama ya nguruwe unaweza kupata kifafa


Ni angalizo zuri INGAWA inawezekana ikawa rahisi kuvumilia maumivu yanayotokana na kuchomwa kwa ncha ya sindano kwenye mboni ya jicho kuliko kuacha kukitumia kitoweo hicho.

Ni mtazamo tu
------------------------------
On Sat, Aug 18, 2012 7:21 AM PDT Augustino Chengula wrote:

>Kwa wale wanofuga nguruwe, wanaokula kiti moto lakini na wale
>wasiohusika na lolote kati ya hayo bado wanaweza kupata ugonjwa
>unatokana na minyoo wanaoitwa tegu (tapeworm) unaoweza kukupelekea
>kuwa na kifafa. Kwa muda mrefu watu wameamini ndugu zao wenye kifafa
>wamelogwa au wameurithi, wengi hawajajua kuwa unaweza kupata ugonjwa
>wa kifafa kwa kula nyama ya nguruwe ikiwa mbichi au haijapikwa vizuri
>(kitimoto jina maarufu nyakati hizi za sasa) yenye lava wa tegu.
>Lakini pia kula mboga za majani zisizooshwa vizuri au kupikwa vizuri.
>Kwa kujielimisha zaidi soma hapa http://achengula.blogspot.com/
>--
>
>
>
>
>*To all the questions of your life YOU are the  most possible answer. To
>all the problems of your life YOU are the best solution. Trust yourself*
>
>--
>Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
>Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
>Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/
>
>Kujiondoa Tuma Email kwenda
>wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
>
>Disclaimer:
>Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
>
>

--
Karibu Jukwaa la http://www.mwanabidii.com/
Pata nafasi mpya za Kazi http://www.kazibongo.blogspot.com/
Blogu ya Habari na Picha http://www.patahabari.blogspot.com/

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com  Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 

--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 
--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 



--
Karibu Jukwaa la www.mwanabidii.com
Pata nafasi mpya za Kazi www.kazibongo.blogspot.com
Blogu ya Habari na Picha www.patahabari.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
 
 

0 comments:

Post a Comment